Jumatatu, 19 Machi 2018

"Vunja Pingu na Ukimbie" (1) - Legeza Pingu na Ujifunze Njia ya Kweli


Utambulisho

    Mzee wa kanisa Li, kutokana na imani pofu katika maneno ya wachungaji wa kidini, alihisi kwamba kazi na maneno yote ya Mungu yaliandikwa katika Biblia na kwamba chochote nje ya Biblia hakingeweza kuwa kazi na neno la Mungu. Li alifikiri kwamba yote aliyohitaji kufanya ni kushika Biblia na wakati Bwana angekuja tena, angenyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo, Li hakuipa fikira kazi ya Mwenyezi Mungukatika siku za mwisho. Wakati mmoja, Mzee Li alipata kujua kwamba mfanyakazi mwenza, Mzee Lin, alikuwa akichunguza Umeme wa Mashariki kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kupitia kufanya ushirika na Mzee Lin, Mzee Li alikuja kuelewa ukweli wa kusikitisha kwamba alikuwa amenaswa na kufungwa na wachungaji wa kidini. Mwishowe, Mzee Li aliweza kulegeza pingu hizi na kuwaongoza wafanyakazi wenza wengine wote kutafuta na kuuchunguza Umeme wa Mashariki pamoja.
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Biblia,
Vunja Pingu na Ukimbie" (1) 
    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni