Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambapo watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo Zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu dunia katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza moyo Wangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu. Kama sehemu kubwa ya maneno Yangu haingeelekezwa kwa udhaifu wa mwanadamu, angejigamba na kutia mambo chumvi, na angehubiri na kubuni nadharia zenye kuvutia, ni kama aliye na maarifa yote na anayejua yote kuhusu masuala duniani. Nani bado anathubutu kujigamba kati ya wale waliokuwa waaminifu Kwangu hapo awali, na ni nani ambaye leo hii anasimama imara mbele Yangu? Ni nani asiyefurahia matarajio yake mwenyewe kisiri?
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho-Chaguzi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho-Chaguzi. Onyesha machapisho yote
Jumanne, 12 Novemba 2019
Ijumaa, 4 Oktoba 2019
Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu
Kila mtu anahisi kuwa usimamizi wa Mungu ni wa ajabu, kwa sababu watu wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu hauna uhusiano wowote na mwanadamu. Wanafikiri kuwa usimamizi wa Mungu ni kazi ya Mungu pekee, shughuli za Mungu, na hivyo wanadamu hawajali kuhusu usimamizi wa Mungu. Kwa njia hii, kuokolewa kwa wanadamu kumekuwa kusiko yakini na kusiko dhahiri, na kumebaki tu maneno matupu. Hata kama mwanadamu anamfuata Mungu ili aokolewe na aingie katika hatima inayopendeza, mwanadamu hajishughulishi na jinsi ambavyo Mungu Hutekeleza kazi Yake. Mwanadamu hashughulishwi na Anachokipanga Mungu na anachopaswa kufanya ili aokolewe.
Alhamisi, 3 Oktoba 2019
Kutanafusi kwa Mwenye Uweza
Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako na kila kitu ambacho mwenye Uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya uchungu isiyokuwa na mwisho, pasipo uwezo wa kukuokoa, hukuna matumaini ya kuishi, umeachwa ukipambana na kuzunguka zunguka tu.…
Jumatano, 2 Oktoba 2019
Maneno ya Mungu | Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu
Kulingana na vitendo na matendo katika maisha yenu, nyote mnahitaji kurasa za maneno ya kuwajaza na kuwajenga kila siku, kwani mko na upungufu mno, na ujuzi na maarifa yenu ya kupokea ni ya hali ya chini sana. Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.
Jumanne, 1 Oktoba 2019
Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani
Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani
Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu.
Jumatatu, 30 Septemba 2019
Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu
Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani. Suala hili si lile ambalo ni geni sana kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo kwenye suala hili.
Jumamosi, 28 Septemba 2019
Maonyo Matatu
Kama muumini wa Mungu, hamfai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla mwisho wenu haujaamuliwa, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. Kabla Sijaendelea, mnafaa kwanza kuelewa yafuatayo: Maneno Ninayoongea ni ukweli unaoelekezwa kwa wanadamu wote, na wala si kwa mtu mahususi au aina fulani ya mtu.
Ijumaa, 27 Septemba 2019
Wewe U Mwaminifu kwa Nani?
Kila siku mnayoiishi sasa ni ya maana sana na muhimu sana kwa hatima yenu na majaliwa yenu, kwa hivyo mnapaswa kufurahia kila mlicho nacho na kila dakika inayopita. Mnapaswa kutumia muda wenu vizuri ili muweze kujinufaisha, ili msije kuishi maisha haya bure. Pengine mnajihisi kukanganyikiwa mnaojiuliza ni kwa nini Ninazungumza maneno haya. Kwa kweli, Sijapendezwa na matendo ya yeyote kati yenu. Kwa maana matumaini ambayo Nimekuwa nayo juu yenu si vile tu mlivyo sasa. Kwa hivyo, Naweza kuelezea hivi: Nyinyi nyote mko hatarini kabisa. Vilio vyenu vya kwanza kwa ajili ya wokovu na matamanio yako ya kwanza ya kufuatilia ukweli na kutafuta nuru vinakaribia mwisho.
Alhamisi, 26 Septemba 2019
Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako
Nimefanya kazi nyingi miongoni mwenu na, ni wazi kwamba, Nimezungumza vizuri pia. Hata hivyo, Nahisi kwamba maneno na kazi Yangu havijatimiza lengo la kazi Yangu ya siku za mwisho. Maana, katika siku za mwisho, kazi Yangu si kwa ajili ya mtu au watu fulani bali ni kwa manufaa ya kufafanua tabia Yangu asilia. Hata hivyo, kutokana na sababu nyingi—pengine ukosefu wa muda au shughuli nyingi za kazi—tabia Yangu haijamwezesha binadamu kunijua hata kidogo. Kwa hivyo, Ninasonga mbele na katika mpango Wangu mpya, kazi Yangu ya mwisho, kufungua ukurasa mpya ili wale ambao wataniona watajipiga kifuani na kuulilia uwepo Wangu bila kukoma.
Jumatano, 25 Septemba 2019
Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele
Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa.
Jumanne, 24 Septemba 2019
Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.
Jumatatu, 23 Septemba 2019
Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?
Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake umeishi maisha ya kawaida tu. Hiyo haijalishi, kwani wewe bado u mfuasi wa Mungu, kwa hivyo tushikiriane kuhusu mada ya kumfuata Mungu. Lakini, lazima Niwakumbushe wote wanaoyasoma maneno haya kwamba neno la Mungu huelekezwa kwa wale wanaomtambua na wale wanaomfuata Mungu, na sio kwa watu wote wa ulimwengu, wakiwemo wale wasiomtambua Mungu.
Jumapili, 22 Septemba 2019
Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo
Nimefanya kazi kubwa miongoni mwa binadamu, na maneno ambayo Nimeeleza wakati huu yamekuwa mengi. Maneno haya ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, na yalikuwa yanaeleza ili binadamu aweze kulingana na Mimi. Ilhali Nimewapokea watu wachache tu duniani ambao wanalingana na Mimi, na hivyo Nimesema kwamba binadamu hathamini maneno Yangu, kwa kuwa binadamu halingani na Mimi. Kwa njia hii, kazi ambayo Naifanya sio tu kwa ajili ya mwanadamu aweze kuniabudu; muhimu zaidi, ni kwa ajili ya mwanadamu aweze kulingana na Mimi.
Ijumaa, 20 Septemba 2019
Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa
Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati yao ni wale wanaohudumu kama makuhani, wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Ninawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu. Moja baada ya mwingine, Ninayaita makundi ya wale Ningependa kuwaokoa kurejea katika nyumba Yangu, kisha Ninawauliza wakubali kazi Yangu katika siku za mwisho. Wakati uo huo, Ninawaainisha wanadamu kulingana na aina, kisha Ninawatunukia au kuwaadhibu kila mmoja kulingana na matendo yake. Hizi ndizo hatua zinazojumuishwa katika kazi Yangu.
Alhamisi, 19 Septemba 2019
Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu
Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo.
Jumatano, 18 Septemba 2019
Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia
Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kuyasikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu anayemfuata Yesu angependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo mtamjua Yesu kweli Atakaporejea? Je, mtaelewa kweli kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali kweli, bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake.
Jumanne, 17 Septemba 2019
Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili)
Wanaopeleka watoto na jamaa zao wasioamini kabisa kanisani ni wachoyo sana na wanaonyesha ukarimu wao. Watu hawa wanasisitiza tu upendo, bila kujali iwapo wanaamini ama iwapo ni matakwa ya Mungu. Wengine wanaleta wake zao mbele ya Mungu, ama kuleta wazazi wao mbele ya Mungu, na bila kujali iwapo Roho Mtakatifu anakubali ama anafanya kazi Yake, kwa upofu “wanawachukua watu wenye vipaji” kwa ajili ya Mungu. Kuna faida gani inayoweza kupatikana kutokana na kueneza ukarimu huu kwa watu hawa wasioamini? Hata kama hawa wasioamini wasio na uwepo wa Roho Mtakatifu wanapambana kumfuata Mungu, bado hawawezi kuokolewa kama mtu anavyodhani wanaweza.
Jumatatu, 16 Septemba 2019
Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza)
Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu. Ilikuwa kwa sababu ya upotovu wa binadamu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake, na ilikuwa pia kwa sababu ya uasi wa malaika mkuu ndipo Mungu alichukuliwa kutoka kwa pumziko Lake.
Jumapili, 15 Septemba 2019
Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili)
Punde tu Shetani anaposhindwa, hivyo ni kusema, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi yake yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani.
Jumamosi, 14 Septemba 2019
Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza)
Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


















