Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III | Kazi ya Bwana Yesu katika umri wa neema
Wanafunzi walipiga masikio ya ngano siku ya Sabato |
Mwenyezi Mungu alisema, Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa katika kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wameamini katika Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa. Kama ni maarifa au matendo halisi, wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo kwenye ufuatiliaji wao wa kale, wametambua hali yao waliyopitia ya juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu.
Maarifa haya kwa upande wa watu ni aina ya maarifa ya kihisia; kufikia kiwango cha maarifa ya kirazini kunahitaji ushughulikiaji wa kina na utiliaji mkazo wa utaratibu kwenye hali yao yote wanayopitia. Kabla ya binadamu kumwelewa Mungu kwa njia ya kweli, kwa dhahania inaweza kusemekana kwamba wanaamini kwa uwepo wa Mungu mioyoni mwao, lakini hawana ufahamu halisi wa maswali mahususi kama vile Yeye ni Mungu wa aina gani kwa hakika, mapenzi Yake ni nini, tabia Yake ni ipi, na mtazamo Wake wa kihalisia ni upi kwa mwanadamu. Hali hii huhusisha pakubwa imani ya watu katika Mungu—imani yao haiwezi kwa ufupi kufikia utakatifu au ukamilifu. Hata kama utakuwa ana kwa ana na neno la Mungu au kuhisi kwamba umekumbana na Mungu kupitia katika hali zako ulizopitia, bado haiwezi kusemwa kwamba unamwelewa Yeye kabisa. Kwa sababu hujui fikira za Mungu au kile Anachopenda na kile Anachochukia, kile kinachomfanya Yeye kuwa na ghadhabu na kile kinachomletea Yeye furaha, huna ufahamu wa kweli wake Yeye. Imani yako imejengwa katika msingi wa hali isiyokuwa dhahiri na ile ya kufikiria, kwa msingi wa matamanio yako ya dhahania. Bado ingali mbali na imani halisia, na wewe bado ungali mbali na kuwa mfuasi wa kweli. Fafanuzi za mifano kutoka kwenye hadithi hizi za Biblia zimemruhusu binadamu kuujua moyo wa Mungu, kujua ni nini Yeye Alichokuwa akifikiria katika kila hatua ya kazi Yake na kwa nini Yeye aliifanya kazi hii, nia Yake asilia ilikuwa nini na mpango Wake ulikuwa upi Alipofanya kazi ile, namna ambavyo Alifikia fikira Zake na namna Alivyojitayarisha na kuendeleza mpango Wake. Kupitia katika hadithi hizi, tunaweza kupata ufahamu mahususi wenye maelezo ya kina, ya kila nia mahususi ya Mungu na kila wazo halisi wakati wa kazi Yake ya usimamizi ya miaka elfu sita, na mtazamo Wake kwa binadamu katika nyakati tofauti na enzi tofauti. Kuelewa kile ambacho Mungu alikuwa Anafikiria, mtazamo Wake ulikuwa upi na tabia Aliyoifichua alipokuwa Akikumbana na kila hali, kunaweza kumsaidia kila mtu kwa kina zaidi kuweza kutambua kuwepo Kwake kwa hakika, na kuhisi kwa kina zaidi ukweli na uhalisia Wake. Shabaha yangu katika kusimulia hadithi hizi si kwamba watu waweze kuelewa historia ya kibiblia, wala si kuwasaidia kupata uzoefu wa vitabu vya kibiblia au watu walio ndani yake, na hasa si kuwasaidia watu kuelewa maelezo zaidi kuhusu kile ambacho Mungu alifanya katika Enzi ya Sheria. Ni kuwasaidia watu kuelewa mapenzi ya Mungu, tabia Yake, na kila sehemu ndogo Yake, na kuongeza ufahamu na maarifa ya Mungu yenye uhalisia zaidi na usahihi zaidi. Kwa njia hii, mioyo ya watu inaweza, hatua kwa hatua, kufunguka kwa ajili ya Mungu na kuwa karibu zaidi na Mungu, na wanaweza kumwelewa Yeye zaidi, tabia Yake, kiini Chake, na kumjua vema zaidi Mungu wa kweli Mwenyewe.
Ufahamu wa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vinaweza kuwa na athari nzuri kwa binadamu. Vinaweza kuwasaidia kuwa na imani zaidi kwa Mungu, na kuwasaidia kufanikisha utiifu wa kweli na uchaji Kwake. Basi, wao tena si wafuasi wasioona, au wanaomwabudu Yeye tu bila mpango. Mungu hataki wajinga au wale wanaofuata wengine bila mpango lakini Anataka kundi la watu ambao wana ufahamu na maarifa wazi katika mioyo yao kuhusu tabia ya Mungu na wanaweza kuchukua nafasi ya mashahidi wa Mungu, watu ambao hawawezi kamwe kumwacha Mungu kwa sababu ya uzuri Wake, kwa sababu ya kile Alicho nacho na kile Alicho, na kwa sababu ya tabia Yake ya haki. Kama mfuasi wa Mungu, endapo katika moyo wako bado kuna ukosefu wa ubayana, au kuna hali ya tata au mkanganyo kuhusu kuwepo kwa kweli kwa Mungu, tabia Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mpango Wake wa kumwokoa binadamu, basi imani yako haiwezi kupata sifa za Mungu. Mungu hataki mtu wa aina hii kumfuata Yeye, na pia Yeye hapendi mtu wa aina hii akija mbele Yake. Kwa sababu mtu wa aina hii hamwelewi Mungu, hawezi kutoa moyo wake kwa Mungu—moyo wake umemfungwa Kwake, hivyo basi imani yake katika Mungu imejaa kasoro mbalimbali. Kumfuata kwake Mungu kunaweza tu kusemwa kuwa ni kwa kipumbavu. Watu wanaweza kupata imani ya kweli na kuwa wafuasi wa kweli kama watakuwa na ufahamu na maarifa ya kweli wa Mungu, jambo ambalo linaleta utiifu na uchaji wa kweli Kwake. Ni kupitia katika njia hii tu ndio anaweza kuutoa moyo wake kwa Mungu, kuufungua Kwake. Hili ndilo Mungu anataka, kwa sababu kila kitu wanachofaya na kufikiria, kinaweza kustahimili majaribu ya Mungu, na wanaweza kumshuhudia Mungu. Kila kitu Ninachowasilisha kwako kuhusiana na tabia ya Mungu, au kuhusu kile Alicho nacho na kile Alicho, au mapenzi Yake na fikira Zake katika kila kitu Anachofanya, na kutoka kwenye mtazamo wowote ule, kutoka kwa upande wowote ule Ninakizungumzia, yote haya ni kukusaidia kuwa na uhakika zaidi kuhusu uwepo wa kweli wa Mungu, na kuelewa na kushukuru zaidi kwa kweli upendo Wake kwa mwanadamu, na kuelewa na kufahamu vyema zaidi kwa kweli kile anachojali Mungu kuhusu binadamu, na tamanio Lake la dhati la kumsimamia na kumwokoa mwanadamu.
Leo kwanza kabisa tutafanya muhtasari wa fikira, mawazo, na kila hatua ya Mungu tangu Alipomuumba binadamu, na kuangalia ni kazi gani Alitekeleza kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwanzo rasmi wa Enzi ya Neema. Tunaweza basi kugundua ni fikira na mawazo yapi ya Mungu ambayo hayajulikani kwa binadamu, na kuanzia hapo tunaweza kuweka wazi mpangilio wa mpango wa usimamizi wa Mungu na kuelewa kwa kina muktadha ambao kwao Mungu alianzisha kazi Yake ya usimamizi, chanzo chake na mchakato wake wa maendeloe, na pia kuelewa kwa undani ni matokeo yapi Anayotaka kutoka katika kazi Yake ya usimamizi—yani, kiini na kusudio la kazi Yake ya usimamizi. Kuelewa mambo haya tunahitaji kurudi hadi ule wakati wa kitambo, mtulivu na kimya wakati ambapo hakukuwa na binadamu …
Wakati Mungu alipoinuka kutoka kitandani Mwake, fikira ya kwanza Aliyokuwa nayo ilikuwa hii: kumuumba binadamu hai, halisia, binadamu anayeishi—mtu wa kuishi naye na kuwa mwenzake Yeye wa kila mara. Mtu huyu angemsikiliza Yeye, na Mungu angempa siri Zake na kuongea na yeye. Kisha, kwa mara ya kwanza Mungu aliuchukua udongo kwenye mkono na kuutumia kumuumba mtu wa kwanza kabisa aliye hai ambaye Alikuwa amemfikiria, na kisha Akakipa kiumbe hiki hai jina—Adamu. Punde Mungu alipompata mtu huyu aliye hai na anayepumua, Alihisi vipi? Kwa mara ya kwanza, Alihisi furaha ya kuwa na mpendwa, na mwandani. Aliweza kuhisi pia kwa mara ya kwanza uwajibikaji wa kuwa baba pamoja na kujali kunakoandamana na hisia hizo. Mtu huyu aliye hai na anayepumua alimletea Mungu furaha na shangwe; Alihisi Amefarijika kwa mara ya kwanza. Hili lilikuwa jambo la kwanza ambalo Mungu aliwahi kufanya ambalo halikukamilishwa kwa fikira Zake au hata matamshi Yake, lakini lilifanywa kwa mikono Yake miwili. Wakati kiumbe aina hii—mtu aliye hai na anayepumua—kiliposimama mbele ya Mungu, kilichoumbwa kwa nyama na damu, kilicho na mwili na umbo, na kilichoweza kuongea na Mungu, Alihisi aina ya shangwe ambayo Hakuwa amewahi kuhisi kabla. Kwa kweli alihisi kwamba uwajibikaji Wake na kiumbe hiki hai haukuwa na uhusiano tu katika moyo Wake, lakini kila jambo dogo alilofanya pia liliugusa moyo Wake na likaupa moyo Wake furaha. Kwa hivyo wakati kiumbe hiki hai kiliposimama mbele ya Mungu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuwahi kufikiria kuwapata watu wengi zaidi kama hawa. Huu ndio uliyokuwa msururu wa matukio ulioanza kwa fikira hii ya kwanza ambayo Mungu alikuwa nayo. Kwa Mungu, matukio haya yote yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza, lakini katika matukio haya ya kwanza, haijalishi vile Alivyohisi wakati huo—furaha, uwajibikaji, kujali—hakukuwa na yeyote yule wa kushiriki furaha hii na Yeye. Kuanzia wakati huo, Mungu alihisi kwa kweli upweke na huzuni ambao Hakuwahi kuwa nao mbeleni. Alihisi kwamba binadamu wasingekubali au kuelewa mapenzi Yake na kujali Kwake, au nia Zake kwa mwanadamu, hivyo basi Alihisi huzuni na maumivu katika moyo Wake. Ingawa Alikuwa amefanya mambo haya kwa binadamu, binadamu hakuwa na habari na wala hakuelewa. Mbali na furaha, shangwe na hali njema ambayo binadamu alimletea pia viliandamana kwa haraka na hisia Zake za kwanza za huzuni na upweke. Hizi ndizo zilizokuwa fikira na hisia za Mungu wakati huo. Wakati Mungu alipokuwa akifanya mambo haya yote, katika moyo Wake Alitoka katika furaha Akaingia katika huzuni na kutoka katika huzuni Akaingia katika maumivu, vyote vikiwa vimechanganyika na wasiwasi. Kile Alichotaka kufanya tu kilikuwa kuharakisha kumruhusu mtu huyu, kizazi hiki cha binadamu kujua ni nini kilichokuwa moyoni Mwake na kuelewa nia Zake haraka iwezekanavyo. Kisha, wangekuwa wafuasi Wake na kupatana na Yeye. Wasingemsikiliza tena Mungu akiongea na kubakia kimya; wasingeendelea kutojua namna ya kujiunga na Mungu katika kazi Yake, na zaidi ya yote, wasingekuwa tena watu wasiojali na kuelewa mahitaji ya Mungu. Mambo haya ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ni yenye maana sana na yanashikilia thamani nyingi kwa minajili ya mpango Wake wa usimamizi na ule wa binadamu leo.
Baada ya kuviumba viumbe vyote na binadamu, Mungu hakupumzika. Asingesubiri kuutekeleza usimamizi Wake wala Asingeweza kusubiri kuwapata watu Aliowapenda mno miongoni mwa wanadamu.
Kishasi kipindi kirefu baada ya Mungu kuwaumba binadamu, tunaona kutoka katika Biblia ya kwamba kulikuwa na gharika kubwa kote ulimwenguni. Nuhu anatajwa kwenye rekodi ya gharika, na inaweza kusemekana kwamba Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuitikia mwito wa Mungu ili afanye kazi na Yeye ili kukamilisha kazi ya Mungu. Bila shaka, wakati huo ndio uliokuwa pia wa kwanza kwa Mungu kumwita mtu ulimwenguni kufanya kitu kulingana na amri Yake. Mara tu Nuhu alipokamilisha kuijenga safina, Mungu alileta gharika katika nchi kwa mara ya kwanza. Wakati Mungu alipoiharibu nchi kwa gharika, ndiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu kuviumba viumbe ambapo Alihisi kuzidiwa na maudhi kwa binadamu; hili ndilo lililomlazimu Mungu kufanya uamuzi wenye maumivu wa kuharibu kizazi hiki cha binadamu kupitia kwa gharika. Baada ya gharika kuiharibu nchi, Mungu alifanya agano Lake la kwanza na binadamu kwamba Hatawahi kufanya hivi tena. Ishara ya agano hili ilikuwa upinde wa mvua. Hili ndilo lililokuwa agano la kwanza la Mungu na mwanadamu, hivyo basi upinde wa mvua ndio uliokuwa ishara ya kwanza ya agano lililotolewa na Mungu; upinde huu wa mvua ni jambo la kihalisia, jambo ambalo lipo hakika. Ni kule kuwepo kabisa kwa upinde huu wa mvua ambako humfanya Mungu mara nyingi kuhisi huzuni kutokana na kizazi cha binadamu cha awali ambacho Amepoteza, na huwa ni kumbusho la kila mara kwake Yeye kuhusiana na kile kilichowafanyikia. … Mungu asingepunguza mwendo Wake—Asingesubiri kuchukua hatua ya kufuata katika usimamizi Wake. Hivyo basi, Mungu alimchagua Ibrahimu kama chaguo Lake la kwanza kwa kazi yake kotekote Israeli. Hii ndiyo iliyokuwa pia mara ya kwanza kwa Mungu kumchagua mteuliwa kama huyo. Mungu aliamua kuanza kutekeleza kazi Yake ya kumwokoa mwanadamu kupitia kwa mtu huyu, na kuendeleza kazi Yake miongoni mwa vizazi vya mtu huyu. Tunaweza kuona katika Biblia kwamba hivi ndivyo Mungu alivyomfanyia Ibrahimu. Basi Mungu akaifanya Israeli kuwa nchi ya kwanza iliyochaguliwa, na Akaianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria kupitia kwa watu Wake waliochaguliwa, Waisraeli. Tena kwa mara ya kwanza, Mungu aliwapa Waisraeli sheria na kanuni za moja kwa moja ambazo mwanadamu anafaa kufuata, na Akazieleza kwa kina. Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpatia binadamu sheria kama hizo mahususi na wastani kuhusu namna wanavyofaa kutoa kafara, namna wanavyofaa kuishi, kile wanachofaa kufanya na kutofanya, ni sherehe na siku gani wanazofaa kutilia maanani, na kanuni za kufuata katika kila kitu walichofanya. Hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpa mwanadamu taratibu na kanuni hizo zenye maelezo na uwastani kwa ajili ya maisha yao.
Ninaposema “mara ya kwanza,” inamaanisha Mungu hakuwa Amewahi kukamilisha kazi kama hiyo tena. Ni kitu ambacho hakikuwepo awali, na hata ingawa Mungu alikuwa Amemuumba mwanadamu na Alikuwa Ameumba aina zote za viumbe na vitu vyenye uhai, hakuwahi kukamilisha aina hiyo ya kazi. Usimamizi wa Mungu kwa binadamu; yote ilihusu binadamu na wokovu Wake na usimamizi wa binadamu. Baada ya Ibrahimu, Mungu alifanya chaguo tena kwa mara ya kwanza—Alimchagua Ayubu kuwa ndiye chini ya sheria ndiye ambaye angestahimili majaribio ya Shetani huku akiendelea kumcha Mungu na kujiepusha na uovu na kuweza kumtolea Yeye ushuhuda. Hii pia ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kuruhusu Shetani kumjaribu mtu na mara ya kwanza Alipoweka dau na Shetani. Mwishowe, kwa mara ya kwanza, Mungu alimpata mtu aliyekuwa na uwezo wa kusimama kama shahidi Wake huku akiwa amemkabili Shetani—mtu ambaye angeweza kumshuhudia Yeye na kumwaibisha kabisa Shetani. Tangu Mungu alipomuumba mwanadamu, huyu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza, aliyempata ambaye aliweza kumshuhudia Yeye. Punde alipokuwa amempata mtu huyu, Mungu alikuwa na hata hamu zaidi ya kuendeleza usimamizi Wake na kuchukua hatua inayofuata katika kazi Yake, Akitayarisha chaguo Lake lifuatalo na mahali Pake pa kazi.
Baada ya kukuonyesha kuhusu haya yote, je, unao ufahamu wa kweli wa mapenzi ya Mungu? Mungu anaona tukio hili la usimamizi wa mwanadamu, wa kuwaokoa wanadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia matamshi Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa mwanadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi ukubwa wa changamoto zilivyo, haijalishi ni vipi ambavyo binadamu ni wanyonge, au ni vipi mwanadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha binadamu bila kuficha bidii Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anafichua bila kuacha chochote haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …
Baada ya kusikia haya yote leo, unaweza kuhisi kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni kawaida sana. Yaonekana kwamba binadamu siku zote wamehisi mapenzi fulani ya Mungu kwao kutokana na matamshi Yake na pia kazi Yake, lakini siku zote kuna umbali fulani katikati ya hisia zao au maarifa yao na kile ambacho Mungu anafikiria. Kwa hivyo, Nafikiri ni muhimu kuwa na mawasiliano na watu wote kuhusu ni kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu, na maelezo zaidi yanayoonyesha tamanio Lake la kuwapata watu aliokuwa Akitumainia. Ni muhimu kushiriki habari hii na kila mmoja, ili kila mmoja aweze kuwa uwazi katika moyo wake. Kwa sababu kila fikira na wazo la Mungu, na kila awamu na kila kipindi cha kazi Yake vinafungamana ndani ya, na vyote hivi vimeunganishwa kwa karibu na, usimamizi Wake mzima wa kazi, unapoelewa fikira mawazo ya Mungu, na mapenzi Yake katika kila hatua ya kazi Yake, ni sawa na ufahamu wa chanzo cha kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Ni katika msingi huu ndipo ufahamu wako wa Mungu unapoanza kuwa wa kina. Ingawa kila kitu ambacho Mungu alifanya Alipoumba kwanza ulimwengu ambacho Nilitaja awali ni taarifa fulani tu kwa watu sasa na yaonekana kwamba hayana umuhimu sana katika utafutaji wa ukweli, katika mkondo wa kile ambacho utapitia kutakuwa na siku ambapo hutafikiria kuwa ni jambo rahisi sana kama mkusanyiko tu wa taarifa, wala kwamba ni kitu rahisi sana kama mafumbo fulani. Kwa kadri maisha yako yanavyoendelea na pale ambapo pana msimamo kidogo wa Mungu katika moyo wako, au unapokuja kuelewa waziwazi na kwa kina mapenzi Yake, utaweza kuelewa kwa kweli umuhimu na haja ya kile Ninachozungumzia leo. Haijalishi ni kwa kiwango kipi umeyakubali haya; ni muhimu kwamba uelewe na ujue mambo haya. Wakati Mungu anapofanya jambo, wakati Anapotekeleza kazi Yake, haijalishi kama amefanya na mawazo Yake au kwa mikono Yake, haijalishi kama ni mara ya kwanza ambapo Amelifanya au kama ni mara ya mwisho—mwishowe, Mungu anao mpango, na kusudio Lake na fikira Zake vyote vimo katika kila kitu Anachokifanya. Makusudio na fikira hizi zinawakilisha tabia ya Mungu, na zinaonyesha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vitu hivi viwili—tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho—lazima vieleweke na kila mmoja. Punde mtu anapoelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ataanza kuelewa kwa utaratibu ni kwa nini Mungu anafanya kile Anachofanya na kwa nini Anasema kile Anachosema. Kutokana na hayo, anaweza kuwa na imani zaidi ya kumfuata Mungu, kuufuatilia ukweli, na kufuatilia mabadiliko katika tabia. Hivi ni kusema, ufahamu wa binadamu kuhusu Mungu na imani yake katika Mungu ni vitu viwili visivyoteganishwa.
Hata ingawa kile watu wanachosikia kuhusu au kupata ufahamu huo ni tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, kile wanachofaidi ni maisha yanayotoka kwa Mungu. Baada ya maisha haya kuhemshwa ndani yako, uchaji wako wa Mungu utakuwa mkubwa zaidi na zaidi, na kuvuna mavuno haya kunafanyika kwa kawaida sana. Kama hutaki kuelewa au kujua kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake, kama hutaki hata kutafakari juu ya au kuzingatia mambo haya, Ninaweza kukuambia kwa hakika kwamba hiyo njia unayoifuatilia katika imani yako kwa Mungu haitawahi kukuruhusu kuridhisha mapenzi Yake au kupata sifa Zake. Zaidi ya hayo, huwezi kamwe kufikia wokovu—hizi ndizo athari za mwisho. Wakati watu hawamwelewi Mungu na hawajui tabia Yake, mioyo yao haiwezi kamwe kuwa wazi Kwake. Punde wanapomwelewa Mungu, wataanza kuelewa na kufurahia kile kilicho moyoni Mwake kwa kivutio na imani. Unapoelewa na kufurahia kile kilichomo ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utaanza kwa utaratibu, kidogokidogo, kuwa wazi Kwake. Wakati moyo wako unakuwa wazi Kwake, utahisi namna ambavyo mabadilishano yako na Mungu yatakavyokuwa ya aibu na duni, madai yako kutoka kwa Mungu na matamanio yako mengi binafsi. Wakati moyo wako unapofunguka kwa kweli kwa Mungu, utaona kwamba moyo Wake ni ulimwengu usio na mwisho, na utaingia katika ulimwengu ambao hujawahi kuupitia awali. Katika ulimwengu huu hakuna udanganyifu, hakuna ujanja, hakuna giza, hakuna maovu. Kunao ukweli wa dhati na uaminifu; kunayo nuru na uadilifu tu; kunayo haki na huruma. Umejaa upendo na utunzaji, umejaa rehema na uvumilivu, na kupitia katika ulimwengu huu utahisi shangwe na furaha ya kuwa hai. Mambo haya ndiyo ambayo Atakufichulia utakapoufungua moyo wako kwa Mungu. Hii dunia isiyo na kikomo imejaa hekima ya Mungu, Na imejaa hali Yake ya kuwa kila pahali; umejaa pia upendo Wake na mamlaka Yake. Hapa unaweza kuona kila dhana ya kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, ni nini kinachomletea Yeye shangwe, kwa nini Anakuwa na wasiwasi na kwa nini Anakuwa na huzuni, kwa nini Anakuwa na hasira…. Haya ndiyo ambayo kila mmoja anaweza kuona anayeufungua moyo wake na kumruhusu Mungu kuingia ndani. Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako kama utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako. Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile Alicho nacho na kile Alicho kina thamani sana ya kuthaminiwa. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vifaa na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna kifaa chochote cha anasa ambacho kitaweza kukuvuta kwacho tena, na vitu hivi haviwezi kukufanya kuvilipia gharama yoyote tena. Kwa unyenyekevu wa Mungu utaona ukubwa Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya uliloliamini kuwa dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake. Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokufanyikia katika maisha yako, na hata kwa wale unaopenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu unayethamini zaidi. Wakati siku hiyo itawadia, Ninaamini kwamba kutakuwa na baadhi ya watu watakaosema: Upendo wa Mungu ni mkubwa na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna ujanja, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu Alicho nacho Mungu na kile Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na na kuwa na hamu ya kuvipata. Ni katika msingi gani uwezo wa mwanadamu wa kutimiza haya umejengwa? Unajengewa katika msingi wa ufahamu wa binadamu katika tabia ya Mungu, na ufahamu wao kuhusu kiini cha Mungu. Hivyo basi kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, ni funzo la maisha yote kwa kila mtu na ni shabaha ya maisha yote linalofuatiliwa na kila mtu anayelenga kubadilisha tabia yake, na kutamani kumjua Mungu.
Tumezungumza tu kuhusu kazi yote ambayo Mungu amekamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia binafsi ya Mungu na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa bora zaidi kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele kulinganga na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema. Katika enzi hii, Mungu tena Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza. Kazi katika enzi hii mpya kwa Mungu na hata kwa mwanadamu ilikuwa sehemu mpya ya kuanzia. Sehemu hii mpya ya kuanzia ilikuwa tena kazi mpya ambayo Mungu alifanya kwa mara ya kwanza. Kazi hii mpya ilikuwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea ambacho Mungu alitekeleza na hakikufikirika na binadamu na viumbe vyote.Ni kitu ambacho kwa sasa kinajulikana kwa wote—hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu aligeuka kuwa binadamu, mara ya kwanza Alianza kazi mpya kwa umbo la binadamu, Akiwa na utambulisho wa mwanamume. Kazi hii mpya ilionyesha kwamba Mungu alikuwa Amekamilisha kazi Yake katika Enzi ya Sheria, kwamba Asingefanya au kusema tena chochote kulingana sheria. Wala Asingewahi tena kuzungumza au kufanya chochote kwa mfano wa sheria au kulingana na kanuni au masharti ya sheria. Yaani, kazi Yake yote inayotokana na sheria ilisitishwa milele na isingeendelezwa, kwa sababu Mungu alitaka kuanza kazi mpya na kufanya mambo mapya, na mpango Wake kwa mara nyingine tena ulikuwa na sehemu mpya ya kuanzia. Hivyo basi, Mungu lazima Angemwongoza mwanadamu hadi katika enzi inayofuata.
Kama hizi zilikuwa habari za shangwe au za kisirani kwa binadamu ilitegemea kiini chao kilikuwa kipi. Inaweza kusemekana kwamba hizi hazikuwa habari za shangwe, lakini zilikuwa habari za kisirani kwa baadhi ya watu, kwa sababu wakati Mungu alipoanza kazi Yake mpya, watu hao ambao walifuata tu sheria na masharti, ambao walifuata tu kanuni lakini hawakumcha Mungu wangeegemea upande wa kutumia kazi nzee ya Mungu ili kuishutumu kazi Yake mpya. Kwa watu hawa, hizi zilikuwa habari za kisirani; lakini kwa kila mtu aliyekuwa hana hatia na aliyekuwa wazi, aliyekuwa mwenye ukweli na mwaminifu kwa Mungu na aliyekuwa radhi kupokea ukombozi Wake, Mungu kuwa mwili kwa mara ya kwanza zilikuwa habari zenye shangwe sana. Kwani tangu hapo kuliwahi kuwepo na binadamu, hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu kuonekana na kuishi miongoni mwa wanadamu katika umbo ambalo halikuwa Roho; badala yake, Alizaliwa na mwanadamu na kuishi miongoni mwa watu kama Mwana wa Adamu, na kufanya kazi katikati yao. Hii “mara ya kwanza” ilizivunja dhana za watu na pia ilikuwa zaidi ya kufikiria kote. Aidha, wafuasi wote wa Mungu walipata manufaa ya kushikika na kuonekana. Mungu hakuikomesha tu enzi nzee, lakini pia Alikomesha mbinu Zake za kale za kufanya kazi pamoja na mitindo ya kufanya kazi. Hakuruhusu tena wajumbe Wake kuwasilisha kile Alicho, na hakufichika tena katika mawingu na hakuonekana tena au kuongea kwa binadamu kupitia kwa ishara za amri kwa “radi.” Tofauti na chochote kile cha awali, kupitia kwa mbinu ambayo haikufirika kwa binadamu ambayo pia ilikuwa ngumu kwa wao kuelewa na kukubali—kupata mwili—Aligeuka na kuwa Mwana wa Adamu ili kuendeleza kazi ya enzi hiyo. Hatua hii ilimshangaza mwanadamu, na ikawa pia isiyo na utulivu kwao, kwa sababu Mungu kwa mara nyingine alikuwa ameanza kazi mpya ambayo hakuwahi kufanya tena. Leo, tutaangalia ni kazi gani mpya ambayo Mungu alikamilisha katika enzi mpya, na katika haya yote ya kazi mpya, tabia ya Mungu nayo ilikuwa vipi, na nini Alicho nacho na kile Alicho ambayo tunaweza kuelewa?
Yafuatayo ni maneno yaliyorekodiwa katika Agano Jipya la Biblia.
1. (Mat 12:1) Wakati ule Yesu alipita katika mashamba ya mahindi siku ya sabato; na wanafunzi wake walihisi njaa, wakaanza kuvunja masuke ya mahindi na kuyala.
2. (Mat 12:6-8) Lakini nawaambia, Kwamba mahali hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. Lakini kama mngalijua maana ya hili, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa sabato.
Hebu kwanza tuangalie dondoo hii: “Wakati ule Yesu alipita katika mashamba ya mahindi siku ya sabato; na wanafunzi wake walihisi njaa, wakaanza kuvunja masuke ya mahindi na kuyala.”
Kwa nini tumeichagua dondoo hii? Dondoo hii ina uhusiano upi na tabia ya Mungu? Katika maandiko haya kitu cha kwanza tunachojua ni kwamba ilikuwa ni siku ya Sabato, lakini Bwana Yesu alipita kule nje na kuwaongoza wanafunzi Wake katika mashamba ya masuke. Lakini zaidi “cha kufedhehesha” ni kwamba waliweza hata “kuvunja masuke ya mahindi na kuyala.” Katika Enzi ya Sheria, sheria za Yehova Mungu zilikuwa kwamba watu wasingeweza kuenda vivi hivi tu au kushiriki katika shughuli za Sabato—kulikuwa na mambo mengi ambayo hayangefanywa siku ya Sabato. Hatua hii ya Bwana Yesu ilikuwa ya kuchanganya hasa kwa wale waliokuwa wameishi chini ya sheria kwa muda mrefu, na iliweza hata kuchochea upinzani mkubwa. Kuhusiana na mchanganyiko wao na namna walivyouzungumzia kile ambacho Yesu alifanya, tutaweka hilo pembeni kwa sasa na kuzungumzia kwanza kwa nini Bwana Yesu alichagua kufanya hivi katika siku ya Sabato, kwa siku zote, na kile Alichotaka kuwasilisha kwa watu waliokuwa wakiishi katika enzi ya kale kupitia katika hatua hii. Huu ndio uhusiano kati ya dondoo hii na tabia ya Mungu ambayo Ningependa kuzungumzia.
Wakati Bwana Yesu alipokuja, Alitumia vitendo Vyake vya kihalisia kuweza kuwasiliana na watu: Mungu alikuwa ameiondoa Enzi ya Sheria na alikuwa ameanza kazi mpya, na kazi hii mpya haikuhitaji uadhimisho wa Sabato; wakati Mungu alipotoka katika mipaka ya siku ya Sabato, hicho kilikuwa tu kionjo cha mapema cha kazi Yake mpya, na kwa kweli kazi Yake kubwa ilikuwa ikiendelea kujitokeza. Wakati Bwana Yesu aliopanza kazi Yake, tayari Alikuwa ameacha nyuma zile pingu za Enzi ya Sheria, na alikuwa ametupilia mbali zile taratibu na kanuni zilizokuwa za enzi hiyo. Ndani yake hakuwa na dalili za chochote kuhusiana na sheria; Alikuwa ameitupa nje mzima mzima na hakuifuata tena, na Hakuhitaji tena mwanadamu kuifuata. Kwa hivyo hapa unamwona Bwana Yesu akipita katika mashamba siku ya Sabato; Bwana hakupumzika lakini, alikuwa akipita kule nje akifanya kazi. Hatua hii Yake ilikuwa ya kushtua kwa dhana za watu na iliweza kuwawasilishia ujumbe kwamba Hakuishi tena chini ya sheria na kwamba Alikuwa ameacha ile mipaka ya Sabato na kujitokeza mbele ya mwanadamu na katikati yao katika taswira mpya, huku akiwa na njia mpya ya kufanya kazi. Hatua hii Yake iliwaambia watu kwamba Alikuwa ameleta pamoja Naye kazi mpya iliyoanza kwa kwenda nje ya sheria na kwenda nje ya Sabato. Wakati Mungu alitekeleza kazi Yake mpya, Hakushikilia tena ya kale, na Hakujali tena kuhusu taratibu za Enzi ya Sheria. Wala Hakuathirika na kazi Yake mwenyewe katika enzi ya awali, lakini Alifanya kazi kwa kawaida katika siku ya Sabato na wakati wanafunzi Wake walipoona njaa, waliweza kuvunja masuke na wakala. Haya yote yalikuwa kawaida sana machoni mwa Mungu. Mungu angeweza kuwa na mwanzo mpya kwa nyingi za kazi Anazotaka kufanya na mambo Anayotaka kusema. Punde Anapokuwa na mwanzo mpya, Hataji kazi Yake ya awali tena wala kuiendeleza. Kwani Mungu anazo kanuni Zake katika kazi Yake. Wakati Anapotaka kuanzisha kazi mpya, ndipo Anapotaka kumleta mwanadamu katika awamu mpya ya kazi Yake, na wakati kazi Yake imeingia katika awamu ya juu zaidi. Kama watu wanaendelea kutenda kulingana na misemo au taratibu za kale au kuendelea kushikilia kabisa kwazo, Hatakumbuka au kulisifu jambo hili. Hii ni kwa sababu tayari Ameileta kazi mpya, na ameingia katika awamu mpya ya kazi Yake. Wakati Anapoanzisha kazi mpya, Anaonekana kwa mwanadamu akiwa na taswira mpya kabisa, kutoka katika mtazamo mpya kabisa, na kwa njia mpya kabisa ili watu waweze kuona dhana zile tofauti za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hii ni mojawapo ya shabaha zake katika kazi Yake mpya. Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia isiyotumika na wengi; wakati Anapofanya kazi na kuongea hakatazi chochote kama vile watu wanavyofikiria. Ndani ya Mungu, yote ni huru na yamekombolewa, na hakuna hali ya kukinga, hakuna vizuizi—kile Anachomletea mwanadamu ni uhuru na ukombozi. Yeye ni Mungu aliye hai, Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo. Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo, na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu. Yeye Yu hai na mwenye nguvu na kile ambacho maneno Yake na kazi Yake humletea binadamu yote ni uzima na nuru, uhuru na ukombozi wote, kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajabanwa na chochote katika kazi yoyote Yake. Bila kujali watu wanavyosema na namna wanavyoona au kukadiria kazi Yake mpya, Ataitekeleza kazi Yake bila wasiwasi wowote. Hatakuwa na wasiwasi kuhusu dhana zozote za yeyote au kazi na maneno Yake kuelekezewa vidole, au hata upinzani wao mkubwa katika kazi Yake mpya. Hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyote anayeweza kutumia akili ya binadamu, au kufikiria kwa binadamu, maarifa au maadili ya binadamu kupima au kufasili kile ambacho Mungu anafanya, kutia fedheha, au kutatiza au kukwamiza kazi Yake. Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachofanya, na haitawekewa kubanwa kokote na binadamu yeyote, kitu chochote, au kifaa chochote, na haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili. Katika kazi Yake mpya, yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za kikatili na uvumi wote na hoja za uwongo zote kutoka kwa mwanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu. Haijalishi ni hatua gani mpya ya kazi Yake ambayo Anatekeleza, lazima iendelezwe na ipanuliwe katika mwanadamu, na lazima itekelezwe bila kuzuiliwa kotekote ulimwenguni mpaka pale kazi Yake kubwa imekamilika. Huu ndio uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu Zake. Hivyo basi, Bwana Yesu angeweza kwenda kule nje waziwazi na kufanya kazi katika siku ya Sabato kwa sababu ndani ya moyo Wake hakukuwa na sheria zozote, na hakukuwa na maarifa au kanuni zozote zilizotokana na mwanadamu. Kile Alichokuwa nacho kilikuwa ni kazi mpya ya Mungu na njia Yake, na kazi Yake ndio iliyokuwa njia ya kumweka huru mwanadamu, kumwachilia, kumruhusu kuwepo katika nuru na kumruhusu kuishi. Na wale wanaoabudu sanamu au miungu ya uwongo wanaishi kila siku wakiwa wamefungwa na Shetani, wakiwa wamezuiliwa na aina zote za sheria na mila—leo kitu kimoja hakiruhusiwi, kesho kingine—hakuna uhuru katika maisha yao. Wao ni sawa na wafungwa katika pingu wasio na shangwe ya kuzungumzia. “Kuzuiliwa” inawakilisha nini? Inawakilisha shurutisho, utumwa na uovu. Punde tu mtu anapoabudu sanamu, anaabudu mungu wa uwongo, kumwabudu roho wa uovu. Kuzuiliwa kunaenda sambamba na hilo. Huwezi kula hiki au kile, leo huwezi kwenda nje, kesho huwezi kuwasha jiko lako, siku inayofuata huwezi kuhamia katika nyumba mpya, siku fulani lazima zichaguliwe kwa minajili ya harusi na mazishi, na hata za wakati wa kujifungua mtoto. Haya yote yanaitwa nini? Haya yanaitwa kuzuiliwa; ni utumwa wa mwanadamu, na ndizo pingu za maisha za Shetani na roho wa maovu wanaowadhibiti, na wanaozuilia mioyo yao na mili yao. Je, kuzuiliwa huku kunapatikana kwa Mungu? Wakati tunapozungumzia utakatifu wa Mungu, unafaa kwanza kufikira haya: Kwa Mungu hakuna kuzuiliwa. Mungu anazo kanuni katika maneno na kazi Yake, lakini hakuna kuzuiliwa, kwa sababu Mungu Mwenyewe ndiye ukweli, njia na uzima.
Sasa hebu tuangalie dondoo ifuatayo: “Lakini nawaambia, Kwamba mahali hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. Lakini kama mngalijua maana ya hili, Nataka rehema, wala si sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa sabato.” (Mat 12:6-8). “Hekalu” hapa inamaanisha nini? Kwa ufupi, “hekalu” inaashiria jengo refu la kupendeza, na katika Enzi ya Sheria, hekalu lilikuwa ni pahali pa makuhani kumwabudu Mungu. Wakati Bwana Yesu aliposema “hapa yupo mmoja aliye mkuu kuliko hekalu,” “mmoja” ilikuwa ikirejelea nani? Ni wazi, “mmoja” ni Bwana Yesu katika mwili kwa sababu Yeye tu ndiye aliyekuwa mkuu kuliko hekalu. Na maneno hayo yaliwaambia watu nini? Yaliwaambia watu watoke hekaluni—Mungu alikuwa tayari ameshatoka nje na hakuwa tena akifanyia kazi ndani yake, hivyo basi watu wanafaa kutafuta nyayo za Mungu nje ya hekalu na kufuata nyayo Zake katika kazi Yake mpya. Usuli wa Bwana Yesu kusema haya ilikuwa kwamba chini ya sheria, , watu walikuwa wameiona hekalu kama kitu kilichokuwa kikuu zaidi kuliko Mungu Mwenyewe. Yani, watu waliliabudu hekalu badala ya kumwabudu Mungu, hivyo basi Bwana Yesu akawaonya kutoabudu sanamu, lakini kumwabudu Mungu kwa sababu Yeye ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi. Hivyo basi, alisema: “Nataka rehema, na wala si sadaka.” Ni wazi kwamba katika macho ya Bwana Yesu, watu wengi sana katika sheria hawakumwabudu tena Yehova, lakini walikuwa tu wakipitia mchakato wa kutoa sadaka na Bwana Yesu aliamua kwamba mchakato huu ulikuwa “ibada ya sanamu.” Waabudu sanamu hawa waliliona hekalu kama kitu kikuu, cha juu zaidi kuliko Mungu. Ndani ya mioyo yao kulikuwa tu na hekalu, wala si Mungu, na kama wangelipoteza hekalu, wangepoteza mahali pao pa kukaa. Bila ya hekalu hawakuwa na mahali popote pa kuabudu na wasingeweza kutoa sadaka zao. Mahali pao pa kukaa kama palivyojulikana ndipo walipofanyia shughuli zao kwa jina la kumwabudu Yehova Mungu, na hivyo basi wakaruhusiwa kuishi katika hekalu na kutekeleza shughuli zao binafsi. Ule utoaji sadaka kama ulivyojulikana ulikuwa tu kutekeleza shughuli zao za kibinafsi za aibu wakisingizia kwamba walikuwa wanaendesha ibada yao katika hekalu. Hii ndiyo iliyokuwa sababu iliyowafanya watu wakati huo kuliona hekalu kuwa kuu kuliko Mungu. Kwa sababu walilitumia hekalu kama maficho, na sadaka kama kisingizio cha kuwadanganya watu na kumdanganya Mungu, naye Bwana Yesu akasema haya ili kuwapa onyo watu hao. Mkitumia maneno haya kwa wakati wa sasa, yangali bado halali na yenye umuhimu sawa. Ingawa watu wa leo wameweza kupitia kazi tofauti za Mungu kuliko watu wa Enzi ya Sheria walivyowahi kupitia, kiini cha asili yao ni kile kile. Katika muktadha wa kazi leo, watu bado watafanya aina sawa ya mambo kama yale ya “hekalu kuwa kuu kuliko Mungu.” Kwa mfano, watu huona kutimiza wajibu wao kama kazi yao; wanaona kutoa ushuhuda kwa Mungu na kupigana na joka kubwa jekundu kama harakati ya kisiasa ya kulinda haki za kibanadamu, kwa ajili ya demokrasia na uhuru; wao hugeuza wajibu wao ili kutumia weledi wao kuwa ajira, lakini wanachukulia kumcha Mungu na kujiepusha na maovu tu kama kipande cha kanuni ya kidini ya kufuatwa; na kadhalika. Je, maonyesho haya kutoka kwa na binadamu hasa hayako sawa na “hekalu ni kuu kumliko Mungu”? Isipokuwa tu kwamba miaka elfu mbili iliyopita, watu walikuwa wakiendeleza shughuli zao za kibinafsi katika hekalu linaloshikika, lakini leo, watu wanaendeleza shughuli zao za kibinafsi katika mahekalu yasiyogusika. Wale watu wanaothamini masharti huona masharti kuwa kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda hadhi huona hadhi kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda ajira zao huziona ajira hizo kuwa kuu zaidi kuliko Mungu na kadhalika—maonyesho yao yote yananifanya Mimi kusema: “Watu humsifu Mungu kuwa ndiye mkuu zaidi kupitia kwa maneno yao, lakini kupitia kwa macho yao kila kitu ni kikuu zaidi kuliko Mungu.” Hii ni kwa sababu punde tu watu wanapopata fursa katika njia yao ya kumfuata Mungu ili kuonyesha vipaji vyao, au kuendelea na shughuli zao binafsi za kibiashara au ajira yao binafsi, wanakuwa mbali na Mungu na kufanya kwa bidii ajira wanayoipenda. Kuhusiana na kile ambacho Mungu amewaaminia, na mapenzi Yake, mambo hayo yote yametupiliwa mbali kitambo. Katika hali hii, ni nini tofauti baina ya watu hawa na wale wanaoendesha biashara zao katika hekalu miaka elfu mbili iliyopita.
Kisha, hebu tuangalie sentensi ya mwisho katika dondoo hii ya maandiko: “Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa siku ya sabato.” Je, kunao upande wa kimatendo wa sentensi hii? Je, unaweza kuona upande wa kimatendo wa sentensi hii? Kila kitu anachosema Mungu kinatoka moyoni Mwake, kwa hivyo kwa nini alisema hivi? Unaielewa vipi sentensi hii? Unaweza kuelewa maana ya sentensi hii sasa, lakini wakati huo si watu wengi walikuwa wanaielewa kwa sababu mwanadamu alikuwa tu ametoka katika Enzi ya Sheria. Kwa wao, kutoka katika Sabato kulikuwa jambo gumu sana kufanya, sembuse kuelewa Sabato ya kweli ilikuwa nini.
Sentensi “Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa siku ya sabato” inawaambia watu kwamba kila kitu cha Mungu ni visivyo vya mwili, na ingawa Mungu anaweza kukupa mahitaji yako yote ya kimwili, punde tu mahitaji yako yote ya mwili yametimizwa, utoshelevu unaotokana na mambo haya unaweza kuchukua nafasi ya ufuatiliaji wako wa ukweli? Kwa kweli hiyo haiwezekani! Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo tumeweza kushiriki pamoja ni kweli. Haiwezi kupimwa kupitia kwa gharama ya juu ya vifaa vya kimwili wala thamani yake kupimwa kwa pesa, kwa sababu si kifaa cha anasa, na kinatoa mahitaji ya moyo wa kila mmoja. Kwa kila mmoja, thamani ya ukweli huu usioshikika inafaa kuwa kubwa zaidi kuliko thamani ya vitu vyovyote vya anasa unavyofikiria kuwa ni vizuri, sivyo? Kauli hii ni kitu unachohitaji kukiwazia. Hoja kuu ya kile nilichosema ni kwamba kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho na kila kitu cha Mungu ndivyo vitu muhimu zaidi kwa kila mtu na haviwezi kubadilishwa na kifaa chochote cha anasa. Nitakupa mfano: Ukiwa na njaa, unahitaji chakula. Chakula hiki kinaweza kuwa kizuri kwa kiasi fulani au kinaweza kuwa kimekosa kitu fulani kwa kiasi fulani, lakini mradi tu umekula ukashiba, hisia ile mbaya ya kuwa na njaa haitakuwepo tena—itakuwa imeondoka. Unaweza kuketi pale kwa amani, na mwili wako utakuwa umepumzika. Njaa ya watu inaweza kutatuliwa kwa chakula, lakini ukiwa unamfuata Mungu na kuhisi kwamba huna ufahamu wowote Wake, unawezaje kutatua utupu huu katika moyo wako? Hali hii inaweza kusuluhishwa kwa chakula? Au wakati unapomfuata Mungu na huelewi mapenzi Yake, ni nini unachoweza kutumia ili kufidia ile njaa katika moyo wako? Katika mchakato wa uzoefu wako wa wokovu kupitia kwa Mungu, wakati ukifuatilia mabadiliko katika tabia yako, kama huelewi mapenzi Yake au hujui ukweli ni nini, kama huelewi tabia ya Mungu, huhisi wasiwasi sana? Huhisi njaa na kiu kuu katika moyo wako? Je, hizi hisia hazikuzuii dhidi ya kuhisi amani katika moyo wako? Hivyo basi unaweza kufidia vipi njaa hiyo katika moyo wako—kunayo njia ya kutatua suala hilo? Baadhi ya watu huenda kufanya ununuzi, baadhi hupata rafiki wa kuwaambia yaliyo moyoni, baadhi hulala mpaka watosheke, wengine husoma zaidi maneno ya Mungu, au wakatia bidii zaidi na kutumia jitihada nyingi zaidi kukamilisha wajibu wao. Je, mambo haya yanaweza kutatua ugumu wako halisi? Nyinyi nyote mnaelewa kikamilifu aina hizi za mazoea. Unapohisi kuwa huna nguvu, unapohisi tamanio kubwa la kupata nuru kutoka kwa Mungu ili kukuruhusu kujua uhalisia wa ukweli na mapenzi Yake, ni nini unachohitaji kingi zaidi? Kile unachohitaji si mlo kamili, na wala si maneno machache mema. Na zaidi ya hayo, si lile tulizo na kutosheka kwa muda kwa mwili—kile unachohitaji ni Mungu kuweza kukueleza kwa njia ya moja kwa moja, wazi kile unachofaa kufanya na namna unavyofaa kukifanya, kuweza kukuonyesha wazi ukweli ni nini. Baada ya kuelewa haya, hata kama ni sehemu ndogo tu, huhisi kuwa umetosheka zaidi katika moyo wako kuliko vile ambavyo ungekuwa umekula mlo mzuri? Wakati moyo wako umetosheka, huo moyo wako, nafsi yako nzima, hayapati amani ya kweli? Kutokana na mfano huu na uchambuzi, unaelewa sasa ni kwa nini Nilitaka kusemezana na nyinyi kuhusu sentensi hii, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana hata wa siku ya sabato”? Maana yake ni kwamba kile kinachotoka kwa Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na kila kitu Chake vyote ni vikuu zaidi kuliko kitu kingine chochote, kikiwemo kile kitu au yule mtu ambaye uliwahi kusadiki kuwa unamthamini zaidi. Hivyo ni kusema, kama mtu hawezi kupata maneno kutoka katika kinywa cha Mungu au kama haelewi mapenzi Yake, hawezi kupata amani. Katika yale utakayopitia katika siku zako za usoni, utaelewa ni kwa nini Nilitaka wewe kuuona dondoo hii leo—hii ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na maisha. Ukweli kwa mwanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako wewe hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea amani moyoni mwako.
Je, ufahamu wako wa ukweli umefungamana na hali yako ya kibinafsi? Katika maisha halisi, lazima kwanza ufikirie ukweli upi unahusiana na watu, vitu, na vifaa ambavyo umekumbana navyo; ni miongoni mwa ukweli huu ndimo unaweza kupata mapenzi ya Mungu na kuunganisha kile ulichokumbana nacho na mapenzi Yake. Kama hujui ni vipengele vipi vya ukweli vinavyohusiana na mambo uliyokumbana nayo lakini unaenda kwa njia ya moja kwa moja kutafuta mapenzi ya Mungu, mtazamo huu hauna mwelekeo kwa kiasi fulani na hauwezi kufanikisha matokeo. Kama unataka kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu, kwanza unahitaji kuangalia ni mambo ya aina gani ambayo umekumbana nayo, ni vipengele vipi vya ukweli ambavyo mambo hayo yanauhusiano navyo, na kisha uutafute ukweli katika neno la Mungu ambalo linahusiana na kile ulichopitia. Kisha utafute njia ya matendo sahihi kwako katika ukweli huo; kwa njia hii unaweza kupata ufahamu usio wa moja kwa moja kuhusu mapenzi ya Mungu. Kutafuta na kutenda ukweli si kutumia kanuni au kufuata fomyula bila kufikiria. Ukweli si kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni maisha, ni kitu kilicho na uhai, na ni kanuni ambayo lazima kiumbe kifuate katika miaka yake hapa duniani na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima uelewe zaidi kutoka kwa uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeelezewa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vyenyewe ni ukweli; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kukionyesha waziwazi; inakuonyesha kwa njia ya moja kwa moja kile Mungu Anapenda, kile Hapendi, kile Anachotaka wewe kufanya na kile Hakuruhusu wewe kufanya, ni watu gani Anadharau na ni watu gani Anafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake. Bali na kujua kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na kuelewa tabia Yake kutoka katika neno Lake, kile kilicho muhimu zaidi ni haja ya kufikia ufahamu huu kupitia kwa uzoefu wa kimatendo. Kama mtu atajiondoa katika maisha halisi ili kumjua Mungu, hataweza kutimiza hayo. Hata kama kuna watu wanaoweza kupata ufahamu fulani kutoka katika neno la Mungu, ufahamu huo umewekewa mipaka ya nadharia na maneno, na kuna tofauti na vile ambavyo Mungu alivyo kwa kweli.
Kile tunachozungumzia sasa kimo ndani ya ule upana wa hadithi zilizorekodiwa katika Biblia. Kupitia katika hadithi hizi, na kupitia uchambuzi wa mambo haya yaliyofanyika, watu wanaweza kuelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo Ameonyesha, na kuwaruhusu kujua kila kipengele cha Mungu kwa upana zaidi, kwa kina zaidi, kikamilifu, na kwa undani zaidi. Hivyo basi, njia pekee ya kujua kila kipengele cha Mungu ni kupitia hadithi hizi? La, sivyo! Kwani kile Mungu anachosema na kazi Anayofanya katika Enzi ya Ufalme kinaweza kusaidia watu kwa njia bora zaidi kujua tabia Yake, na kuijua kikamilifu. Hata hivyo, Nafikiri ni rahisi zaidi kujua tabia ya Mungu na kuelewa kile Alicho nacho na kile Alicho kupitia baadhi ya mifano au hadithi zilizorekodiwa katika Biblia ambazo watu wamezoeana nazo.Nikichukua maneno ya hukumu na kuadibu na ukweli ambao Mungu anaonyesha leo ili kukufanya wewe kumjua Yeye neno kwa neno, utahisi kwamba haipendezi inachosha mno, na baadhi ya watu hata watahisi kwamba maneno ya Mungu yanaonekana kuwa yanafuata fomyula fulani. Lakini tukichukulia hadithi hizi za Biblia kama mifano ya kuwasaidia watu kujua tabia ya Mungu, basi haitaonekana kuwa ya kuchosha. Unaweza kusema kwamba katika mkondo wa kuonyesha mifano hii, maelezo ya kile kilichokuwa moyoni mwa Mungu wakati huo—hali Yake ya moyo au hisia Zake za moyoni, au fikira na mawazo Yake—vimesimuliwa kwa watu katika lugha za kibinadamu, na shabaha ya haya yote ni kuwaruhusu kushukuru, kuhisi kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho na kujua kwamba si fomula. Si hadithi ya kale, au kitu ambacho watu hawawezi kuona wala kugusa. Ni kitu ambacho kwa kweli kipo ambacho watu wanaweza kuhisi, na kufahamu. Hii ndiyo shabaha kuu. Unaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika enzi hii wamebarikiwa. Wanaweza kuzitumia hadithi za Biblia kupata ufahamu mpana zaidi wa kazi za awali za Mungu; wanaweza kuiona tabia Yake kupitia katika kazi ambayo Yeye amefanya. Na wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu kupitia kwa tabia hizi ambazo Ameonyesha, kuelewa maonyesho yale thabiti ya utakatifu Wake na utunzaji Wake kwa binadamu ili kuweza kufikia maelezo zaidi na maarifa ya kina zaidi kuhusu tabia ya Mungu. Ninasadiki kwamba nyinyi nyote mnaweza kuhisi haya yote!
Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho. Kilielezewa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake. Ndani ya Mwana wa Adamu, watu waliweza kuona namna ambavyo Mungu katika mwili alivyoishi kwa kudhihirisha ubinadamu Wake, na wakaona uungu wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kwa mwili. Aina hizi mbili za maelezo ziliwaruhusu watu kuweza kumwona Mungu aliye halisi sana, na kuwaruhusu kuwa na dhana tofauti ya Mungu. Hata hivyo, katika kipindi cha muda kati ya uumbaji wa ulimwengu na mwisho wa Enzi ya Sheria, yani, kabla ya Enzi ya Neema, kile kilichoonekana, kilichosikizwa, na kupitiwa na watu kilikuwa tu kipengele takatifu cha Mungu. Kilikuwa kile ambacho Mungu alifanya na kusema katika himaya ile isiyoshikika, na mambo ambayo Aliyaonyesha kutoka katika nafsi Yake halisi ambayo yasingeweza kuonekana au kuguswa. Mara nyingi, mambo haya yaliwafanya watu kuhisi kwamba Mungu alikuwa mkubwa sana, na kwamba wasingeweza kusonga karibu na Yeye. Picha ambayo Mungu kwa kawaida aliwapa watu ilikuwa kwamba Alionekana akipotea, na watu walihisi hata kwamba kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake yalikuwa yenye mafumbo mno na yasiyoeleweka mno kiasi kwamba hakukuwa na njia ya kuyafikia, isitoshe hata kujaribu kuelewa na kuyashukuru. Kwa watu, kila kitu kuhusu Mungu kilikuwa cha mbali—mbali mno kiasi kwamba watu wasingeweza kukiona, wasingeweza kukigusa. Ilionekana Alikuwa juu katika mbingu, na ilionekana kwamba Hakukuwepo kamwe. Hivyo basi kwa watu, kuelewa moyo na akili ya Mungu au kufikiria kwake kokote kusingeweza kutimizika, na hata kufikika. Ingawa Mungu alitenda kazi fulani thabiti katika Enzi ya Sheria, na Akaweza kutoa pia maneno fulani na kuonyesha tabia fulani mahususi ili kuwaruhusu watu kushukuru na kuona maarifa halisi fulani kuhusu Yeye, ilhali hatimaye, hilo lilikuwa ni maelezo ya Mungu kuhusu Alicho nacho na kile Alicho katika himaya isiyoshikika, na kile watu walielewa, kile wAlichojua kilikuwa bado kile cha kipengele takatifu kuhusu kile Alicho nacho na kile Alicho. Mwanadamu asingeweza kupata dhana thabiti kutoka kwa ya[a] kile Alicho nacho na na kile Alicho, na ile picha waliyokuwa nayo kuhusu Mungu ilikuwa bado ndani ya mawanda ya “Roho iliyo ngumu kukaribia, inayoonekana na kupotea.” Kwa sababu Mungu hakutumia kifaa mahususi au taswira katika himaya ya kimwili kuonekanakwa watu, bado wasingeweza kumfafanua Yeye kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Katika mioyo na akili za watu, siku zote walitaka kutumia lugha yao binafsi ili kuanzisha kiwango kwa ajili ya Mungu, kumfanya Yeye wa kugusikaka na kumfanya Yeye kuwa binadamu, kama vile Alikuwa mrefu kiasi gani, Alikuwa mkubwa kiasi gani, Alifanana vipi, Anapenda nini hasa na hulka Yake mahususi ni gani. Kwa kweli, moyoni Mwake Mungu alijua kwamba watu walifikiria hivyo. Alikuwa wazi sana kuhusu mahitaji ya watu, na bila shaka Alijua pia kile Alichofaa kufanya, hivyo basi Alitenda kazi Yake kwa njia tofauti na Enzi ya Neema. Njia hii ilikuwa takatifu na vilevile iliyostaarabishwa. Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kukaribia Yeye. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kung'amua mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliweza pia kufichua kwa watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika himaya ya kiroho. Kile watu wAlichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hali hii iliweza kuwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa wanadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika himaya ya kiroho, kila kitu kumhusu Yeye kiliwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi huongea kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na mwanadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.
Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni