Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kazi-ya-kanisa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kazi-ya-kanisa. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 5 Januari 2019

2. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Ile ya Pepo Wabaya

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

2. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Ile ya Pepo Wabaya

Maneno Husika ya Mungu:
Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake ya kishetani na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli.