Jumamosi, 4 Novemba 2017

Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Umeme wa Mashariki,  Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu,
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II


Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Mwenyezi Mungu alisema:Kwenye mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, wakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwako? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwako? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inakuvutia zaidi? Ni sehemu ipi unayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwako wewe kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inawakilisha Mungu Mwenyewe; kwenye mpango wa usimamizi wa ujumla wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.

Ijumaa, 3 Novemba 2017

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV | Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu,  Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,
Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV | Utakatifu wa Mungu (I)


Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Utakatifu wa Mungu (I)

Mwenyezi Mungu alisema:Tumekuwa na ushirika wa ziada wa mamlaka ya Mungu leo, na hatutazungumza kuhusu haki ya Mungu sasa hivi. Leo tutazungumza kuhusu mada nzima mpya—utakatifu wa Mungu. Utakatifu wa Mungu pia ni kipengele kingine cha kiini cha kipekee cha Mungu, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kushiriki mada hii hapa. Hiki kipengele cha kiini cha Mungu ambacho Nitashiriki, pamoja na vile vipengele viwili tulivyoshiriki mbeleni, tabia ya haki ya Mungu na mamlaka ya Mungu—yote ni ya kipekee? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu pia ni wa kipekee, basi msingi wa upekee huu, mzizi wa upekee huu, ni maudhui ya ushirika wetu wa leo. Mnaelewa?

Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,
Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Umeme wa Mashariki | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Mwenyezi Mungu alisema: Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. Tukizungumzia umuhimu, ni nini kitu muhimu zaidi kwa kila muumini katika Mungu?

Alhamisi, 2 Novemba 2017

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu,

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III,Mamlaka ya Mungu (II)


Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Mamlaka ya Mungu (II)

Mwenyezi Mungu alisema:Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee.” Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, umepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamekusaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya “Mamlaka ya Mungu.”

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

 Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu,

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II,Tabia ya Haki ya Mungu


Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema:Kwa vile sasa mumesikiliza kikao cha ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mumejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kushika, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo-upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe.Ufahamu huu ni sehemu moja ya kumjua Mungu. Sehemu ile nyingine ni nini, hivyo basi? Hii ndiyo mada ambayo Ningependa tuweze kushiriki pamoja leo—tabia ya haki ya Mungu.

Jumatano, 1 Novemba 2017

Umeme wa Mashariki | Kazi Katika Enzi ya Sheria

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, kanisa,

Umeme wa MasharikiKazi katika Enzi ya Sheria

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Alichagua watu Alioona kwamba walifaa ili kuwawekea mipaka upana wa kazi Yake.

Umeme wa Mashariki | Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele"




Nitampenda Mungu Milele

Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.

Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.

Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.

Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,

na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.

Lakini Hujawahi kuniacha.