Jumatatu, 21 Januari 2019

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 18

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 18

Maneno yote ya Mungu yana sehemu ya tabia Yake; tabia Yake haiwezi kuonyeshwa kwa ukamilifu kwa maneno, kwa hiyo hii inaonyesha kiasi gani cha utajiri kiko ndani Yake. Kile ambacho watu wanaweza kukiona na kukigusa ni, hata hivyo, finyu, kama ulivyo uwezo wa watu. Ingawa maneno ya Mungu ni dhahiri, watu hawawezi kuyaelewa kwa ukamilifu. Kama maneno haya tu: "Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja.

Jumapili, 20 Januari 2019

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 26

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Fasiri ya Mafumbo ya Maneno ya Mungu | Sura ya 26

Kutoka kwa maneno yote yaliyonenwa na Mungu, inaweza kuonekana kwamba siku ya Mungu inakaribia kila siku inapopita. Ni kama kwamba siku hii iko mbele ya macho ya watu, kama kwamba itafika kesho. Hivyo, baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wote wanajawa na hofu, na pia wana hisia kiasi fulani ya ukiwa wa dunia. Ni kama kwamba, jinsi majani yanavyoanguka na manyunyu kushuka, watu wote wametoweka wasionekane tena, kama kwamba wote wameondolewa kabisa kutoka duniani.

Jumamosi, 19 Januari 2019

Neno la Mwenyezi Mungu | Sura ya 94

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi MunguSura ya 94

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni. Hili linamaanisha kwamba tutarudi kutoka kwa nyama hadi kwa mwili wa awali.

Ijumaa, 18 Januari 2019

Sura ya 8 Miisho ya Aina Mbalimbali za Watu na Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu

Sura ya 8 Miisho ya Aina Mbalimbali za Watu na Ahadi ya Mungu kwa Mwanadamu

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi Yangu inadumu kwa miaka elfu sita tu, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala Sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kudhibiti yote Hatafanya kazi tena duniani.

Alhamisi, 17 Januari 2019

7. Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

7. Waumini katika Mungu Wanapasa Kujiandaa kwa Ajili ya Hatima Yao kwa Matendo Mema ya Kutosha

Maneno Husika ya Mungu:
Huruma Zangu zinaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima wenyewe. Na adhabu inayoletwa kwa waovu ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, zaidi sana, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapokuja, njaa na baa litawakumba wale wote wanaopinga Mimi na watalia kwa uchungu. Wale wote ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, wakijipata katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra katika mamilioni ya miaka, wataishi katika hali ya kila siku ya taharuki na woga.

Jumatano, 16 Januari 2019

6. Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

6. Maana ya Mateso na ni Mateso ya Aina Gani Ambayo Waumini wa Mungu Lazima Wastahimili

Maneno Husika ya Mungu:
Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu!

Jumanne, 15 Januari 2019

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Sura ya 7 Vipengele Vingine vya Ukweli Ambavyo Unafaa Kueleweka Katika Imani Yako kwa Mungu

5. Imani Katika Mungu Haipasi Kuwa kwa ajili ya Kutafuta Amani na Baraka Pekee

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Sasa mnajua nyote ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na ustawi wa mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo wa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu.