Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo imani-katika-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo imani-katika-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 17 Agosti 2019

Unajua Nini Kuhusu Imani?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Ndani ya binadamu, kunalo neno lisilokuwa la uhakika, ilhali binadamu hajui imani inajumuisha nini, na vilevile hajui ni kwa nini anayo imani. Binadamu huelewa kidogo sana, na binadamumwenyewe amepungukiwa sana; yeye anakuwa tu na imani ndani Yangu bila kujali na bila kujua. Ingawa hajui imani ni nini wala ni kwa nini anayo imani ndani Yangu, anaendelea kufanya hivyo kwa shauku mno. Kile Ninachomwomba binadamu, si tu yeye kuniita Mimi kwa shauku kwa njia hii au kuniamini Mimi kwa mtindo huu wa kukosa mwelekeo. Kwani kazi Ninayoifanya ni yake binadamu kunijia Mimi na kunijia Mimi, wala si kwa binadamu kuvutiwa na kuniangalia Mimi kwa njia mpya kwa sababu ya kazi Yangu.

Jumamosi, 20 Julai 2019

Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Maisha ya kanisa

Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watiifu kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru.

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu.

Jumamosi, 9 Juni 2018

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli


Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli

Mwenyezi Mungu alisema, Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, na kwa kiwango cha chini zaidi hawaijui kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa makini kwa kuwa kuamini katika Mungu ni jambo geni, jambo lisolo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu. Kwa maneno mengine, ikiwa watu hawamjui Mungu, hawajui kazi Yake, basi hawafai kwa matumizi na Mungu, na zaidi ya hayo hawawezi kutimiza hamu ya Mungu.

Alhamisi, 10 Mei 2018

"Imani katika Mungu" (6) - Imani ya Kweli katika Mungu Inamaanisha Nini?


"Imani katika Mungu" (6) - Imani ya Kweli katika Mungu Inamaanisha Nini?


Utambulisho


Watu wengi wanaamini kwamba imani katika Mungu ni imani katika Biblia, na kwamba kumfanyia Bwana kazi kwa bidii ni uhalisi wa kuamini katika Mungu. Hakuna mtu katika ulimwengu wa dini ana uwezo wa kuelewa kabisa imani ya kweli katika Mungu ina maana gani. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Imani katika Mungu’ inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu sio sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni hali ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini.

Alhamisi, 16 Novemba 2017

Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?


Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu,

Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?


Mwenyezi Mungu alisema, Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushirikiane  kuhusu mada ya kumfuata Mungu.