Jumatano, 17 Oktoba 2018

85. Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo

85. Maneno Ya Mungu Ni Ukweli Usiobadilika Milele

I
Maneno ya Mungu ni ukweli, yasiobadilika milele.
Mungu ndiye mtoaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Thamani na maana ya maneno Yake yanabainishwa na kiini chao,
sio kama mwanadamu anayakubali ama kuyatambua.
Hata kama hakuna mwanadamu ulimwenguni anayepokea maneno Yake,
thamani yao na usaidizi kwa mwanadamu hayapimiki.
Maneno ya Mungu ni ukweli, yasiobadilika milele.
Mungu ndiye mtoaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
II
Kwa wale wanaoasi, kupinga na kutoheshimu maneno Yake,
Jibu pekee la Mungu kwao ni hili:
Acha muda na ukweli uwe shahidi Wake,
uonyeshe maneno Yake ni ukweli, njia na uzima;
uonyeshe kuwa yote Aliyosema ni kweli,
ni kile ambacho mwanadamu anafaa kuwa nacho na kufuata.
Maneno ya Mungu ni ukweli, yasiobadilika milele.
Mungu ndiye mtoaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
III
Kwa wale wote wanaomfuata Mungu atawaruhusu kuona ukweli huu:
Wale ambao hawakubali maneno Yake ama kuyatekeleza katika matendo yao,
na wale ambao hawawezi kugundua kusudi ama wanaokosa kupata wokovu katika maneno Yake,
hawa watu wote ni wale ambao maneno ya Mungu yamewalaani.
Wamepoteza wokovu wa Mungu.
Kutoka kwao, adhabu Yake haitakaa mbali kamwe.
Maneno ya Mungu ni ukweli, yasiobadilika milele.
Mungu ndiye mtoaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
Maneno ya Mungu ni ukweli, yasiobadilika milele,
Mungu ndiye mtoaji wa uzima, na kiongozi pekee wa mwanadamu.
kutoka kwa "Unapaswa Kuzingatia Matendo Yako" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni