Mnayaonaje maono ya Ufalme wa Milenia? Baadhi ya watu hutafakari sana kuuhusu na kusema kuwa Ufalme wa Milenia utadumu duniani kwa miaka elfu moja, hivyo basi ikiwa waumini wazee katika kanisa hawajaoa, je, wanapaswa kuoa? Familia yangu haina pesa, je napaswa nianze kutafuta pesa? … Ufalme wa Milenia ni nini? Je, mnajua? Watu ni nusu vipofu na wanapitia mateso mengi. Kwa hakika, Ufalme wa Milenia bado haujafika rasmi. Katika hatua ya kuwafanya wanadamu wakamilike, Ufalme wa Milenia ni mfano mdogo tu; katika kipindi cha Ufalme wa Milenia uliozungumziwa na Mungu, mwanadamu atakuwa amefanywa mkamilifu.
Jumanne, 6 Agosti 2019
Jumatatu, 5 Agosti 2019
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza)
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu.
Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli
Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote.
Jumapili, 4 Agosti 2019
Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne
Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu anasema, “Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: ‘Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi.’ Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: ‘Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.’ Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. ‘Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.’ Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu.... Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi na midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Kinywa chake hakikubariki tu jina la Mungu, lakini ndani ya moyo wake alibariki pia jina la Mungu; mdomo na moyo wake ulikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.”
Tazama Zaidi: Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuijua Kazi ya Mungu Leo"
Jumamosi, 3 Agosti 2019
Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu
Mungu huzungumza maneno Yake na kufanya kazi Yake kulingana na enzi tofauti, na katika enzi tofauti, Anazungumza maneno tofauti. Mungu hafuati sheria, ama kurudia kazi ya awali, ama kuhisi hali ya kumbukumbu kwa vitu vilivyopita; ni Mungu ambaye ni mpya kila wakati na hazeeki, na kila siku anazungumza maneno mapya. Lazima uyafuate yale ambayo lazima yafuatwe leo; haya ni majukumu na kazi ya mwanadamu. Ni muhimu kwamba utendaji uwekwe katika nuru iliyopo na maneno ya Mungu katika siku ya leo. Mungu hafuati masharti, na Anaweza kuzungumza kutoka kwa mitazamo mingi tofauti ili kufanya wazi hekima Yake na uwezo.
Ijumaa, 2 Agosti 2019
Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwenye neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani yake
Alhamisi, 1 Agosti 2019
Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu
Ili uwe na ushuhuda kwa Mungu na kuliaibisha joka jekundu ni sharti uwe na kanuni, na sharti: Katika moyo wako ni lazima umpende Mungu na uingie katika maneno ya Mungu. Kama huingii katika maneno ya Mungu, basi hutakuwa na njia ya kumuaibisha Shetani. Katika ukuaji wa maisha yako, unalikataa joka kuu jekundu na kuliletea aibu kamili, na ni hapo tu ndipo hili joka jekundu kweli linaaibika. Kadiri unavyohiyari kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo, ndivyo unavyothibitisha kwamba unampenda Mungu na kulichukia joka kuu jekundu; kadiri unavyotii maneno ya Mungu, ndivyo unavyothibitisha kwamba unautamani ukweli.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)





