Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja? |
Je, Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu Mmoja?
Kwa maelfu ya miaka, watu wachache wamejua kwa hakika kwamba Bwana Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe, kwamba Yeye ni kuonekana kwa Mungu, na kwamba Bwana Yesu ni kupata mwili kwa Bwana. Kwa kweli, Biblia tayari imetabiri kwa dhahiri kitambo. Katika Kitabu cha Isaya, ilinenwa kwamba "Hata hivyo BWANA aliridhika kumchubua; amempa huzuni: utakapofanya nafsi yake kuwa sadaka ya dhambi (ama: wakati atajitoa mwenyewe kama sadaka kwa ajili ya dhambi)" (Isa 53:10). Kutoka kwa kifungu hiki cha Biblia inaweza kuonekana kwamba kwa Bwana Yesu kutumika kama sadaka ya dhambi ina maana kwamba Yehova alijitoa nafsi kama toleo la dhambi, na kwamba Bwana Yesu alikuwa Yehova. "yule ambaye ameniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14.9). "Baba yuko ndani yangu, nami niko ndani yake" (Yohana 10:38). "Mimi na Baba yangu tu mmoja" (Yohana 10:30). Wakati Bwana Yesu alisema kwamba "Mimi na Baba yangu tu mmoja." Alikuwa akisema kwamba Yeye na Yehova ni roho mmoja naye. Maneno yanayosemwa na Bwana Yesu na yale yanayosemwa na Yehova ni sawa–wote wawili ni ukweli, ni matamshi ya Roho mmoja, na chanzo ni sawa; yaani, Bwana Yesu na Yehova ni Mungu mmoja. Vivyo hivyo, chanzo cha maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho na yale ya Bwana Yesu ni sawa, ni matamshi ya Roho Mtakatifu, ni ukweli, na ni sauti ya Mungu. Wale wanaomwamini Bwana wote wanajua kwamba idadi kubwa ya unabii katika Biblia inahusu kurudi kwa Bwana na kazi ya hukumu ya Mungu wa siku za mwisho. Kama Bwana Yesu alivyosema, “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo" (Yohana 14: 3). "Na tazama, ninakuja upesi" (Ufunuo. 22:12). "Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija katika wingu akiwa na nguvu na utukufu mwingi" (Luk 21:27). "Tazama, nitakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Yeye anikataaye mimi, na hayakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena, ndilo hilo litakalomhukumu siku ya mwisho" (Yohana 12:48). Katika Waraka wa Kwanza wa Petro pia ilisemwa kuwa, "Kwa maana wakati umefika ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu" (1Pet 4:17). Ilizungumzwa kwa dhahiri sana katika maandiko haya kwamba Bwana Yesu angerejea wakati wa siku za mwisho, na angeonyesha maneno na kufanya kazi ya hukumu. Wakati Mwenyezi Mungu anapokuja wakati wa siku za mwisho, Yeye hufanya kazi ya hukumu akianza kwa nyumba ya Mungu juu ya msingi wa kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, na huonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu. Ingawa kazi ya Mwenyezi Mungu na ile ya Bwana Yesu ni tofauti, chanzo chao ni sawa– Mungu Aliye mmoja! Hili hutimiza kikamilifu unabii wa Bwana Yesu: "Bado ningali nayo mengi ya kuwaambia, lakini hivi sasa hamwezi kuyastahimili. Hata hivyo, yeye, Roho wa kweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwa ukweli wote: kwa maana hatanena juu yake mwenyewe; bali yote atakayoyasikia, hayo ndiyo atakayoyanena: na atawaonyesha mambo yajayo" (Yohana 16: 12-13). Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho ni mfano halisi wa Roho wa kweli; Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu.
Kujua zaidi: Asili
ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni