Jumatatu, 23 Aprili 2018

Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kumjua Mungu,
Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake

Kutomcha Mungu na Kutojiepusha na Maovu ni Kumpinga Mungu


Mwenyezi Mungu alisema, Hebu tuanze kwa kuangazia ni wapi ambapo msemo huu “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu” ulitokea. (Kitabu cha Ayubu.) Sasa kwa vile umetaja Ayubu, hebu tumzungumzie. Katika nyakati za Ayubu, Mungu alikuwa Akifanya kazi kwa ajili ya ushindi na wokovu wa binadamu? Alikuwa hafanyi hivyo, kweli? Na kuhusiana na Ayubu, ni maarifa kiwango gani aliyokuwa nayo kumhusu Mungu wakati huo? (Si maarifa mengi.) Na maarifa hayo ya Mungu yanalingana vipi na maarifa uliyo nayo sasa? Inakuwaje kwamba huthubutu kujibu hili? Maarifa ya Ayubu yalikuwa mengi zaidi au machache kuliko maarifa uliyo nayo sasa? (Machache.) Hili ni swali rahisi sana kujibu. Machache! Hili ni la hakika! Sasa hivi unaangaliana uso kwa uso na Mungu, uso kwa uso na neno la Mungu. Maarifa yako ya Mungu ni mengi zaidi kuliko yale ya Ayubu. Kwa nini Naleta suala hili? Kwa nini Ninaongea hivi? Ningependa kukuelezea hoja moja, lakini kabla Sijafanya hivyo, Nataka kukuuliza swali: Ayubu alijua machache sana kumhusu Mungu, ilhali angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo basi kwa nini watu siku hizi wanashindwa kufanya hivyo? (Upotovu mkubwa.) “Upotovu mkubwa”—huo ni ujuu juu wa swali, lakini Sitawahi kulitazama hivyo. Mara nyingi mnachukua mafundisho na barua ambazo mnazungumzia mara kwa mara, kama vile "upotovu mkuu," “kuasi dhidi ya Mungu,” “kutotii Mungu,” “kutotii,” “kutopenda ukweli” na mnatumia vidahizo hivi kuelezea kiini cha kila swali. Hii ni njia yenye hitilafu ya kutenda. Kutumia jibu sawa kueleza maswali yaliyo na asili tofauti bila shaka huibua shaka ya kuukufuru ukweli na Mungu. Sipendi kusikia jibu la aina hii. Hebu fikiria kulihusu! Hakuna yeyote kati yenu amefikiria kuhusu suala hili, lakini kila siku Mimi Ninaliona, na kila siku Mimi Ninalihisi. Hivyo basi, wewe unafanya, na Mimi Ninatazama. Wakati unapolifanya, huwezi kuhisi kiini cha suala hili. Lakini wakati Ninapoliona, Ninaweza kuona kiini chake, na Ninaweza kuhisi kiini chake vilevile. Hivyo basi kiini hiki ni nini basi? Kwa nini watu siku hizi hawamchi Mungu na hawaepuki maovu? Majibu yenu yako mbali na kuweza kueleza kiini cha swali hili, na haziwezi kutatua kiini cha swali hili. Hiyo ni kwa sababu kuna chanzo hapa ambacho nyinyi hamna habari kukihusu. Chanzo hiki ni kipi? Ninajua mnataka kusikia kukihusu, hivyo basi Nitawambia kuhusu chanzo cha swali hili.
Hapo mwanzo kabisa wa kazi ya Mungu, Alimchukulia vipi binadamu? Mungu alimwokoa binadamu; Alimchukulia binadamu kama mmoja wa familia Yake, kama mlengwa wa kazi Yake, kama kile ambacho Alitaka kukishinda, kukiokoa, na kile ambacho Alitaka kufanya kuwa kikamilifu. Huu ndio uliokuwa mwelekeo wa Mungu kwa binadamu mwanzoni mwa kazi Yake. Lakini mwelekeo wa binadamu kwa Mungu wakati huo ulikuwa upi? Mungu alikuwa haeleweki kwa binadamu, na binadamu alimchukulia Mungu kuwa mgeni. Inaweza kusemwa kwamba mwelekeo wa binadamu kwa Mungu ulikuwa si sahihi, na binadamu hakuwa na uwazi mzuri wa namna ya kumchukua Mungu. Hivyo basi Alimshugulikia alivyopenda yeye, na akafanya kile alichopenda yeye. Je, binadamu alikuwa na mtazamo kumhusu Mungu? Hapo mwanzoni, binadamu hakuwa na mtazamo wowote kumhusu Mungu. Mtazamo wa binadamu kama ulivyojulikana, ulikuwa tu dhana fulani na fikira kumhusu Mungu. Kile ambacho kilipatana na dhana za watu kilikubalika; kile ambacho hakikupatana kilitiiwa juujuu, lakini katika mioyo yao watu waligongana pakubwa nacho na wakakipinga. Huu ndio uliokuwa uhusiano wa binadamu na Mungu hapo mwanzoni: Mungu alimwona binadamu kama mwanachama wa familia, ilhali binadamu alimchukulia Mungu kama mgeni. Lakini baada ya kipindi cha kazi ya Mungu, binadamu alielewa hatimaye kile ambacho Mungu alikuwa Akijaribu kutimiza. Watu hatimaye walijua kwamba Mungu ndiye aliyekuwa Mungu wa kweli, na hatimaye wakajua kile ambacho binadamu angepokea kutoka kwa Mungu. Binadamu alimchukulia Mungu wakati huu kuwa nini?
Binadamu alimchukulia Mungu kuwa tegemeo kuu, akitumai kupokea neema, kupokea baraka, kupokea ahadi. Naye Mungu alimchukulia binadamu wakati huu kuwa nini? Mungu alimchukulia binadamu kuwa mlengwa wa ushindi Wake. Mungu alitaka kuyatumia maneno ili kumhukumu binadamu, kumjaribu binadamu, kumpa majaribio binadamu. Lakini kwa wanadamu wakati huu hasa, Mungu alikuwa kifaa ambacho angetumia kutimiza shabaha zake binafsi. Watu waliona kwamba ukweli uliotolewa na Mungu ungeweza kuwashinda na kuwaokoa, na kwamba walikuwa na fursa ya kupokea vitu walivoyvitaka kutoka kwa Mungu, hatima ambayo walikuwa wakitaka. Kwa sababu ya haya, chembe ndogo ya uaminifu kajitunga katika mioyo yao, na walikuwa radhi kumfuata Mungu huyu. Muda ukapita, na watu wakawa na maarifa fulani ya juujuu na ya mafundisho kumhusu Mungu. Inaweza kusemekana kwamba walikuwa wameanza “kuzoeana” zaidi na zaidi na Mungu. Na neno lililonenwa na Mungu, mahubiri Yake, ukweli Aliokuwa ameutoa awali, na kazi Yake—watu walikuwa “wamezoea” zaidi na zaidi. Hivyo basi, watu walidhani kimakosa kwamba Mungu hakuwa tena mgeni, na kwamba tayari walikuwa wakitembea njia ya uwiano na Mungu. Tangu hapo mpaka sasa, watu wamesikiliza mahubiri mengi juu ya ukweli, na wamepitia kazi nyingi ya Mungu. Lakini bado katika uingiliaji kati na uzuiaji wa mambo mengi tofauti na hali, watu wengi hawawezi kufikia hali ya kutia ukweli katika matendo, na hawawezi kufikia hali ya kumridhisha Mungu. Watu wanazidi kuwa goigoi, wanazidi kupungukiwa katika imani. Wanazidi kuhisi ni kana kwamba matokeo yao binafsi hayajulikani. Hawathubutu kuwa na mawazo yoyote ya kupita kiasi, na hawatafuti kupiga hatua yoyote ya maendeleo; wanafuata tu shingo upande, wakienda mbele hatua kwa hatua. Kuhusiana na hali ya sasa ya binadamu, mwelekeo wa Mungu kwa binadamu ni upi? Tamanio la Mungu la pekee ni kuukabidhi ukweli huu kwa binadamu, na kutia moyoni mwa binadamu njia Yake, na kupanga hali mbalimbali ili kumjaribu binadamu katika njia tofauti. Shabaha yake ni kuweza kuchukua maneno haya, ukweli huu, na kazi Yake, na kusababisha matokeo ambapo binadamu anaweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Watu wengi ambao Nimewaona wanalichukua tu neno la Mungu na kuliona kuwa mafundisho, kuliona kuwa barua, kuliona kuwa kanuni za kufuatwa. Wanapoendelea na shughuli zao na kuongea, au kukabiliwa na majaribio, hawachukulii njia ya Mungu kama njia ambayo wanafaa kuifuata. Hali hii hasa ni kweli wakati watu wanapokabiliwa na majaribio makuu; Sijamwona yeyote ambaye alikuwa anatia katika matendo kwa mwelekeo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu ya hili, mwelekeo wa Mungu kwa binadamu umejaa chuki na chukizo ya kupindukia. Baada ya Mungu kuwapa watu majaribio kadhaa, hata mamia ya wakati, bado hawana mwelekeo wazi wa kuonyesha bidii yao—ninataka kumcha Mungu na kujiepusha na maovu! Kwa sababu watu hawana bidii hii, na hawaonyeshi ishara kama hii, mwelekeo wa sasa wa Mungu kwao si kama ule wa hapo nyuma, Alipotoa rehema Yake, akatoa uvumilivu wake, akatoa ustahimilivu na subira Yake. Badala yake, Amesikitishwa mno na binadamu. Ni nani aliyesababisha masikitiko haya? Aina ya mwelekeo ambao Mungu anao kwa binadamu, unamtegemea nani? Unategemea kila mtu anayemfuata Mungu. Kwenye mkondo wa miaka Yake mingi ya kazi, Mungu ametaja mahitaji mengi kwa binadamu, na kupanga hali nyingi kwa binadamu. Lakini haijalishi ni vipi binadamu ametenda, na haijalishi ni mwelekeo upi ambao binadamu anao kwa Mungu, binadamu hawezi kutenda kwa njia wazi kulingana na shabaha ya kumcha Mungu na kujiepusha na uovu. Hivyo basi, Nitajumlisha yote haya kwa msemo mmoja, na kutumia msemo huu kueleza kila kitu ambacho tumeweza kuzungumzia kuhusiana na ni kwa nini watu hawawezi kutembea katika njia ya Mungu—mche Mungu na kujiepusha na maovu. Msemo huu ni upi? Msemo huu ni: Mungu humchukulia binadamu kama kifaa cha wokovu Wake, kifaa cha kazi Yake; binadamu humchukulia Mungu kama adui wake, kama tabaini yake. Je, unalielewa suala hili sasa? Kile ambacho ndicho mwelekeo wa binadamu; kile ambacho ndicho mwelekeo wa Mungu; kile ambacho ni uhusiano wa binadamu na Mungu—hivi vyote viko wazi sana sasa. Haijalishi ni kiwango kipi cha mahubiri ambayo mmeyasikiliza, yale mambo ambayo mmejijumuishia nyinyi wenyewe—kama vile kuwa mwaminifu kwa Mungu, kumtii Mungu, kutafuta njia ya kulingana na Mungu, kutaka kuishi daima dawamu kwa ajili ya Mungu, kuishi kwa ajili ya Mungu—kwangu Mimi mambo hayo hayajumuishi kutembea kwa njia ya Mungu kwa nadhari, ambako ni kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Badala yake, ni njia mbalimbali kupitia kwazo mnaweza kufikia shabaha fulani. Ili kutimiza shabaha hizi, mnaangalia shingo upande baadhi ya taratibu. Na ni taratibu hizi hasa ambazo huwapeleka watu mbali zaidi kutoka katika njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kumweka Mungu katika upinzani na binadamu kwa mara nyingine.
Swali tunalolizungumzia leo ni zito kidogo, lakini licha ya chochote, bado Natumai kwamba mtakapopitia yale yote yajayo, na kwenye nyakati zijazo, mnaweza kufanya kile ambacho Nimewaambia mfanye. Msimpuuze Mungu na kumchukulia Yeye kama hewa tupu, kuhisi kwamba Anakuwepo tu nyakati zile Anapokuwa Mwenye manufaa kwako, lakini wakati ule ambao humhitaji unahisi kwamba Yeye hayupo. Unapos hikilia uelewa huu katika bila ufahamu, tayari umemghadhabisha Mungu. Pengine kunao watu wanaosema: “Mimi simchukulii Mungu kama hewa tupu, mimi siku zote humwomba Mungu, siku zote mimi humridhisha Mungu, na kila kitu ninakichofanya huwa katika ule upana na kiwango na kanuni zinazohitajika na Mungu. Bila shaka siendelei kulingana na mawazo yangu binafsi.” Ndiyo, namna ambayo unafanya mambo ni sahihi. Lakini unafikiria vipi wakati unakumbana uso kwa uso na suala? Unatenda vipi unapokabiliwa na suala? Baadhi ya watu huhisi kwamba Mungu yupo wakati wanapomwomba Yeye, na Kumsihi kuwasikiliza. Lakini wakati wanapokabiliwa na suala, wanakuwa na fikira zao binafsi na wanataka kuzitii. Hapa Mungu huchukuliwa kama hewa tupu. Aina hii ya hali humfanya Mungu kutokuwepo. Watu hufikiria kwamba Mungu anafaa kuwepo wakati wanapomhitaji, na wakati hawamhitaji Mungu Hafai kuwepo. Watu hufikiria kwamba kufanya mambo kulingana na mawazo yao katika matendo ya maisha kunatosha. Wanasadiki kwamba wanaweza kufanya mambo vyovyote vile wapendavyo. Wanafikiria tu kwamba hawahitaji kutafuta njia ya Mungu. Watu ambao kwa sasa wamo katika hali ya aina hii, hali ya namna hii—huoni kwamba karibu wataingia hatarini? Baadhi ya watu husema: “Haijalishi kama karibu nitaingia hatarini au la, nimesadiki kwa miaka mingi sana, na ninasadiki kwamba Mungu hataniacha kwa sababu Asingeweza kustahimili kuniacha mimi.” Watu wengine husema: “Hata tangu nilipokuwa kwenye tumbo la mama yangu, nilimsadiki Bwana, tangu hapo mpaka sasa, jumla ya miaka arubaini au hamsini hivi. Kwa mujibu wa muda, mimi ndimi nimefuzu zaidi kuokolewa na Mungu; mimi ndimi nimefuzu zaidi kunusurika. Kwenye kipindi hiki cha muda cha miongo minne au mitano, niliiacha familia yangu na kazi yangu. Nilijitolea kila kitu nilichokuwa nacho kwa Mungu, kama pesa, ardhi, anasa na muda wa familia; sijala vyakula vingi vitamu; sijafurahia vitu vingi vya kusisimua; sijatembelea sehemu nyingi za kuvutia; nimeweza hata kupitia mateso ambayo hata watu wa kawaida wasingevumulia. Kama Mungu hawezi kuniokoa mimi kwa sababu ya haya yote, basi mimi nashughulikiwa kwa njia isiyo ya haki na siwezi kuamini kwa Mungu wa aina hii.” Je, kunao watu wengi walio na mtazamo wa aina hii? (Kunao wengi sana.) Basi leo Nitawasaidia kuelewa hoja moja: Kila mmoja wa hao anayeshikilia maoni ya aina hii anachukua hatua zitakazomdhuru mwenyewe. Hii ni kwa sababu wanatumia mawazo yao binafsi katika kuyafunika macho yao. Ni kufikiria kwao hasa, na hitimisho yao binafsi vinavyochukua nafasi ya kiwango cha kile Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu, ndivyo vinavyowashikilia dhidi ya kukubali nia za kweli za Mungu, na kuwafanya kutoweza kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu, na kuwafanya pia kupoteza fursa yao kufanywa kuwa watimilifu na Mungu na kutokuwa na sehemu au mgao katika ahadi ya Mungu.

kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Soma zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni