Kwa nini unamwamini Mungu? Watu wengi wanafadhaishwa na swali hili. Siku zote wana mitazamo tofauti kuhusu Mungu wa vitendo na Mungu wa mbinguni, jambo linaloonyesha kwamba wanamwamini Mungu sio ili wamtii, bali kupata manufaa fulani, au kuepuka mateso ya janga. Wakati huo tu ndipo wanakuwa watiifu kwa kiasi fulani, lakini utii wao ni wa masharti, ni kwa ajili ya matarajio yao wenyewe, na kushinikiziwa. Hivyo: kwa nini unamwamini Mungu? Ikiwa ni kwa ajili ya matarajio yako tu, na majaliwa yako, basi ni bora zaidi usingeamini. Imani kama hii ni kujidanganya, kujihakikishia, na kujishukuru.
Maneno Husika ya Mungu:
Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwake. Yaani, yanahusisha moja kwa moja mitazamo ya mtu kuhusu maisha na maadili yake, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake. Mtu ambaye hawezi kukubali ukweli hatakuwa na mabadiliko katika hali hizi. Ni kwa kupitia kazi ya Mungu pekee, kuingia kikamilifu katika ukweli, kubadili maadili na mitazamo yake kuhusu kuwepo na maisha, kulinganisha msoni yake na ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zake zinaweza kusemekana zimebadilika.











