Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Moja
Mwenyezi Mungu alisema, Kwa macho ya mwanadamu, inaonekana hakuna badiliko katika matamshi ya Mungu wakati wa kipindi hiki, ambalo ni kwa sababu watu hawawezi kuelewa sheria ambazo kwazo Mungu hunena, na hawafahamu muktadha wa maneno Yake. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu hawaamini kwamba kuna mafumbo yoyote mapya katika maneno haya; hivyo, hawawezi kuishi maisha yaliyo mapya kiajabu, na badala yake huishi maisha yaliyokwama na yasiyokuwa na uhai. Lakini katika matamshi ya Mungu, tunaona kwamba kuna kiwango cha kina cha maana, kile kisichofahamika na pia kisichofikika na mwanadamu.
