Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo kutoka-kwa-Mambo-Muhimu-ya-Muumini-Mpya. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 14 Septemba 2018

5. Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumatano, 11 Julai 2018

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

Jumanne, 10 Julai 2018

1. Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?