Jumamosi, 11 Novemba 2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (2)

Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (2)


Umeme wa Mashariki
 | Kuhusu Biblia (2)

    Mwenyezi Mungu alisema: Biblia pia huitwa Agano la Kale na Agano Jipya. Je, wajua “agano” linarejelea nini? “Agano” katika “Agano Jipya” linatokana na makubaliano ya Yehova na watu wa Israeli Alipowaua Wamisri na kuwaokoa Waisraeli kutoka kwa Farao. Bila Shaka, uthibitisho wa haya makubaliano ulikuwa damu ya mwanakondoo iliyopakwa kwenye linta kupitia kwayo Mungu Alianzisha agano na mwanadamu, moja ambalo ilisemwa kuwa wale wote waliokuwa na damu ya mwanakondoo juu na pembeni mwa viunzi vya mlango walikuwa Waisraeli, walikuwa wateuliwa wa Mungu, na wote wangeokolewa na Yehova (kwa kuwa Yehova wakati ule Alikuwa karibu kuwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri wote na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe). Agano hili lina viwango viwili vya maana. Hakuna mmoja wa watu au wanyama wa Misri angeokolewa naYehova; Angewaua wazaliwa wa kwanza wa kiume na wazaliwa wa kwanza wa kondoo na ng’ombe wao wote. Kwa hivyo, katika vitabu vingi vya unabii kulitabiriwa kwamba Wamisri wangeadibiwa vikali kutokana na agano la Yehova. Hiki ndicho kiwango cha kwanza cha maana. Yehova Aliwaua wazaliwa wa kwanza wa kiume wa Misri na wazaliwa wa kwanza wa mifugo wao wote, na kuwaacha Waisraeli wote, jambo lililomaanisha kuwa wale wote waliokuwa wa nchi ya Israeli walipendwa na Yehova na wote wangeokolewa; Alidhamiria kufanya kazi ya muda mrefu ndani yao, na Alianzisha agano nao kwa kutumia damu ya mwanakondoo. Tangu wakati ule kuendelea, Yehova Asingewaua Waisraeli na Alisema kuwa daima wangekuwa wateuliwa Wake. Angeianza kazi Yake ya Enzi Nzima ya Sheria Miongoni mwa makabila kumi na mawili ya Israeli, Angeziweka wazi sheria Zake zote kwa Waisraeli, na kuchagua manabii na waamuzi kutoka kati yao, na wangekuwa katikati ya kazi Yake. Alifanya Agano nao: Angefanya kazi tu miongoni mwa wateuliwa isipokuwa enzi ibadilike. Agano la Yehova lilikuwa lisilobadilika kwani lilitengenezwa kwa damu, na lilianzishwa na wateuliwa Wake. La muhimu zaidi, Alikuwa Ameteua mawanda na malengo yafaayo ya kazi Yake katika enzi nzima, na kwa hivyo watu waliliona agano kuwa la umuhimu sana. Hiki ndicho kiwango cha pili cha maana ya agano. Isipokuwa kitabu cha Mwanzo, ambacho kilikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa agano, vitabu vingine vyote vya Agano la Kale vinaeleza kuhusu kazi miongoni mwa Waisraeli baada ya kuanzishwa kwa agano hili. Bila shaka, yapo maelezo ya hapa na pale ya Watu wa Mataifa, ila kwa ujumla, Agano la Kale linaeleza kuhusu kazi ya Mungu nchini Israeli. Kwa sababu ya Agano kati ya Yehova na Waisraeli, vitabu vilivyoandikwa katika Enzi ya Sheria vinaitwa “Agano la Kale.” Vimepatiwa jina hili kutokana na agano la Yehova na Waisraeli.

    Agano Jipya lilipatiwa jina hilo kutokana na damu iliyomwagwa na Yesu msalabani na agano Lake na wale wote waliomwamini. Agano la Yesu lilikuwa hili: Watu hawakuwa na budi kumwamini ili dhambi zao zisamehewe kwa kumwagika kwa damu Yake, na kwa njia hiyo wangeokolewa na kuzaliwa upya kupitia Kwake, na kamwe wasingeendelea kuwa wenye dhambi; watu walipaswa kumwamini ili wapokee neema Yake, na hawangeteseka jehanamu baada ya kufa. Vitabu vyote vilivyoandkwa wakati wa Enzi ya Neema vilizuka baada ya hili agano, na vyote vinaeleza kuhusu kazi na matamshi yaliyomo. Havielezi zaidi ya wokovu wa kusulubishwa kwa Bwana Yesu au hili agano; vyote ni vitabu vilivyoandikwa na wapendwa katika Bwana waliokuwa na tajriba. Kwa hivyo hivi vitabu vilevile vimepatiwa jina kutokana na agano: Vinaitwa “Agano Jipya.” Haya “Maagano” mawili yanajumuisha tu Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria na hayana uhusiano na enzi ya mwisho. Hivyo basi, Biblia haina msaada mkubwa kwa watu wa leo wa siku za mwisho. Zaidi, hutumika kama marejeleo ya muda mfupi, ila kimsingi haina matumizi ya thamani kubwa. Ila watu wa dini bado wanaienzi kuliko kitu kingine chochote. Hawaijui Biblia; wanajua tu jinsi ya kuieleza Biblia na kimsingi hawajui asili yake. Mtazamo wao kuhusu Biblia ni: Kila kitu katika Biblia ni sahihi, haina upungufu au makosa. Baada ya hapo wao huanza kuichunguza. Kwa sababu kwanza wameshakubali kwamba Biblia iko sahihi, bila makosa, wanaichunguza na kuitathimini kwa shauku kubwa. Hatua ya leo ya kazi haikutabiriwa kwa Biblia. Hakukutajwa kazi ya ushindi katika sehemu za giza zaidi, kwani hii ni kazi mpya zaidi. Kwa sababu enzi ya kazi ni tofauti, hata Yesu Mwenyewe hakufahamu kuwa hatua hii ya kazi ingefanywa katika siku za mwisho—basi, watu wa siku za mwisho wangetathimini vipi kuigundua hii hatua ya kazi?

    Wengi wa wale wanaoeleza Biblia wanatumia mitazamo ya kimantiki na hawana usuli wa uhalisia. Wanatumia mantiki tu kivielewa vitu vingi. Kwa miaka na miaka, hakuna aliyethubutu kuichanganua Biblia, au kusema “hapana” kwa Biblia, kwa sababu kitabu hiki ni “kitabu kitakatifu,” na watu wanakiabudu kama Mungu. Hili limeendelea kwa maelfu kadhaa ya miaka. Mungu hajashughulishwa na hakuna aliyegundua maelezo wa ndani kuhusu Biblia. Tunasema kwamba kuithamini sana Biblia ni kuabudu miungu, na bado hakuna kati ya hawa waumini anayethubutu kuyaona mambo kwa njia hii, na watakwambia: “Ndugu! Usiseme hivyo, ni vibaya! Wawezaje kumkufuru Mungu?” Baadaye watakuwa na hisia za uchungu: “Lo, Yesu wa huruma, Bwana wa wokovu, nakuomba umsamehe dhambi zake kwa kuwa Wewe ni Bwana Ampendaye mwanadamu, nasi sote tumekosa, tafadhali tuonee huruma kubwa, amina.” Umeona jinsi walivyo wacha Mungu; ingekuwaje rahisi kwa wao kuukubali ukweli? Msomo wako ambao utawaogopesha kipumbavu. Hakuna ambaye angethubutu kufikiri kuwa Biblia ingeweza kupakwa doa na mawazo ya binadamu na dhana za binadamu, na hakuna awezaye kuiona hii dosari. Baadhi ya mambo katika Biblia ni uzoefu na ufahamu wa wanadamu, baadhi ni kupatiwa nuru ya Roho Mtakatifu, na pia kuna unajisi wa akili na fikra za wanadamu. Mungu hajawahi kuingilia mambo haya lakini kuna kikomo: Hayawezi kuzidi fikra ya kawaida ya watu, na yakipita, yatakuwa yakiingilia na kuitatiza kazi ya Mungu. Kile kinachozidi fikra za kawaida za watu ni kazi ya Shetani, kwa kuwa kinatoa watu wajibu wao, ni kazi ya Shetani, na kuelekezwa na Shetani, na katika kipindi hiki Roho Mtakatifu Hatakuruhusu kutenda mambo kwa njia hiyo. Wakati mwingine ndugu na dada huuliza: “Ni sawa nikitenda mambo kwa namna hii na ile?” Mimi hutazama kimo chao na kusema: “Sawa!” Vilevile kunao watu ambao husema: “Nikitenda namna hii na ile, je, hali yangu ni ya kawaida?” Nami hujibu: “Ndiyo, ni ya kawaida, kawaida haswa!” Wengine husema: “Je, ni sawa nikifanya hivi?” Nami husema: “Hapana!” Wao husema: “Ni kwa nini ni sawa kwake na si sawa kwangu?” Nami husema: “Kwa sababu unachokifanya kinatoka kwa Shetani, kinasumbua, na chanzo cha motisha yako ni uasi.” Huwepo pia wakati ambapo kazi haijasonga kadiri inavyotakiwa na ndugu na dada hawatambui. Wengine huniuliza kama ni sawa kufanya kazi namna ile, na Nionapo kuwa matendo yao hayatatatiza kazi ya siku za usoni, Mimi husema: “Ni sawa.” Kazi ya Roho Mtakatifu huwapa watu upeo; watu hawalazimiki kufuata mapenzi ya Roho Mtakatifu hadi nukta ya mwisho, kwani watu wana fikra ya kawaida na udhaifu, na wana mahitaji ya kimwili, wana matatizo halisi, na katika bongo zao kuna mawazo ambayo kimsingi hawana njia za kuyadhibiti. Kila Ninachohitaji kutoka kwa wanadamu kina mipaka. Wengine huamini kuwa maneno Yangu yana utata, kwamba Nawaambia kutenda mambo kwa njia yoyote ile—hii ni kwa sababu hamfahamu kuwa kuna upeo ufaao katika mahitaji Yangu. Ingekuwa mnavyodhani—Ningekuwa na mahitaji sawa kwa kila mtu bila kighairi, na kuwahitaji wafikie kimo sawa—basi hili lisingefanyika. Huku ni kuuliza lisilowezekana, na ni kanuni ya kazi ya mwanadamu, si kanuni ya kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu huendeshwa kulingana na hali halisi ya wanadamu, na imekitwa katika ubora wao asilia. Hii vilevile ni kanuni ya kueneza injili: Ni lazima uifanye taratibu, na kuruhusu hali asilia kuchukua mkondo wake hadi wakati utakapomwambia mtu ukweli wazi wazi. Ni hapo ndipo watakapoelewa, na ni wakati huo tu ndipo wataweza kuiweka kando Biblia. Ikiwa Mungu Asingefanya hatua hii ya kazi, ni nani angeweza kuyavunja desturi? Ni nani angeweza kuifanya kazi mpya? Ni nani angeweza kutafuta njia mpya nje ya Biblia? Kwa sababu dhana za jadi ya watu na maadili ya kijamii ni maudhi, hawana uwezo wa kuviacha hivi vitu wao wenyewe, wala hawana ujasiri wa kufanya hivyo. Hapo ni bila kutaja namna watu wa leo wametekwa na maneno machache yaliyokufa katika Biblia, maneno ambayo yameimiliki mioyo yao. Watakuwaje radhi kuiacha Biblia? Watawezaje kukubali kwa urahisi njia iliyo nje ya Biblia? Hilo haliwezekani pasipo na wewe kuzungumza wazi kuhusu simulizi ya ndani ya Biblia na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, ili watu wote washawishiwe kabisa—ambalo ni la haja kubwa. Hii ni kwa sababu kila aliye ndani ya dini anaiheshimu Biblia na kuiabudu kama Mungu, vilevile wanajaribu kumfunga Mungu katika mipaka ya Biblia, na ndivyo hutimiza madhumuni yao punde tu wanapomuangika Mungu msalabani kwa mara nyingine.

Yaliyopendekezwa : Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni