Jumanne, 11 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" (Official Video)
Mwenyezi Mungu anasema, "Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno."

Sikiliza zaidi: Injili ya Ufalme wa Mbinguni, Video za Nyimbo za Dini

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

Jumatatu, 10 Desemba 2018

Wimbo Mpya wa Dini | "Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa" | Have You Followed God's Footsteps?

Wimbo Mpya wa Dini | "Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa" | Have You Followed God's Footsteps? (Official Video)
Kazi ya Mungu inaendelea kuwa bora; ingawa kusudi linabaki bila kubadilika, mbinu ya kazi Yake inabadilika daima, na hivyo pia wale wanaomfuata. Kadiri ambavyo Mungu anafanya kazi zaidi, ndivyo anavyozidi mwanadamu kumjua, kikamilifu, ndivyo tabia ya mwanadamu inavyozidi kubadilika pamoja na kazi Yake ifaavyo.

Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo

Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo

Wale miongoni mwa ndugu na dada ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika Imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi hawatashindwa tu kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomuasi Mungu. Wakati mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi Yeye, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini.

Jumapili, 9 Desemba 2018

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu"


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu"
Mwenyezi Mungu anasema, "Kama huelewi tabia ya Mungu, basi itakuwa haiwezekani kwako wewe kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, ndivyo pia haitawezekana kubakiza hali ya kumcha na kumwogopa Yeye, utakuwa ni uzembe na kuepuka kusema ukweli wote kwa kutojali, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, ilhali hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakinifu au kudadisi suala hili. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuuzilia mbali amri za kiutawala Nilizozitoa.

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu

Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika. Mambo mengi hayawezi kusemwa kwenu moja kwa moja na athari ya awali haiwezi kutimizwa. Kwa hiyo, kazi za ziada zinapaswa kuongezwa kwa kazi Yangu.

Jumamosi, 8 Desemba 2018

Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachoitwa nyakati za sasa "wazazi" wa Petro?