Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, "Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Iwapo hukumu Yako itaonyesha tabia Yako, na kuruhusu tabia Yako ya haki kuonekana na viumbe wote, na iwapo inaweza kufanya upendo wangu Kwako uwe safi zaidi, ili niweze kufikia mfano wa mwenye haki, basi hukumu Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo.
Mwenyezi Mungu anasema, "Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. ... Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka."




