Jumamosi, 8 Desemba 2018

Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Ikiwa watu wanaweza kweli kuielewa kikamilifu njia sahihi ya maisha ya binadamu na vilevile kusudi la usimamizi wa Mungu wa binadamu, wasingeshikilia mategemeo yao ya baadaye na majaliwa yao binafsi kama hazina mioyoni mwao. Wasingetamani tena kuwatumikia wazazi wao ambao ni wabaya zaidi kuliko nguruwe na mbwa. Je, mategemeo ya baadaye na majaliwa ya mwanadamu si kabisa kile kinachoitwa nyakati za sasa "wazazi" wa Petro?

Ijumaa, 7 Desemba 2018

Neno la Mungu | "Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi" (Official Video)

Neno la Mungu | "Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi" (Official Video)
Mwenyezi Mungu anasema, "Hata hivyo unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hapo awali hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na sumu yake. Hivyo, Naliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kilichoumbwa na mkono Wangu, Wapendwa Wangu walio watakatifu ambao kamwe hawajawahi kumilikiwa na mwingine yoyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu tena.

Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzimam | Utangulizi

"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni kundi la pili la matamshi yanayoonyeshwa na Kristo. Ndani yake, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na "Maneno ya Roho kwa Makanisa." "Maneno ya Roho kwa makanisa" inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho. Hatimaye, inaisha kwa "majaribu ya watendaji huduma." Hata hivyo, "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima," inaanza na hitimisho la utambulisho wa watu kama watendaji huduma na mwanzo wa maisha yao kama watu wa Mungu. 

Alhamisi, 6 Desemba 2018

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)
Mwenyezi Mungu anasema, "Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habalidiliki na humfafanua kulingana na Bibilia, kana kwamba mwanadamu ameona ndani ya usimamizi wa Mungu, kana kwamba kila kitu Atendacho Mungu kiko mikononi mwa mwanadamu. Wanadamu ni wa kufanya mzaha pakubwa, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha lugha ya kushawishi ya kujivuna. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, Bado Nasema kwamba bado humfahamu Mungu, kwamba hakuna walio wapinzani wa Mungu zaidi, na kwamba unamshutumu Mungu, kwa kuwa huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili ya Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hajui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi na kwa sababu badala ya kufuata ukweli, maarifa yake yote ya Mungu yametolewa kutoka kwenye chanzo kimoja, chenye ugumu na kisichobadilika. Hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Amesulubishwa kwa mara nyingine msalabani na mwanadamu. ... Je wewe ni mmoja wa wale ambao wamemsulubisha Yesu msalabani tena? Mwisho, Ninasema hivi: Ole wao wamsulubishao Mungu."

Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu.

Jumatano, 5 Desemba 2018

Wimbo Mpya wa Dini "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu"


Wimbo Mpya wa Dini "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Have You Enjoyed the Joy of Gaining the Work of the Holy Spirit? (Official Video)
Wakati hamumwelewi Mungu na hamjui asili Yake, mioyo yenu haiwezi kamwe kufunguka, kufungukia Mungu. Mara utakapomwelewa Mungu wako, utaelewa kilicho moyoni Mwake, na kufurahia kilicho ndani Yake kwa imani na usikivu wako wote. Unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, kidogo kidogo, siku baada ya siku, unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utakuwa wazi Kwake.

Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani (IV) | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea Makanisani (IV) | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu; hii ni kwa kuwa asili potovu ya mwanadamu inatokana kabisa na Shetani na asili ya mwanadamu imemilikiwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, na aidha haishi katika mwanga. Kwa hivyo, haiwezekani ukweli kumilikiwa kiasili katika asili ya kila mtu, na zaidi ya hayo, hawawezi kuzaliwa na kiini cha kumwogopa, kiini cha kumheshimu Mungu.