Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu;
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo VITABU. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo VITABU. Onyesha machapisho yote
Jumapili, 29 Desemba 2019
Jumamosi, 28 Desemba 2019
Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.
Ijumaa, 27 Desemba 2019
Sura ya 21
Mwanadamu huanguka katikati ya mwanga Wangu, na anasimama imara kwa sababu ya wokovu Wangu. Niletapo wokovu ulimwenguni kote, mwanadamu hujaribu kutafuta njia za kuingia miongoni mwa mtiririko wa urejesho Wangu, ilhali kuna watu wengi ambao huoshwa wasijulikane waliko na gharika hili la urejesho; kuna watu wengi ambao wamezama na kumezwa na mafuriko haya ya maji; na kuna watu wengi pia ambao husimama imara huku kukiwa na mafuriko, ambao hawajawahi kupoteza hisia zao za mwelekeo, na ambao basi wamefuata mafuriko mpaka sasa. Ninaenda hatua kwa hatua na mwanadamu, lakini yeye hajawahi kunitambua; yeye anajua tu nguo Ninazovaa kwa nje, na hajui utajiri uliofichika ndani Mwangu. Ingawa Mimi humruzuku mwanadamu na kumpa kila siku, hana uwezo wa kukubali kwa kweli, hana uwezo wa kupokea utajiri wote niliompa. Hakuna jambo lolote kuhusu upotovu wa mwanadamu ambalo huniepuka;
Jumanne, 24 Desemba 2019
Jua madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu
Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.
Jumatatu, 23 Desemba 2019
Sura ya 20
Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana.
Jumamosi, 21 Desemba 2019
Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).
“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1).
Maneno Husika ya Mungu:
Ijumaa, 20 Desemba 2019
Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu” (Yohana 1:1-2).
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6).
“Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai” (Yohana 6:63).
Alhamisi, 19 Desemba 2019
Sura ya 19
Ni wajibu wa mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kuuliza matata, kutafuta maangamizo yake mwenyewe. Binadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu badala, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha. Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda michango ya mwanadamu, lakini Nachukia madai yake.
Jumatatu, 16 Desemba 2019
Sura ya 18
Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oo, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope! Ah, Mambo mengi ya uumbaji Ninayoyashikilia mikononi Mwangu! Wanawezaje, kukosa kufanywa upya, kupitia maneno Yangu?
Jumapili, 15 Desemba 2019
Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. Naye atahukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi: nao wata, nao watafua panga zao ili ziwe majembe, na mikuki yao ili iwe mundu: hakuna taifa litakaloinua upanga dhidi ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena. Enyi wa nyumba ya Yakobo, njooni, tutembee katika nuru ya Yehova” (Isaya 2:2-5).
Jumamosi, 14 Desemba 2019
Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu. Kama ninyi mngelinijua, pia mngelimjua Baba yangu: na kuanzia sasa mnamjua, na mmemwona” (Yohana 14:6-7).
Jumanne, 10 Desemba 2019
Nikiongozwa na Maneno ya Mungu, Nilishinda Ukandamizaji wa Nguvu za Giza
Na Wang Li, Mkoa wa Zhejiang
Nilimwamini Bwana Yesu pamoja na mama yangu tangu nilipokuwa msichana mdogo; katika siku zangu za kumfuata Bwana Yesu, mara nyingi niliguswa na upendo Wake. Nilihisi kwamba Alitupenda sana hata Akasulibiwa na kumwaga kila tone la damu Yake ili kutukomboa. Wakati huo, ndugu katika kanisa letu wote walikuwa wenye upendo na wenye kusaidiana, lakini kwa bahati mbaya imani yetu katika Bwana ilikutana na mateso na kukandamizwa mikononi mwa serikali ya CCP.
Jumatatu, 9 Desemba 2019
Sura ya 17
Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani.
Jumamosi, 7 Desemba 2019
Sura ya 16
Kuna mengi ambayo Natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine. Lakini Simwangamizi mwanadamu kwa ajili ya ukosefu wake wa nguvu, wala Siudhiki na udhaifu wake. Naifanya kazi Yangu tu, na kuongea jinsi ambavyo Nimefanya, hata kama mwanadamu haelewi matakwa Yangu; siku itakapokuja, watu watanijua ndani kabisa ya nyoyo zao, na watanikumbuka katika mawazo yao.
Jumanne, 3 Desemba 2019
Sura ya 15
Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika.
Jumapili, 1 Desemba 2019
Wimbo wa Maneno ya Mungu Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote
I
Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia,
unaanza kutenda wajibu wako.
Katika mpango na utaratibu wa Mungu,
unachukua nafasi yako,
na unaanza safari ya maisha.
Vyovyote vilivyo msingi wako
ama safari iliyo mbele yako,
hakuna anayeweza kuepuka utaratibu
na mpango ambao Mbingu imeweka,
na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake,
kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote
ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.
Jumamosi, 30 Novemba 2019
Sura ya 14
Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, binadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme.
Alhamisi, 28 Novemba 2019
Sura ya 13
Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje, bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu. Hata ingawa Nimeyaweka maneno Yangu wazi, kuna yeyote aliyeelewa? Nilitoka Sayuni Nikaja miongoni mwa wanadamu.
Jumanne, 26 Novemba 2019
Sura ya 12
Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangazwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya asili, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya.
Jumamosi, 23 Novemba 2019
Sura ya 11
Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)












