Umeme wa Mashariki | Tamko la Thelathini na Mbili
Mwanga ni nini? Katika siku za nyuma kwa kweli mliuona mbadiliko wa kazi ya Roho Mtakatifu kama mwanga. Kuna mwanga wa kweli wakati wote, unaojumuisha ninyi kupata kile Mungu alicho kupitia kwa kunikaribia na kushirikiana na Mimi; kuwa na utambuzi katika maneno ya Mungu na kufahamu mapenzi ya Mungu katika maneno Yake—yaani, mnapokula na kunywa, mnahisi Roho wa maneno ya Mungu na kupokea maneno ya Mungu ndani yenu; kuelewa kile Alicho huku mkipitia na kupokea mwangaza wa Mungu huku mkizungumza na Yeye; na pia kupewa nuru na kuwa na utambuzi mpya katika maneno ya Mungu wakati wote huku mkifikiria na kutafakari. Ukielewa neno la Mungu na uhisi mwanga mpya, basi hutakuwa na nguvu katika huduma yako? Ninyi hujitia wasiwasi sana katika huduma yenu!

