Jumapili, 13 Januari 2019

3. Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu





Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

3. Katika Kumwamini Mungu, Unapaswa Kuweka Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu. Una uwezo wa kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu kila unapofanya chochote; hata kama huelewi mapenzi ya Mungu, bado ni lazima utimize wajibu na majukumu yako kadri ya uwezo wako. Hujachelewa sana kusubiri mapenzi ya Mungu yafichuliwe kwako na kisha kuyaweka katika vitendo. Wakati uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa juu ya msingi wa maneno ya Mungu. Kupitia katika kula na kunywa maneno ya Mungu, tenda kulingana na mahitaji ya Mungu, weka sawa maoni yako, usitende mambo yanayompinga Mungu au kuingilia kati mambo ya kanisa. Usifanye vitu visivyo na manufaa kwa maisha ya ndugu, usiseme maneno yasiyosaidia wengine, usifanye vitu vya kufedhehesha. Kuwa mwadilifu na mwenye heshima unapofanya mambo yote na kuyafanya ya kupendeza mbele ya Mungu. Hata ingawa kutakuwa na nyakati ambazo mwili ni dhaifu, unaweza kushikiza umuhimu mkubwa kabisa kwa kufaidi familia ya Mungu, kutotamani faida yako mwenyewe, na kutekeleza haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.
kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kila unapofanya chochote, lazima uchunguze iwapo motisha yako ni sahihi. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Hiki ndicho kigezo cha chini zaidi. Iwapo, unapochunguza motisha yako, kunatokea zile zisizo sahihi, na iwapo unaweza kuzikwepa na kutenda kulingana na maneno ya Mungu, basi utakuwa mtu ambaye ni mwema mbele ya Mungu, kitu ambacho kitaonyesha kuwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba kila unachofanya ni kwa ajili ya Mungu, na sio kwa sababu yako binafsi. Ni lazima uuweke moyo wako sawa kila unapofanya ama kusema chochote, uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, au utende kulingana na mapenzi yako: Haya ndiyo maadili ambayo wale wanaoamini katika Mungu wanatenda kulingana nayo. Motisha za mtu na kimo chake vinaweza kufichuliwa katika kitu kidogo, na hivyo, kwa watu kuingia kwa njia ya kufanywa wakamilifu na Mungu, ni lazima kwanza wasuluhishe motisha yao wenyewe na uhusiano wao na Mungu. Ni pale ambapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utaweza kufanywa mkamilifu na Mungu, na ni hapo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, nidhamu, na usafishaji wa Mungu kwako utaweza kupata matokeo yanayotakiwa. Hiyo kusema, watu wanaweza kuwa na Mungu mioyoni mwao, wasitafute maslahi binafsi, wasifikirie kuhusu maisha yao binafsi ya baadaye (ikirejelea kufikiri juu ya mwili), lakini badala yake wanabeba mzigo wa kuingia katika maisha, wanajitahidi wawezavyo kufuatilia ukweli, na kuitii kazi ya Mungu. Kwa namna hii, makusudi unayoyatafuta ni sahihi, na uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Inaweza kusemwa kwamba kuutengeneza uhusiano wako na Mungu ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia kwako katika safari ya kiroho. Ingawa hatima yako iko mikononi mwa Mungu, na imeshaamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na wewe mwenyewe, kwamba unaweza au huwezi kufanywa mkamilifu au kupatwa na Mungu kunategemea na kama uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la. Pengine kuna sehemu ndani yako ambazo ni dhaifu au zenye kutotii—lakini bora tu mtazamo wako wa nje ni sawa na motisha yako ni sahihi, na bora tu umeuweka uhusiano wako na Mungu sawa na kuufanya wa kawaida, basi utafuzu kufanywa mkamilifu na Mungu. Iwapo huna uhusiano sahihi na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili, au familia yako, basi haijalishi kiwango cha kazi unayofanya kwa bidii, itakuwa bure. Iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii chochote kingine, bali anaangalia tu iwapo mitazamo yako kwa kuamini kwa Mungu ni sawa: unayemwamini, ni kwa ajili ya nani unaamini, na ni kwa nini unaamini. Iwapo unaweza kuona vitu hivi kwa udhahiri, na unaweza kuweka mitazamo yako iwe sawa na kuweza kutenda, basi maisha yako yatapiga hatua, na una uhakika wa kuweza kuingia kwenye njia sahihi. Iwapo uhusiano wako na Mungu sio wa kawaida, na mitazamo yako kwa kuamini katika Mungu inakiuka maadili, basi haya yatazuia mengine yote. Haijalishi jinsi unavyoamini katika Mungu, hutafaidi chochote. Iwapo tu uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida ndipo utasifiwa na Mungu unapoupa mwili kisogo, unapoomba, unapoteseka, unapostahimili, unapotii, unapowasaidia ndugu na dada zako, unaweka juhudi zaidi kwa Mungu, na kadhalika.
kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu. Baada tu ya kuutoa moyo wako mzima katika Mungu ndipo utaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho hatua kwa hatua. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu. Mungu hawezi kupata kitu chochote kutoka kwa aina hii ya mtu; aina hii ya mtu anaweza tu kutumika kama foili[a] kwa kazi ya Mungu, kama pambo katika nyumba ya Mungu, kuchukua nafasi, naye hana manufaa—Mungu hamtumii aina hii ya mtu. Katika mtu kama huyo, sio tu kwamba hakuna nafasi kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu, hata zaidi hakuna thamani ya ukamilifu; aina hii ya mtu ni “mfu atembeaye” halisi—hana sehemu ambazo zinaweza kutumika na Roho Mtakatifu—wao wote wametwaliwa na Shetani, kupotoshwa kwa kiwango kilichokithiri na Shetani, ambao ni chombo cha kuondolewa na Mungu. Kwa sasa Roho Mtakatifu hawatumii tu watu kwa kuyaweka maadili yao katika matumizi, lakini pia kuwakamilisha na kubadilisha dosari zao. Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi na sifa za kuhitimu ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi, utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia dosari zako. Unapoutoa moyo wako kwa Mungu, unaweza kuingia kwa undani zaidi kwenye upande mzuri na kuwa kwenye kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa na dosari zako mwenyewe, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na hutakuwa katika hali ya kukaa tu, utaingia ndani kwa utendaji. Hii itamaanisha kuwa wewe ni mtu sahihi.
kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa unataka kuwa na uhusiano wa kufaa na Mungu, lazima moyo wako umgeukie Mungu, na juu ya msingi huu, pia utakuwa na uhusiano wa kufaa na watu wengine. Iwapo huna uhusiano unaofaa na Mungu, haijalishi unachofanya kudumisha uhusiano wako na watu wengine, haijalishi jinsi gani unafanya kazi kwa bidii au ni nguvu kiasi gani unaweka ndani yake, bado ni ya falsafa ya mwanadamu ya maisha. Unadumisha nafasi yako miongoni mwa watu kupitia mtazamo wa mwanadamu na falsafa ya mwanadamu ili kwamba wakupe wewe sifa. Hauundi uhusiano unaofaa na watu kulingana na neno la Mungu. Iwapo hutilii maanani uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano unaofaa na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa unaofaa. Kwa njia hii, uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwanadamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada za binadamu—unawekwa katika matendo kupitia maadili ya neno la Mungu. Je, unayo hiari ya kuwa mwenye kufikiria mapenzi ya Mungu? Je, uko tayari kuwa mtu “bila mantiki” mbele za Mungu? Je, uko tayari kuutoa moyo wako kwa Mungu kabisa, na kutofikiri kuhusu msimamo wako kati ya watu? Kati ya watu wote ambao una mawasiliano nao, ni gani ambao kati yao unayo mahusiano bora zaidi? Wepi kati yao ambao unayo mahusiano mabaya zaidi nao? Je, mahusiano yako na watu ni ya kufaa? Je, unawachukulia watu wote kwa usawa? Je, uhusiano wako na wengine umeimarishwa kwa mujibu wa falsafa yako ya maisha, ama umejengwa kwenye msingi wa upendo wa Mungu? Wakati mtu hautoi moyo wake kwa Mungu, basi roho yake inakuwa butu, inakufa ganzi na kutofahamu. Aina hii ya mtu kamwe hataelewa maneno ya Mungu na kamwe hatakuwa na uhusiano wa kufaa na Mungu; aina hii ya mtu kamwe hatabadilisha tabia yake. Kubadilisha tabia ya mtu ni mchakato wa mtu kuutoa kabisa moyo wake kwa Mungu, na wa kupokea nuru na mwangaza kutoka kwa maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu inaweza, kumruhusu mtu kuingia kwa utendaji, na pia kumwezesha kuepuka masuala yake hasi baada ya kupata maarifa. Unapoweza kuutoa moyo wako kwa Mungu, utaweza kuhisi kila harakati yenye hila ndani ya roho yako, nawe utajua kila nuru na mwangaza upokelewao kutoka kwa Mungu. Shikilia hili, nawe utaingia katika njia ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu hatua kwa hatua. Kadri moyo wako unavyoweza kuwa mtulivu mbele za Mungu, ndivyo roho yako itakavyokuwa makini zaidi na wa kutaka uangalifu mkubwa, na kadri roho yako itakavyoweza kutambua kuchochewa na Roho Mtakatifu, kisha uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kufaa zaidi na zaidi. Uhusiano unaofaa kati ya watu unaundwa juu ya msingi wa kumpa Mungu moyo wako; haufanikishwi kupitia jitihada za binadamu. Bila Mungu mioyoni mwao, uhusiano kati ya watu ni uhusiano wa mwili tu. Sio uhusiano unaofaa, bali ni kujiingiza katika tamaa za mwili—ni uhusiano ambao Mungu anachukia, Asioupenda. Ukisema kuwa roho yako imeguzwa, lakini daima unataka kuwa na ushirika na watu wanaokupendeza, na wale unaowachukulia kwa hali ya juu, na iwapo kuna mtafutaji mwingine ambaye hakupendezi, ambaye huna upendeleo kwake na huwezi kujihusisha naye, huu ni ushahidi zaidi kuwa wewe ni mtu mwenye hisia na kuwa huna uhusiano unaofaa na Mungu kamwe. Unajaribu kumdanganya Mungu na kuficha ubaya wako mwenyewe. Hata ingawa unaweza kushirikisha uelewano kiasi lakini unabeba ubaya moyoni mwako, kila kitu unachofanya ni kizuri tu kwa kiwango cha mwanadamu. Mungu hatakusifu—unatenda kulingana na mwili, sio kulingana na mzigo wa Mungu. Iwapo unaweza kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu na kuwa na ushirikiano wa kufaa na wale wote wanaompenda Mungu, ni hapo tu ndipo utakuwa uko tayari kwa matumizi ya Mungu. Kwa njia hii, haijalishi jinsi unavyopatana na wengine, haitakuwa kulingana na falsafa ya maisha, lakini itakuwa kuishi mbele ya Mungu, kuufikiria mzigo Wake.
kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa kila tamshi la Mungu, baada ya kulisoma na kupata ufahamu, utaliweka katika vitendo. Bila kujali ulivyokuwa ukitenda kabla—pengine huko nyuma mwili wako ulikuwa dhaifu, ulikuwa muasi, na ulipinga—hili silo jambo kubwa, na haliwezi kuzuia maisha yako yasikue leo. Ilimradi unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, basi kuna tumaini. Ikiwa kwa kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, unakuwa na mbadiliko na kuruhusu watu wengine kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa mazuri, inaonyesha kwamba una uhusiano wa kawaida na Mungu na kwamba umewekwa sawa. Mungu hashughulikii watu kulingana na dhambi zao. Ilimradi unaweza kutoasi tena na hupingi tena baada ya wewe kuelewa na kufahamu, basi Mungu atakuwa bado Ana huruma na wewe. Unapokuwa na ufahamu huu na nia ya kutafuta kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Bila kujali unachofanya, zingatia: Mungu atafikiri nini ikiwa nitafanya hiki? Je, kitawafaidi ndugu? Je, kitakuwa cha faida kwa kazi ya nyumba ya Mungu? Chunguza makusudi yako katika maombi, ushirika, usemi, kazi na kuhusiana na watu, na chunguza endapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au si wa kawaida. Ikiwa huwezi kutofautisha makusudi yako na fikra zako, basi huna ubaguzi, kitu ambacho kinathibitisha kwamba unaelewa kidogo sana kuhusu ukweli. Ikiwa unaweza kuwa na ufahamu ulio wazi wa kila kitu ambacho Mungu hufanya, vitazame vitu kulingana na neno la Mungu na vitazame vitu kwa kusimama katika upande wa Mungu, basi mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hiyo, kujenga uhusiano mzuri na Mungu ni kipaumbele cha juu kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuichukulia kama kazi muhimu na kama tukio lao kubwa la maisha. Kila kitu unachofanya kinapaswa kipimwe dhidi ya iwapo una uhusiano wa kawaida na Mungu au la. Ikiwa uhusianao wako na Mungu ni wa kawaida na makusudi yako ni sahihi, basi kifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupoteza maslahi binafsi, hupaswi kumruhusu Shetani kushinda, hupaswi kumruhusu Shetani kupata kitu dhidi yako, na hupaswi kumruhusu Shetani kukufanya uwe kichekesho. Kusudi kama hili ni udhihirisho kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Si kwa ajili ya mwili, badala yake ni kwa ajili ya amani ya roho, ni kwa ajili ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa kuweka sawa mtazamo wako wa imani kwa Mungu. Ni kumruhusu Mungu kukupata, kumruhusu Mungu kufichua matunda ya maneno Yake kwako na kukuangazia na kukupatia nuru zaidi. Kwa namna hii utaingia katika tabia nzuri. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya sasa, ingia katika njia ya sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu, fanya kulingana na matakwa ya Mungu ya sasa, usifuate mazoea ya kale, using’ang’anie njia za zamani za kufanya mambo, na haraka ingia katika namna ya kazi ya leo. Kwa njia hii uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utaingia katika njia sahihi ya kumwamini Mungu.
kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki, Injili ya Ufalme wa Mbinguni

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni