Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo dutu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo dutu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 25 Septemba 2019

Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, ukweli-njia-uzima

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa.

Jumamosi, 21 Septemba 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II Tabia ya Haki ya Mungu” Sehemu ya Pili

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote
Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri
Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu
Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Alhamisi, 19 Septemba 2019

Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kristo

Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na wote hutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mnaweza kuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mmemwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki hata zaidi kwa mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo.

Ijumaa, 13 Septemba 2019

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu Kristo

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu.

Jumatatu, 9 Septemba 2019

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi.

Jumatatu, 2 Septemba 2019

Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, kimsingi, ni kwa kurejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu. Sizungumzii kazi ambayo inatokana na matakwa ya mwanadamu bali kazi ya mitume, watendaji kazi au kaka na dada wa kawaida waliopo katika mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Ijumaa, 30 Agosti 2019

Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu katika Mwili

Ni lazima myafahamu maono ya kazi ya Mungu na mpate mwelekeo wa kazi Yake. Huku ni kuingia kwa njia nzuri. Punde mnapong’amua ukweli wa maono kwa usahihi, kuingia wako utakuwa salama; bila kujali kazi Yake hubadilika kiasi gani, utaendelea kuwa imara moyoni mwako, utakuwa wazi kuhusu maono, na utakuwa na lengo la kuingia na kazi yako. Kwa njia hiyo, tajriba na ufahamu ulio ndani yako utakua kwa kina na kutakaswa zaidi. Punde unapong’amua ukweli wote, hutapoteza kitu maishani na hutapotea. Kama hutazijua hatua hizi za kazi, utapata hasara kwa kila mojawapo.

Jumatano, 14 Agosti 2019

Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Utatu Mtakatifu Upo

Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili.

Jumamosi, 3 Agosti 2019

Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Lazima uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu. Ni muhimu kwamba utendaji uwekwe katika nuru iliyopo na maneno ya Mungu katika siku ya leo. Mungu hafuati masharti, na Anaweza kuzungumza kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ili kufanya wazi hekima Yake na uwezo.

Jumanne, 30 Julai 2019

Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu Kristo

Kwa miaka mingi Roho wa Mungu Amekuwa akitafuta bila kikomo Akifanya kazi duniani. Kwa enzi nyingi Mungu Ametumia wanadamu wengi kufanya kazi Yake. Hata hivyo Roho wa Mungu bado hana mahali pazuri pa kupumzika. Kwa hivyo Mungu hupitia wanadamu mbalimbali kufanya kazi Yake na kwa kiasi kikubwa hutumia wanadamu kufanya hivyo. Yaani, katika miaka hii yote mingi, kazi ya Mungu haijawahi kusimama. Inaendelezwa mbele kupitia mwanadamu, bila kikomo mpaka siku ya leo. Ingawa Mungu Amesema na Ametenda mengi, mwanadamu bado hamjui Mungu, hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kuonekana na mwanadamu na Yeye Hana umbo.

Alhamisi, 18 Julai 2019

Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Binadamu amekuwa akiishi katika funiko la ushawishi wa giza, huku akiwa amezuiliwa bila ya kuachiliwa na ushawishi wa Shetani. Nayo tabia ya binadamu, baada ya kutengenezwa na Shetani, inaendelea kuongezeka kuwa potovu. Mtu anaweza kusema kwamba binadamu huishi daima na tabia yake potovu ya kishetani, asiweze kumpenda Mungu kwa kweli. Kwa sababu ya hili, kama binadamu anataka kumpenda Mungu, lazima anyang'anywe kujidai kwake, kujigamba, kiburi, majivuno, na sifa nyingine kama hizo zinazomilikiwa na tabia ya Shetani.

Ijumaa, 12 Julai 2019

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake Sehemu ya Nne


Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu
Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo?

Jumanne, 25 Juni 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili, angalau, ni lazima liwe ukweli. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. ...

Ijumaa, 21 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Nne


     Hebu turudi kuzungumza kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu. Tumeongea karibuni kuhusu mbinu mbalimbali ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu na ambazo kila mmoja wenu mnaweza kupitia nyinyi wenyewe, kwa hivyo sitatoa maelezo zaidi. Lakini katika mioyo yenu pengine mmechanganyikiwa kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu, ama kwa kiwango cha chini zaidi ana upungufu wa maelezo. Ni ya manufaa kwenu kwa Mimi kuzungumzia hili tena? (Ndiyo.) Je, mnataka kumwelewa? (Ndiyo.) Pengine wengine wenu watauliza: "Mbona tuzungumze kuhusu Shetani tena? Punde tunapoongea kuhusu Shetani, tunakuwa na hasira, na tunaposikia jina lake tunahisi kutotulia kila mahali."

Jumatatu, 17 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Kwanza


Neno la Mwenyezi Mungu|Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu III Sehemu ya Kwanza

Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini mada inayohusiana na kiini cha Mungu katika ushirika wetu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu.

Jumapili, 16 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Nne



  5. Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Mienendo ya kijamii ilianza lini? Je, ni kitu kipya? (La.) Hivyo mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.)

Jumatano, 12 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II Sehemu ya Kwanza


Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu "Upendo Safi Bila dosari.")
1. "Upendo" unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi hautadanganya, kulalamika, kusaliti, kuasi, kushurutisha, au kutafuta kupata kitu au kupata kiasi fulani.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I Sehemu ya Kwanza

Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni cha tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo.

Jumapili, 30 Desemba 2018

1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sura ya 5 Ukweli Kuhusu Mungu Kupata Mwili

1. Mungu Kupata Mwili Ni Nini? Kiini cha Mungu Kupata Mwili Ni Nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu. Maisha Yake ya kimwili na kazi vinaweza kugawanywa katika hatua mbili. Kwanza ni maisha Anayoishi kabla ya kuanza kutekeleza huduma Yake.

Jumapili, 24 Juni 2018

Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu,

Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Qingxin    Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Kuhusu kipengele cha ukweli cha "Mungu ni mwenye haki ", siku zote nilikuwa na ufahamu wa upuuzi kwa kiasi fulani. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa, mtu huyo atakabiliwa na rada, au kupoteza kazi yake au aathiriwe na adhabu. Hiyo ni haki ya Mungu. Kutokana na ufahamu huu usio sahihi, pamoja na hofu ya kupoteza kazi yangu kutokana na kufanya makosa katika kazi yangu, nilifikiria juu ya utaratibu "mjanja":