Jumamosi, 14 Septemba 2019

Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kikristo

Mwanadamu anaelewa sehemu ndogo ya kazi ya leo na kazi ya baadaye, lakini hafahamu hatima ambapo mwanadamu ataingia. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe: Mwanadamu anapaswa kumfuata Mungu kwa lolote afanyalo, na mnapaswa muendelee mbele kwa njia yoyote ambayo Nitawaambia. Wewe huna mbinu ya kufanya mipango yako mwenyewe, na huna uwezo wa kujitawala mwenyewe; yote ni lazima yaachwe kwa rehema za Mungu, na kila kitu kinadhibitiwa na mikono Yake.

Ijumaa, 13 Septemba 2019

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu Kristo

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu.

Alhamisi, 12 Septemba 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote.

Jumatano, 11 Septemba 2019

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Kazi-ya-Mungu

Wakati kazi ya Mungu inafikia hatua fulani, na usimamizi Wake kufikia hatua fulani, wale wanaoutafuta moyo Wake wote huwa na uwezo wa kutimiza matakwa yake. Mungu humwekea mwanadamu matakwa kulingana na viwango Vyake mwenyewe, na kulingana na kile ambacho mwanadamu anaweza kufanikisha. Akiwa anazungumzia usimamizi Wake, Yeye humwonyesha njia mwanadamu , na kumpa mwanadamu namna ya kudumu. Usimamizi wa Mungu na vitendo vya mwanadamu vipo katika hatua sawia kikazi, na yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Mazungumzo kuhusu usimamizi wa Mungu yanagusia mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, na yanazungumzia kuhusu yale yafaayo kufanywa na mwanadamu, na mabadiliko katika tabia ya mwanadamu, hugusia kazi ya Mungu; hakuna wakati ambao haya mawili yanaweza kutenganishwa. Vitendo vya mwanadamu vinabadilika, hatua kwa hatua.

Jumanne, 10 Septemba 2019

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kazi ya Mungu

Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. Hakuna anayeweza kupinga hili, kwani ndio ukweli. Kila Akifanyacho Mungu ni kwa faida ya mwanadamu, na kinalenga hila za Shetani. Kila anachokihitaji mwanadamu kinatoka kwa Mungu, na Mungu ndiye chanzo cha maisha ya mwanadamu.

Jumatatu, 9 Septemba 2019

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili. Kabla Aanze kutekeleza kazi ya huduma Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bila kuonyesha ishara ya uungu Wake, na ni baada tu ya kuanza rasmi kutekeleza huduma Yake ndipo uungu Wake uliwekwa wazi.

Jumapili, 8 Septemba 2019

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kazi Yake katika mwili ni ya umuhimu mkubwa, ambao umezungumzwa kuhusiana na kazi, na Yule ambaye hatimaye anahitimisha kazi ni Mungu mwenye mwili, na sio Roho. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Mungu wakati fulani anaweza kuja duniani na kumtokea mwanadamu, ambapo atawahukumu wanadamu wote, akimjaribu mmoja baada ya mwingine bila mtu yeyote kupitwa. Wale wanaofikiri kwa namna hii hawafahamu hatua hii ya kazi ya Mungu mwenye mwili. Mungu hamhukumu mwanadamu mmoja baada ya mwingine, na hamjaribu mwanadamu mmoja baada ya mwingine; kufanya hivyo sio kazi ya hukumu.