Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo majaribio. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo majaribio. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 12 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Nne


Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu
Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo?

Alhamisi, 11 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Tatu


Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu
Kabla ya kuwa na mitazamo au hitimisho zako binafsi, unafaa kwanza kuelewa mwelekeo wa Mungu kwako, kile ambacho Mungu anafikiria, na kuamua kama kufikiria kwako ni sahihi au la. Mungu hajawahi kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya mtu, na Hajawahi kutumia kiwango cha mateso yaliyovumiliwa na mtu katika kuasisi matokeo yake.

Jumatatu, 24 Desemba 2018

4. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

4. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Majaribio na Utakasaji

Maneno Husika ya Mungu:
Majaribu haya yanailenga hali gani ya ndani ya watu? Yanalenga tabia ya uasi ndani ya watu ambayo haiwezi kumridhisha Mungu. Kuna mengi ambayo ni machafu ndani ya watu, na mengi ambayo ni ya unafiki, na kwa hivyo Mungu anawatia katika majaribu ili kuwasafisha. ...

Alhamisi, 13 Desemba 2018

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Unapaswaje Kuitembea Hatua ya Mwisho ya Njia

Sasa mko kwenye hatua ya mwisho ya njia, na hii ni sehemu muhimu. Labda umevumilia mateso mengi kabisa, umefanya kazi nyingi, umetembea barabara nyingi, na umesikiliza mahubiri mengi, na haijakuwa rahisi kufika hadi sasa. Ikiwa huwezi kuvumilia mateso yaliyo mbele yako na kama unaendelea kama ulivyofanya zamani, basi huwezi kufanywa mkamilifu. Hii si ili kukutisha—huu ni ukweli. Baada ya Petro kupitia kazi ya Mungu kiasi fulani, alipata umaizi na ufahamu mwingi.