Alhamisi, 14 Februari 2019

Maonyesho ya Mungu | “Wewe U Mwaminifu kwa Nani?” (Official video)


Maonyesho ya Mungu | “Wewe U Mwaminifu kwa Nani?” (Official video)
Mwenyezi Mungu anasema, “Mmekuwa wafuasi Wangu kwa miaka mingi sana, lakini hamjawahi kunionesha hata chembe ya uaminifu. Badala yake mmekuwa mkizunguka kwa watu mnaowapenda na vitu vinavyowapendeza sana, na kuviweka karibu na mioyo yenu na havijawahi kuachwa, wakati wowote, mahali popote. ... Mnajiweka wenyewe katika shughuli ambazo mnazipenda: Wengine ni waaminifu kwa watoto, wengine kwa waume, wake, utajiri, kazi, wenye vyeo, umaarufu, au wanawake.

Jumatano, 13 Februari 2019

Ni Nini Maana ya Krismasi, na Je, Unamwabudu Bwana Yesu Kweli?

Ni Nini Maana ya Krismasi, na Je, Unamwabudu Bwana Yesu Kweli?

Na Siyuan
Vyanzo vya Krismasi
Kila mwaka, Krismasi inapokaribia, maduka kwenye mitaa hutayarisha maonyesho yang’aayo ya zawadi za Krismasi, pamoja na Baba Krismasi na miti ya Krismasi, na kadhalika. Kuna taa nyingi za rangi nyingi zilizoning’inizwa katika miti na kwenye majengo, na miji mizima hupambwa kwa fanusi na mapazia ya rangi nyingi, na kila mahali kuna furaha na msisimko. Kwa Ukristo, Krismasi ni likizo ya pekee sana, na miezi kadhaa kabla ya Krismasi, makanisa mengi yataanza kujishughulisha na kuandaa kila kitu kilicho muhimu kwa likizo ya Krismasi. Katika Siku ya Krismasi, makanisa hujaa, na ndugu hushiriki katika sherehe, wakila chakula rasmi cha Krismasi, kuigiza na kumwabudu Bwana Yesu, na kadhalika. Uso wa kila mtu hujawa na furaha.

Jumanne, 12 Februari 2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 2)

Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Katika siku chache zilizofuata, ingawa Jingru hakuwa ameanguka katika majaribu ya Shetani na alijua kwamba hangeweza kuwa mwenzi wa Wang Wei kamwe, mkutano wake na Wang Wei jioni hiyo na ungamo lake la kweli vilirudiwa akilini mwake tena na tena kama onyesho katika filamu …
Wang Wei alipompigia simu tena, moyo wa Jingru ulishtuka kidogo, naye akajiambia: “Sote wawili hatuwezi kuwa kitu kimoja, lakini bado tunaweza kuwa marafiki wa kawaida. Mradi nijizuie ili nisifanye chochote kinachoenda mbali mno, basi itakuwa sawa.” Kisha akajibu simu kutoka kwa Wang Wei na kuzungumza naye.

Jumatatu, 11 Februari 2019

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Ushuhuda wa Mkristo: Jinsi Alivyoshinda Majaribu ya Kuwa na Mpenzi wa Siri (Sehemu ya 1)

Na Xiyue, Mkoa wa Henan
Jioni moja, Jingru alikuwa akinadhifisha kwake.
“Krr, krr.” Simu ilianza kulia. Aliijibu na sauti ngeni lakini bado inayojulikana ililia sikioni mwake: “Halo! Ni Wang Wei. Uko nyumbani!”
“Wang Wei?” Jingru kwa namna fulani alistaajabu: Kwa nini alikuwa akimpigia simu sasa baada ya miaka mingi sana?
“Ndiyo … niko nyumbani. Kuna nini?” aliuliza Jingru kwa mshangao.
“Hatujaonana kwa muda mrefu. Ningependa kukupeleka matembezini. Niko njiani kuja kwako na nitawasili hivi punde. Nisubiri nje ya mlango wako!” Wang Wei akasema.

Jumapili, 10 Februari 2019

Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu


Baada ya Usaliti wa Mumewe Mungu Alimuokoa Kutoka kwenye Fadhaa ya Uchungu

Na Ouyang Mo, Mkoa wa Hubei
Baada ya miongo miwili ya mema na mabaya ambayo yeye na mumewe walipitia pamoja, hakuwahi kamwe kufikiria kwamba mumewe angekuwa na uhusiano wa nje ya ndoa. Alishindwa kabisa kuvumilia wakati alipogundua hilo. Licha ya kujaribu kila kitu ili kumfanya mumewe ampende tena, yote ilikuwa kazi bure.

Jumamosi, 9 Februari 2019

Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Wimbo wa Maneno ya Mungu | Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake

I

      Ni Wakati tu Mungu anapojinyenyekeza kwa kiwango fulani,
kumaanisha Anakuwa mwili ili kuishi kati ya wanadamu,
ndipo wataweza kuwa wasiri Wake,
ndipo watakuwa marafiki Zake wa karibu.
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
Wakati Mungu ni wa Roho,
‘metukuka na mgumu kumwelewa?

Ijumaa, 8 Februari 2019

Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God
Maombi ni njia moja ya mwanadamu kushirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kuangaziwa na kuwa mwenye nguvu-nia. Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.