Jumatatu, 16 Julai 2018

Umeme wa Mashariki | Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, wokovu,

Shahidi uzoefu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Wuzhi    Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 2006, nilinyang'anywa cheo changu kama kiongozi na nikarudishwa nilikotoka kwa sababu nilifikiriwa kuwa "bwana ndiyo" sana. Niliporejea mara ya kwanza, nilitumbukia ndani ya kikalibu cha mateso na maumivu makubwa. Sikuwahi kufikiri kwamba baada ya miaka mingi ya uongozi mambo yangeharibika kwa sababu ya kuwa "bwana ndiyo." Huu ulikuwa ndio mwisho kwangu, nilidhani, kila mtu aliyenijua angejua juu ya kushindwa kwangu na ningefanywa kama mfano mbaya katika kanisa. Ningewezaje kukabiliana na wengine baada ya haya yote? Jinsi nilivyozidi kufikiria, ndivyo nilivyozidi kuwa hasi, mpaka hatimaye nikapoteza imani ya kuendelea kutafuta ukweli.

Jumamosi, 14 Julai 2018

Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, wafuasi wa Kristo,

Mimi Sistahili Kumwona Kristo

Huanbao    Mji wa Dalian, Mkoa wa Liaoning
Tangu kwanza nianze kumwamini Mwenyezi Mungu, daima nimewapenda wale ndugu wa kiume na wa kike ambao wanaweza kupokea huduma ya kibinafsi ya Kristo, ambao wanaweza kusikia mahubiri Yake kwa masikio yao wenyewe. Katika moyo wangu, nimewaza jinsi ingekuwa vizuri sana kama siku moja katika siku zijazo ninaweza kusikia mahubiri ya Kristo, bila shaka kumwona Yeye kungekuwa kwa ajabu hata zaidi. Lakini hivi karibuni, kwa njia ya kusikiliza ushirika Wake, nimekuja kuhisi kwa undani moyoni mwangu kwamba mimi sifai kumwona Kristo.

Ijumaa, 13 Julai 2018

Umeme wa Mashariki | Tafakuri kuhusu Kubadilishwa

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, mapenzi ya Mungu,

Shahidi uzoefu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tafakuri kuhusu Kubadilishwa

Yi Ran    Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu. Kwa hiyo sikuweza kujua asilani jinsi mtu fulani aliyetafuta ukweli sana angeweza kubadilishwa. Inawezekana kwamba yeye alizungumza juu ya maonyesho yake mwenyewe ya upotovu sana, na hivyo kiongozi wake kwa makosa alimchukua kuwa mtu asiyefuatilia ukweli, na kumbadilisha? Kama hili ndilo lililotokea kweli, basi si fursa ya mafunzo kwa mtu ambaye alikuwa anafuta ukweli imeangamizwa?

Jumatano, 11 Julai 2018

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,




Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

2. Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

Jumanne, 10 Julai 2018

1. Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu,

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

1. Kazi ya Kusimamia Mwanadamu ni Gani?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.

Jumatatu, 9 Julai 2018

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu,

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Mwenyezi Mungu alisema, Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, “Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Iwapo hukumu Yako itaonyesha tabia Yako, na kuruhusu tabia Yako ya haki kuonekana na viumbe wote, na iwapo inaweza kufanya upendo wangu Kwako uwe safi zaidi, ili niweze kufikia mfano wa mwenye haki, basi hukumu Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo. Najua kwamba bado kuna mengi ndani yangu yaliyo ya uasi, na kwamba mimi bado sifai kuja mbele Yako.

Jumapili, 8 Julai 2018

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Yesu,

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Mwenyezi Mungu alisema, Katika kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilimkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita.