Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu.
Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini
Mungu aliwaumba wanadamu wote, na amewaongoza wanadamu wote mpaka leo. Hivyo, Mungu anajua yote yafanyikayo miongoni mwa wanadamu: Anajua uchungu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, Anaelewa utamu ulio ndani ya ulimwengu wa mwanadamu, na kwa hiyo kila siku Yeye hufafanua hali za maisha za wanadamu wote, na, zaidi ya hayo, hushughulikia udhaifu na upotovu wa wanadamu wote. Si mapenzi ya Mungu kwamba wanadamu wote watupwe jahanamu, au kwamba wanadamu wote waokolewe. Kila mara huwa kuna kanuni kwa matendo ya Mungu, lakini hakuna anayeweza kuelewa sheria za yote Afanyayo.











