Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neema-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Neema-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 25 Mei 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu Sehemu ya Tano


Aina Tano za Watu
Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika kategoria mbalimbali, kulingana na ufahamu wao wa Mungu na ufahamu wao na kile wamepitia kuhusiana na tabia ya haki Yake, ili muweze kujua awamu ambayo kwa sasa mnapatikana ndani pamoja na kimo chenu cha sasa. Kuhusiana na maarifa yao ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, awamu na kimo tofauti ambavyo watu huwa navyo vinaweza kugawanywa katika aina tano.

Jumatano, 13 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 73

Matamshi ya Mwenyezi MunguSura ya 73

Maneno Yangu yanatimizwa mara tu yanaposemwa; hayabadiliki kamwe na ni sahihi kabisa. Kumbuka hili! Kila neno na kirai kutoka katika kinywa Changu lazima yafikiriwe kwa uangalifu. Kuwa makini zaidi, usije ukapitia upotezaji na kupokea hukumu Yangu, ghadhabu Yangu na moto Wangu pekee. Kazi Yangu sasa inasonga kwa haraka sana, lakini ni safi na ni ya kutaka uangalifu mkubwa hadi kwa kiasi fulani—karibu haionekani kwa jicho tupu na haiwezi kuguswa na mikono ya mwanadamu. Ni ya kutaka uangalifu mkubwa hasa. Maneno Yangu si matupu kamwe na yote ni ya kweli.

Jumamosi, 10 Novemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu"
Mwenyezi Mungu anasema, "Wale Ninaosema wanampinga Mungu ni wale wasiomjua Mungu, wale wanaokiri Mungu na maneno matupu ilhali hawamjui, wale wanaomfuata Mungu lakini hawamtii, na wale wanaofurahia neema ya Mungu lakini hawawezi kumshuhudia. Bila ufahamu wa madhumuni ya kazi ya Mungu na kazi ya Mungu kwa mwanadamu, mwanadamu hawezi kuwa katika ulinganifu na moyo wa Mungu, na hawezi kumshuhudia Mungu. Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu."

Jumamosi, 10 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Njia... (8)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Roho Mtakatifu,

Umeme wa Mashariki | Njia... (8)

Umeme wa Mashariki | Njia... (8)

Mwenyezi Mungu alisema, Wakati ambapo Mungu anakuja duniani kuchanganyika na wanadamu, kuishi nao, sio tu kwa siku moja au mbili. Labda kwa wakati huu wote watu wamemjua Mungu kwa kiwango fulani, na labda wamepata utambuzi muhimu wa kumhudumia Mungu, na wamepata uzoefu sana katika imani yao katika Mungu. Hata iweje, watu wanaelewa vizuri sana tabia ya Mungu, na maonyesha ya kila aina ya tabia za binadamu yanatofautiana kwa kweli. Jinsi Nionavyo, maonyesho tofautitofauti ya watu yanatosha kwa Mungu kuyatumia kama sampuli, na shughuli zao za fikira zinatosha kwa Yeye kurejelea.

Alhamisi, 8 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Njia… (4)

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, neema,
Njia… (4)

Njia… (4)


Mwenyezi Mungu alisema, Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu. Kila Nifikiriapo juu ya hili Mimi huhisi kwa uthabiti kupendeza kwa Mungu. Ni kweli kwamba Mungu anatupenda. La sivyo, nani angeweza kutambua kupendeza Kwake? Ni kutoka tu kwa hili ndio Naona kwamba kazi hii yote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu. Natoa shukrani kwa Mungu kwa hili, na Ningependa ndugu na dada Zangu wajiunge na Mimi kumsifu Mungu:

Ijumaa, 29 Desemba 2017

Umeme wa Mashariki | Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri | kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

 Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, hukumu,
 Umeme wa Mashariki | Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

2. Umeme wa Mashariki | Kuona Uhalisi Wangu Kwa Dhahiri

Xiaoxiao Jijini Xuzhou, Mkoani Jiangsu
Kwa sababu ya mahitaji ya kazi ya kanisa, nilihamishwa mpaka mahali pengine ili kutimiza wajibu wangu. Wakati huo, kazi ya injili mahali pale ilikuwa katika hali duni, na hali ya akina kaka na dada kwa kawaida haikuwa nzuri. Lakini kwa kuwa nilikuwa nimeguswa na Roho Mtakatifu, bado nilijitwisha kila kitu nilichoaminiwa nacho kwa matumaini kamili. Baada ya kukubali kuaminiwa, nilihisi uwajibikaji kamili, kupata nuru kamili, na hata nikafikiri kwamba nilikuwa na uamuzi kiasi fulani. Niliamini kuwa nilikuwa na uwezo na ningeweza kutekeleza kazi hii vizuri. Kwa kweli, wakati huo sikuwa na maarifa kabisa ya kazi ya Roho Mtakatifu au ya asili yangu mwenyewe. Nilikuwa naishi kabisa katika kujiridhisha na kujitamani.