Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Siku-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Siku-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 20 Oktoba 2018

Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini na Saba


Leo, maneno ya Mungu yamefikia kilele chake, ambako ni kusema, sehemu ya pili ya enzi ya hukumu imefikia kilele chake. Lakini sio kilele cha juu kabisa. Wakati huu, sauti ya Mungu imebadilika, si ya kudhihaki wala ya ucheshi, na haigongi au kulaani; Mungu ametuliza sauti ya maneno Yake. Sasa, Mungu anaanza "kubadilishana maoni" na mwanadamu. Mungu anaendeleza kazi ya enzi ya hukumu na pia kufungua njia ya sehemu inayofuata ya kazi, ili sehemu zote za kazi Yake zipatane. Kwa upande mmoja, Anasema kuhusu "ukaidi na uhalifu sugu wa mwanadamu," na kwa upande mwingine, Anasema "katika furaha na huzuni ya kutengana na kuunganika Kwangu na mwanadamu"— vyote viwili vinachochea mjibizo katika mioyo ya watu, na hata vinawasisimua walio sugu zaidi kati yao.

Jumatatu, 27 Novemba 2017

Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?

 Umeme wa Mashariki,  Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?


Mwenyezi Mungu alisema,Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati.