Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 5 Agosti 2018

Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mapenzi ya Mungu,

Sura ya 12. Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana

1. Usijishughulishe na Ikiwa Umejaaliwa na Mungu, bali Ujishughulishe na Ufuatiliaji Wako
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi hawaelewi mapenzi ya Mungu; wanafikiri kuwa kila mtu ambaye ameamuliwa na Mungu ataokolewa bila kuepuka na wanafikiri kuwa kila mtu asiyeamuliwa na Mungu hataokolewa hata wakiyafanya mambo vyema zaidi. Wanafikiri kwamba Mungu hataamua matokeo ya watu kulingana na utendaji na tabia yao. Iwapo unafikiri hivi, basi unamwelewa Mungu visivyo kabisa. Iwapo Mungu angefanya hili kweli, basi Mungu angekuwa mwenye haki? Mungu huamua matokeo ya watu kulingana na kanuni: Mwishowe matokeo ya watu yataamuliwa kulingana na utendaji wao wa kibinafsi na tabia.

Jumamosi, 30 Juni 2018

Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisema, Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli; hii inamaanisha kuwa watakumbana na matatizo fulani. Je, mnaweza kusema kuwa yule ambaye hatendi ukweli amewahi kuutafuta ukweli? Hajautafuta kabisa! Fikira zake binafsi hutokea: “Njia hii ni nzuri, ni kwa faida yangu.” Mwishowe, bado anatenda kulingana na mawazo yake binafsi. Hatafuti ukweli kwa sababu kuna kitu kisicho sawa na moyo wake, moyo wake hauko sawa.

Ijumaa, 29 Juni 2018

Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Umuhimu na Mazoezi ya Sala

Mwenyezi Mungu alisema, Je, mnaomba vipi kwa sasa? Ni maendeleo kwa sala za kidini jinsi gani? Mnaelewa nini hasa kuhusu umuhimu wa sala? Je mmechunguza maswali haya? Kila mtu ambaye hafanyi sala ako mbali na Mungu, kila mtu ambaye hasali anafuata mapenzi yake; Kukosekana kwa sala kunaashiria kwenda mbali na Mungu na usaliti wa Mungu. Ni nini uzoefu wenu hasa na sala? Sasa hivi, kazi ya Mungu tayari inakaribia mwisho na uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu unaweza kuonekana kutoka kwa maombi ya mwanadamu. Je wewe hutenda vipi wakati watu walio chini yako wanakurai na kukupa sifa kwa matokeo unayozalisha katika kazi yako? Je wewe hutenda vipi wakati watu wanakupa mapendekezo? Je, wewe huomba mbele ya Mungu? Mnasali wakati mna mambo na matatizo, lakini je, mnasali wakati hali zenu ni nzuri, au wakati mnahisi mmekuwa na mkutano wa mafanikio? Kwa hivyo wengi wenu huwa hamsali!

Alhamisi, 28 Juni 2018

Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, na mazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia. Iwapo umetambua jinsi ya kupata uzoefu katika hali zote, muktadha na mazingira, bila kushindwa hata kwenye mazingira ya kuchukiza zaidi, na iwapo katika mazingira mazuri kabisa na ya kustarehesha kabisa na katika hali za majaribu makubwa kabisa, haupotoshwi au kudanganyika na katu hauanguki, basi utakuwa umepiga hatua na kuzidisha kimo. Je, yote haya yaweza kuchukuliwa kama wokovu? Kwa hakika, bado haujaokolewa. Lakini angalau, mazingira yako hayawezi kushawishi imani yako kwa Mungu au kusadiki kwako kwa Mungu, na unao msingi.

Jumapili, 22 Aprili 2018

Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata

1. Kama hali ya Watu Ni Ya Kawaida Inategemea na Kama Wanapenda Ukweli au La
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wengi wameibua suala lifuatalo: Baada ya ushirika wa juu, wanahisi wazi kabisa, wanakuwa na nguvu zaidi, na hawana hisia hasi—lakini hali kama hiyo inabaki tu kwa karibu siku kumi, ambapo baadaye hawawezi kudumisha hali ya kawaida. Suala ni nini? Je mmewahi kujiuliza kinachosababisha hili? Mbona hali zenu ni nzuri sana katika siku hizo takriban kumi za kwanza? Wengine wanasema kuwa hili ni tokeo la kutolenga ukweli. Lakini hivyo ungeweza vipi kufikia kiwango hiki cha kawaida baada ya kusikia ushirika? Mbona ulikuwa na furaha sana baada ya kuusikia ukweli? Wengine wanasema ni kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Mbona basi kazi ya Roho Mtakatifu inakoma baada ya takriban siku kumi? Wengine husema ni kwa sababu wanakuwa wazembe na kuacha kusonga mbele na juu. Mbona basi hili linafanyika hata wakati watu wanapojaribu kufanya maendeleo? Mbona Roho Mtakatifu pia hafanyi kazi? Je, hukuwa unajaribu kusonga mbele na juu? Basi mbona Roho Mtakatifu hayuko kazini?

Jumamosi, 21 Aprili 2018

Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo

Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo

Mwenyezi Mungu alisema, Punde tu watu wanapokuwa na haraka wakati wakiutumiza wajibu wao, hawajui jinsi ya kuuzoea; punde tu wanaposhughulika na mambo, hali yao ya kiroho inakuwa na matatizo; hawawezi kudumisha hali yao ya kawaida. Inawezekanaje kuwa hivi? Unapoombwa kufanya kazi kidogo, haufuati ukawaida, unakosa mipaka, husogei karibu na Mungu na unajitenga mbali na Mungu. Hili linadhibitisha kwamba watu hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu. Haidhuru nini ufanyacho, unapaswa kwanza kuelewa halisi kwa nini unalifanya hili na asili ya jambo hili ni lipi. Ikiwa imepangwa kama kutimiza wajibu wako, basi unapaswa kutafakari: Nitalifanyaje hili? Nitatimizaje wajibu wangu vyema ili nisiwe nafanya kwa uzembe? Hili ni jambo ambalo kwalo unapaswa kusogea karibu na Mungu. Kusogea karibu na Mungu ni kutafuta ukweli katika jambo hili, ni kutafuta jinsi ya kutenda, ni kutafuta mapenzi ya Mungu, na ni kutafuta jinsi ya kumridhisha Mungu. Hizi ndizo njia za kusogea karibu na Mungu unapofanya vitu; sio kufanya sherehe za kidini au tendo lionekanalo kwa nje; inafanywa kwa kusudi la kutenda kulingana na kweli baada ya kufauta mapenzi ya Mungu.