Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumtumikia-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumtumikia-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 21 Julai 2019

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao kwa Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako. Ukifika mahali hapo utafurahia kujua imani katika Mungu ni nini, namna ya kumwamini Mungu vizuri, na kile unachopaswa kufanya ili kutenda mambo kwa upatanifu na mapenzi ya Mungu.

Ijumaa, 19 Julai 2019

Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni.

Ijumaa, 6 Julai 2018

Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, kumtumikia Mungu,

Usitafute Mbinu Mpya Unapomtumikia Mungu

Heyi   Mji wa Zhuanghe, Mkoa wa Liaoning
Nilikuwa nimepandishwa cheo tu kuchukua jukumu la kiongozi wa kanisa. Lakini baada ya kipindi cha kazi ngumu, sio tu kuwa kazi ya kiinjili ilikuwa bila uhai kiasi, lakini ndugu zangu wa kiume na wa kike katika timu ya kiinjili walikuwa pia wakiishi katika hali hasi na ya udhaifu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, sikuweza tena kudhibiti hisia zangu. Ni vipi tena ningeweza kuiamsha kazi ya kiinjili? Baada ya kupiga ubongo wangu, hatimaye nilifikiria suluhisho zuri: Kama ningefanya sherehe ya kila mwezi kwa timu ya kiinjili na kuwachagua watu waliojipambanua na wahubiri wa kielelezo, yeyote ambaye angeshinda roho zaidi kwa ajili ya Mungu angepewa thawabu, na yeyote ambaye angeshinda roho chache angeonywa.

Alhamisi, 5 Julai 2018

Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, kumtumikia Mungu,

Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

Ding Ning Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong
Katika siku chache zilizopita, kanisa limepanga mabadiliko katika kazi yangu. Nilipopokea wajibu huu mpya, niliwaza, "Ninahitaji kuchukua fursa hii ya mwisho kuita mkutano na ndugu zangu wa kiume na wa kike, niongee nao wazi juu ya mambo, na niwaache na picha nzuri." Kwa hiyo, nilikutana na mashemasi kadhaa, na kufikia mwisho wa wakati wetu pamoja, nikasema, "Nimeulizwa kuondoka hapa na kuenda kwa kazi tofauti. Natumaini mtamkubali kiongozi ambaye anakuja kuchukua nafasi yangu na kufanya kazi pamoja naye kwa moyo mmoja na wazo moja." Mara tu waliposikia nikisema maneno haya, baadhi ya dada waliokuwepo walipauka, na tabasamu zikawatoka nyusoni.

Jumatano, 7 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Njia… (1)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Roho Mtakatifu,
Njia… (1)


Umeme wa Mashariki | Njia… (1)


Mwenyezi Mungu alisema, Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi ataenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa ambayo atapata mara kwa mara. Kwa wengine ni katika kazi yao, kwa wengine ni katika matazamio yao ya siku za baadaye, kwa wengine ni katika familia yao ya asili, na kwa wengine ni katika ndoa yao. Lakini kilicho tofauti nayo ni kwamba leo sisi, kundi hili la watu, tunateseka kwa ajili ya neno la Mungu. Yaani, kama mtu anayemtumikia Mungu, amekutana na vipingamizi katika njia ya kuamini katika Yeye, na hii ni njia ambayo waumini wote hufuata na ni njia iliyo chini ya miguu yetu yote. Ni kutoka katika kipengele hiki ndipo tunaanza rasmi mwendo wetu wa kuamini katika Mungu, kuanza maisha yetu kama binadamu, na kuingia katika njia sahihi ya maisha.