Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mambo-Muhimu-ya-Muumini-Mpya. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mambo-Muhimu-ya-Muumini-Mpya. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 14 Septemba 2018

1. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

1. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

Maneno Husika ya Mungu:
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumkamilisha binadamu, na kumwondoa binadamu.

Jumamosi, 8 Septemba 2018

4. Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

4. Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu.

3. Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

3. Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

Jumanne, 7 Agosti 2018

Mwenyezi Mungu Ndiye Yesu Aliyerudi

Sura ya 1 Lazima Ujue Kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Mbingu na Dunia na Kila kitu Ndani Yao

2. Mwenyezi Mungu Ndiye Yesu Aliyerudi.

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu Anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajiachilii mbali. Mtu anaweza kusema kwamba inaonekana kama hatua hii ya kazi Yake inafanyika mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua.

Ijumaa, 27 Julai 2018

Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote. | Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

Sura ya 1 Lazima Ujue Kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Mbingu na Dunia na Kila kitu Ndani Yao

1. Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote.

Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

Alhamisi, 26 Julai 2018

1. Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote

Sura ya 1 Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Ambaye Aliumba Kila kitu

1. Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu Mmoja wa Kweli Anayetawala Juu ya Vitu Vyote

Maneno Husika ya Mungu:
Yote yaliyo duniani humu yanabadilika haraka sawasawa na mawazo ya Mwenye uweza, na chini ya macho Yake. Mambo ambayo wanadamu hawajawahi kuyasikia yanaweza kuja kwa ghafla, ilhali vitu ambavyo wanadamu wamemiliki kwa muda mrefu vinaweza kutoweka bila wao kujua. Hakuna anayeweza kutambua mahali alipo Mwenye uweza sembuse yeyote kuweza kuhisi kuzidi uwezo wa mwanadamu na ukuu wa nguvu za uzima za Mwenye uweza. Anazidi uwezo wa mwanadamu kwa vile Anavyoweza kufahamu yale ambayo wanadamu hawawezi. Yeye ni mkuu kwa vile ni Yeye anayekataliwa na wanadamu na bado Anawaokoa wanadamu.