Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Upendo-wa-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Upendo-wa-Mungu. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 26 Desemba 2019

Latest Swahili Gospel Song 2019 "Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa" (Lyrics)



I

Kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu, Atamwongoza;
kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa;
kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfikisha katika hatima sahihi.
Kwa kuwa Alimuumba mwanadamu na Anamsimamia,
ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu.
Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba.
Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu,
mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.

Jumatatu, 23 Desemba 2019

Sura ya 20

Utajiri wa jumba Langu ni bila idadi na usioeleweka, lakini mwanadamu hajawahi kuja Kwangu kuufurahia. Hana uwezo wa kuufurahia mwenyewe, wala wa kujilinda mwenyewe kwa kutumia juhudi zake mwenyewe; badala yake, yeye daima huweka imani yake kwa wengine. Kati ya wale wote Ninaowatazamia, hakuna mtu aliyewahi kunitafuta kwa makusudi na moja kwa moja. Wao wote huja mbele Zangu kwa kushawishiwa na wengine, wakiwafuata watu wengi, na hawana nia ya kulipa gharama au kutumia muda kustawisha maisha yao. Kwa hivyo, miongoni mwa watu hakuna mtu aliyewahi kuishi katika hali halisi, na watu wote huishi maisha yasiyo na maana.

Jumatano, 18 Desemba 2019

Nitampenda Mungu Maisha Yangu Yote | "Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri" (Video Rasmi ya Muziki)


Juu ya miti, nikiukwea mwezi wa amani. Kama mpendwa wangu, wa haki na mzuri.
Ee mpendwa wangu, Uko wapi? Sasa mimi nina machozi. Je, Wanisikia nikilia?
Wewe Ndiwe hunipa upendo. Wewe Ndiwe Unayenitunza.
Wewe Ndiwe unayeniwaza daima, Wewe Ndiwe unayeyatunza maisha yangu.
Mwezi, nyuma ya upande wa pili wa anga. Usimfanye mpendwa wangu asubiri muda mrefu sana.
Tafadhali mwambie Yeye ninamkosa sana.
Usisahau kuubeba pamoja nawe upendo wangu, pamoja nawe upendo wangu.

Jumamosi, 14 Desemba 2019

Kwa nini ni kwa kupitia na kuitii kazi ya Mungu mwenye mwili pekee ndipo mtu anaweza kumjua Mungu?


Aya za Biblia za Kurejelea:

“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu. Kama ninyi mngelinijua, pia mngelimjua Baba yangu: na kuanzia sasa mnamjua, na mmemwona” (Yohana 14:6-7).

Jumamosi, 30 Novemba 2019

Sura ya 14

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu

Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, binadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme. 

Jumanne, 26 Novemba 2019

Sura ya 12

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangazwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya asili, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya. 

Jumamosi, 23 Novemba 2019

Sura ya 11

Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi. Ambayo ni kusema, Nianzapo binafsi kazi Yangu duniani, na wakati enzi ya hukumu inakaribia tamati yake, Naanza kuelekeza maneno Yangu kwa ulimwengu mzima, na kutoa sauti ya Roho Wangu kwa dunia nzima. 

Ijumaa, 22 Novemba 2019

Sura ya 10

Enzi ya Ufalme ni, hata hivyo, tofauti na nyakati za kale. Haihusu kile anachofanya mwanadamu. Badala yake, Mimi binafsi Natekeleza kazi Yangu baada ya kushuka duniani—kazi ambayo wanadamu hawawezi kuelewa wala kufanikisha. Tangu kuumbwa kwa ulimwengu mpaka leo, miaka hii yote daima imehusu kujenga kanisa, lakini hakuna mtu anayesikia kamwe kuhusu kujenga ufalme. Japokuwa Nazungumza kuhusu haya kwa kinywa Changu mwenyewe, yupo yeyote anayejua asili yake? 

Jumanne, 12 Novemba 2019

Sura ya 8

Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambapo watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo Zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu dunia katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza moyo Wangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu. Kama sehemu kubwa ya maneno Yangu haingeelekezwa kwa udhaifu wa mwanadamu, angejigamba na kutia mambo chumvi, na angehubiri na kubuni nadharia zenye kuvutia, ni kama aliye na maarifa yote na anayejua yote kuhusu masuala duniani. Nani bado anathubutu kujigamba kati ya wale waliokuwa waaminifu Kwangu hapo awali, na ni nani ambaye leo hii anasimama imara mbele Yangu? Ni nani asiyefurahia matarajio yake mwenyewe kisiri? 

Ijumaa, 8 Novemba 2019

“Kutoka kwa Kiti cha Enzi Hububujika Maji ya Uzima” – Jinsi ya Kupata Njia ya Uzima wa Milele | Swahili Gospel Movie Clip 8/9

“Kutoka kwa Kiti cha Enzi Hububujika Maji ya Uzima” – Jinsi ya Kupata Njia ya Uzima wa Milele | Swahili Gospel Movie Clip 8/9


Kwa maelfu ya miaka waumini wa Bwana wametaka kupata uzima wa milele, lakini hakuna mtu ambaye ameweza kutimiza matamanio haya. Sasa, umechanganyikiwa kuhusu kama kweli kuna njia ya uzima wa milele au la au umechanganyikiwa juu ya jinsi unavyoweza kufuatilia hili kwa njia ambayo utapata njia ya uzima wa milele? Hii video fupi itakuambia jinsi ya kupata njia ya uzima wa milele.

Alhamisi, 7 Novemba 2019

“Nimewahi Treni ya Mwisho” – Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu | Swahili Christian Movie Clip 6/6

“Nimewahi Treni ya Mwisho” – Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu | Swahili Christian Movie Clip 6/6


Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, Wayahudi walishikilia kwa ukaidi sheria yao na kukataa kukubali kazi ya Bwana Yesu, ambayo iliwafanya waanguke katika giza na kupoteza wokovu wa Mungu. Sasa katika zile siku za mwisho, dunia nzima ya kidini inalinda tu jina la Bwana Yesu na kukataa kumkubali Mwenyezi Mungu, na hivyo kuisababisha kuwa na ukiwa zaidi na zaidi na kuwa jangwa lilisoweza kuzaa matunda. Kwa nini hasa iko hivi?

Jumatano, 6 Novemba 2019

Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)" Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Kwamba Mungu anakimu ulimwengu ina maana na matumizi mapana sana. Mungu hawakimu tu watu kwa kuwapatia mahitaji yao ya kila siku ya chakula na kinywaji, Anawapatia wanadamu kila kitu wanachohitaji, ikiwa ni pamoja na kila kitu ambacho watu wanakiona na vitu ambavyo haviwezi kuonekana. Mungu anatetea, anasimamia na anatawala mazingira ya kuishi ambayo binadamu anahitaji.

Jumapili, 3 Novemba 2019

Filamu za Kikristo 2018 | "Kumbukumbu Chungu" | Welcoming the Return of the Lord in Judgement



Filamu za Kikristo 2018 | "Kumbukumbu Chungu" | Welcoming the Return of the Lord in Judgement

Fan Guoyi alikuwa mzee wa kanisa la nyumba kule Uchina. Wakati wa zaidi ya miaka ishirini ya huduma, siku zote alimwiga Paulo, na kufanya kazi kwa bidii na akamtumikia Bwana kwa shauku kubwa. Aidha, alisadiki kabisa kwamba katika kufuata imani yake kwa njia hii, alikuwa akitenda mapenzi ya Baba wa mbinguni, na kwamba wakati Bwana angerudi, angenyakuliwa kwa hakika na kuenda kwenye ufalme wa mbinguni.

Alhamisi, 31 Oktoba 2019

Sura ya 5

Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? 

Jumatatu, 28 Oktoba 2019

Swahili Christian Musical Drama "Hadithi ya Xiaozhen" | Mungu ni upendo


Xiaozhen alikuwa Mkristo mwenye moyo safi, ulio na huruma, ambaye kila wakati alikuwa akiwashughulikia wenzake kwa uaminifu. Hata hivyo, ilipokuwa ni kwa manufaa yao, marafiki wake wa awali waligeuka na kuwa maadui wake. Baada ya kuteseka kutokana na msiba huu, Xiaozhen alilazimika kuuacha moyo wake wa kweli na kanuni zake za awali. Alianza kuisaliti dhamiri yake mwenyewe iliyo nzuri na roho safi, na kugaagaa katika kinamasi cha ulimwengu mbaya. … Huku akianguka kutoka kwa rehema na kutembea katika njia ya upotovu, alikanyagwa na ulimwengu na kukung'utwa na makovu na vilio. Alikuwa amefika mwisho kabisa, na katika wakati wa kukata tamaa wakati alikuwa amepoteza matumaini yote, mwishowe mwito wa kuaminika wa Mwenyezi Mungu ukauamsha moyo na roho ya Xiaozhen …

Ijumaa, 25 Oktoba 2019

Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV

Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV


Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu”
ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao.
Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure;
Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru,
huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu.
Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake.
Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo,
yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.

Jumatano, 23 Oktoba 2019

Wimbo wa Kanisa Wewe tu Unaweza Kuniokoa Mimi


Wimbo wa Kanisa 

Wewe tu Unaweza Kuniokoa Mimi

  • I
  • Mnyenyekevu na Uliyejificha,
  • Waambatana na watu katika matatizo yao,
  • Ukiwapa njia ya uzima wa milele.
  • Unawapenda binadamu kama mwili Wako mwenyewe.
  • Na Wastahili upendo wao.
  • Afadhali Uteseke Mwenyewe,
  • ili Umwezeshe mwanadamu apate faida.
  • Na Wanyesha uzima juu yao.

Jumanne, 17 Septemba 2019

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Wanaopeleka watoto na jamaa zao wasioamini kabisa kanisani ni wachoyo sana na wanaonyesha ukarimu wao. Watu hawa wanasisitiza tu upendo, bila kujali iwapo wanaamini ama iwapo ni matakwa ya Mungu. Wengine wanaleta wake zao mbele ya Mungu, ama kuleta wazazi wao mbele ya Mungu, na bila kujali iwapo Roho Mtakatifu anakubali ama anafanya kazi Yake, kwa upofu “wanawachukua watu wenye vipaji” kwa ajili ya Mungu. Kuna faida gani inayoweza kupatikana kutokana na kueneza ukarimu huu kwa watu hawa wasioamini? Hata kama hawa wasioamini wasio na uwepo wa Roho Mtakatifu wanapambana kumfuata Mungu, bado hawawezi kuokolewa kama mtu anavyodhani wanaweza.

Jumatano, 21 Agosti 2019

Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile.

Jumapili, 14 Julai 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”

Mwenyezi Mungu anasema, “Wanadamu, walioacha ruzuku ya uzima kutoka kwa mwenye Uweza, hawajui kwa nini wanaishi, na bado wanaogopa kifo. Hukuna usaidizi, hakuna msaada, lakini bado wanadamu wanasita kufumba macho yao, wakiyakabili yote bila woga, wanaendeleza kwa muda mrefu kuishi kwa aibu ulimwenguni humu katika miili isiyokuwa na utambuzi wa nafsi. Unaishi hivyo, pasipo matumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa maumivu na wanatamani sana majilio Yake.