Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Tabia-ya-Haki-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Tabia-ya-Haki-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 28 Julai 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII ” Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu
Mwenyezi Mungu anasema,"Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu.

Ijumaa, 12 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Nne


Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu
Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo?

Ijumaa, 16 Februari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII | (I) Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Biblia,

Mhutasari juu ya Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

(I) Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu. Sasa, ni kitu gani cha msingi tunachokijadili wakati huu? Hebu sote turudi nyuma kidogo katika hoja kuu. Kuhusiana na kumjua Mungu Mwenyewe, yule wa kipekee, sehemu ya kwanza tuliyoijadili ni ipi? (Mamlaka ya Mungu.) Ya pili ilikuwa ni ipi? (Tabia ya haki ya Mungu.)

Alhamisi, 18 Januari 2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II | Tabia ya Haki ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu

Tabia ya Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa vile sasa mumesikiliza kikao cha ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mumejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kushika, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo-upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe. Ufahamu huu ni sehemu moja ya kumjua Mungu. Sehemu ile nyingine ni nini, hivyo basi? Hii ndiyo mada ambayo Ningependa tuweze kushiriki pamoja leo—tabia ya haki ya Mungu.