Umeme wa Mashariki | Kazi na Kuingia (4)
Mwenyezi Mungu alisema, Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani. “Wanajificha wenyewe katika unyenyekevu.” Ukweli ni kwamba, ni wachache miongoni mwenu mnaojua makusudi ya Mungu kuhusu siku za mwisho. Ni wachache sana miongoni mwenu wanaojua nyayo za Mungu, na wachache zaidi wanajua utimilifu wa mwisho wa Mungu utakavyokuwa. Halafu kila mtu, kwa utashi tupu, anakubali kufundishwa nidhamu na kushughulikiwa na wengine, kana kwamba wanajitayarisha[1] na kusubiri siku ambayo hatimaye wamekwishaifanya na wanaweza kustarehe. Sitatoa maoni yoyote juu ya “maajabu” haya miongoni mwa watu, lakini kuna hoja moja ambayo wote mnapaswa kuielewa. Kwa sasa watu wengi wanaelekea katika hali isiyo ya kawaida,[2] hatua zao za kuingia tayari zinaelekea mwisho kabisa.[4] Pengine watu wengi wanafikiri kwamba mwanadamu anatamani “Shangri-La” (‘bonde la utulivu’), wakiamini kuwa ni “sehemu ya uhuru.” Kimsingi, sivyo ilivyo. Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekwishapotoka tayari. Lakini bila kujali kile watu wanachokifanya, bado Nahitaji kuzungumza juu ya kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia ndani. Ustahilifu na kasoro za umati sio mada ya msingi ya majadiliano haya. Natumaini kwamba ndugu wote wataweza kupokea maneno Yangu kabisa na kwa usahihi na sio kuelewa visivyo nia Yangu.

