Jumamosi, 30 Juni 2018

Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

Kutatua Asili na Kutenda Ukweli

1. Uhusiano Kati ya Ubinadamu na Uwezo wa Kutenda Ukweli
Mwenyezi Mungu alisema, Watu husema kuwa kutenda ukweli ni vigumu kabisa. Basi mbona watu wengine wanaweza kutenda ukweli? Watu wengine husema ni kwa sababu kwa asili wanaipokea kazi ya Roho Mtakatifu ikifanya kazi juu yao, na pia kwa sababu ni wazuri kiasili. Hoja hii ina kiwango fulani cha mantiki. Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli; hii inamaanisha kuwa watakumbana na matatizo fulani. Je, mnaweza kusema kuwa yule ambaye hatendi ukweli amewahi kuutafuta ukweli? Hajautafuta kabisa! Fikira zake binafsi hutokea: “Njia hii ni nzuri, ni kwa faida yangu.” Mwishowe, bado anatenda kulingana na mawazo yake binafsi. Hatafuti ukweli kwa sababu kuna kitu kisicho sawa na moyo wake, moyo wake hauko sawa. Hatafuti, hachunguzi, wala haombi mbele za Mungu; anatenda tu kwa ukaidi kulingana na matakwa yake. Mtu wa aina hii hana upendo wa ukweli kabisa. Kusema kuwa hana upendo wowote kwa ukweli, lakini kuwa anafanya vitu fulani akichunga kanuni na hakiuki kanuni, kutokiuka kwa aina hiyo hakumaanishi kuwa anakusudia kumtafuta Mungu. Inaweza tu kusemwa kuwa ni jambo tukizi tu. Watu wengine hufanya mambo fulani kwa mtindo uliochanganyikiwa na ovyo ovyo bila kutafuta; wakijichunguza tu baada ya tendo. Wakigundua kuwa kufanya mambo ya aina hiyo sio sambamba na ukweli, watajizuia kufanya hivyo wakati ujao. Hili linaweza kuchukuliwa kama kuwa na kiwango fulani cha upendo kwa ukweli. Mtu wa aina hii anaweza kupitia kiwango cha mabadiliko. Wale wasio na upendo kwa ukweli hawatautafuta katika wakati huo, wala hawatajichunguza baadaye. Kamwe hawachunguzi kama tendo lilitekelezwa kwa sawa ama kwa makosa hatimaye, hivyo wanakiuka kanuni kila wakati, wanakiuka ukweli. Hata ukifanya kitu ambacho hakikiuki kanuni, hakilingani na ukweli, na hiki kitu kinachoitwa kutokiuka kanuni ni suala la mtazamo tu. Kwa hivyo mtu wa aina hii yuko katika hali gani anapotenda kulingana na matakwa yake mwenyewe? Hatendi kwa hali ya kutunduwaza na upumbavu: Je, hili linapatana na ukweli katika uchambuzi wa mwisho? Hii siyo hali ambayo wanajipata kwayo, badala yake wanasisitiza kwa ukaidi kutenda kwa namna hiyo; wamefanya uamuzi kutenda kwa njia hiyo, bila nia yoyote kabisa ya kuutafuta ukweli. Ikiwa kwa kweli wanatafuta nia ya Mungu, ilhali wakose kuelewa nia ya Mungu kabla, basi wanaweza kuzingatia njia ifuatayo ya utendaji: Kwanza nitaenda mbele na kuifanya kwa njia hii, ikikubaliana na ukweli basi nitaendelea kufanya kwa njia hii, kama haikubaliani na ukweli, nitaharakisha kurekebisha hii na kutotenda kwa namna hiyo tena. Kama wanaweza kuutafuta ukweli kwa namna hii, wataweza kubadilika baadaye. Bila nia hii, hawataweza kubadilika. Mtu aliye na moyo anaweza kufanya makosa mara moja tu anapofuata utendaji, mara mbili kwa kiwango cha juu zaidi—mara moja ama mbili, sio mara tatu ama nne, hii ni akili ya kawaida. Kama anaweza kutenda makosa hayo sawa mara tatu ama nne, hii inathibitisha kuwa hana upendo wa ukweli, wala hautafuti ukweli. Mtu wa aina hii kwa waziwazi sio mtu mwenye utu. Kama baada ya mara moja ama mbili bila hisia katika moyo wake, hakuna msisimko wa dhamiri yake, anaweza kutenda kitendo hicho hicho mara tatu ama nne, mtu wa aina hii hana uwezo wa kubadilika kabisa, ni mtu wa aina hii tu—hawezi kukombolewa kabisa. Kama baada ya kutenda mara moja, anahisi kuwa kuna jambo lisilo sawa na suala hilo, ajichukie sana kwa tendo hilo na kuhisi mwenye hatia moyoni mwake, katika hali hii, atatenda kwa njia hiyo kwa kiwango cha chini zaidi wakati ujao na hatua kwa hatua hali hii haitatokea baadaye. Hata akitaka moyoni mwake, hatalitenda. Hiki ni kipengele kimoja cha mabadiliko. Pengine utasema: “Siwezi kubadilisha hali hii.” Huwezi kubadilika? Hiyo ni kwa sababu hutaki kubadilika. Kama uko tayari kutenda ukweli, je, huwezi kubadilika? Watu wanaosema hivi wanakosa hiari. Wote ni wanyonge wa kudharauliwa. Hawako tayari kuvumilia mateso. Hawataki kutenda ukweli; badala yake wanasema kuwa ukweli hauwezi kuwabadilisha. Je, mtu wa aina hii si mdanganyifu sana? Ni wao ndio hawawezi kutenda ukweli, ubinadamu wao una dosari, ilhali hawajui asili yao wenyewe kamwe. Badala yake wana shaka kama kazi ya Mungu inaweza kumfanya mwanadamu awe kamili katika kila hatua ama hapana. Nasema kuwa mtu wa aina hii huwa hana nia kamwe ya kuutoa moyo wake kwa Mungu, huwa hana mpango kamwe wa kuvumilia shida. Sababu pekee ya wao kukaa hapa ni kwa nafasi ya nadra tu kuwa wanaweza kupata bahati nzuri baadaye. Tunamwita mtu wa aina hii asiye na ubinadamu. Kama ni mtu mwenye ubinadamu, hata wakati ambapo Roho Mtakatifu hatendi juu yake kwa nguvu, na wana ufahamu kidogo wa ukweli, je, anaweza kushiriki katika matendo mabaya? Mtu mwenye ubinadamu, bila kujali kama Roho Mtakatifu anatenda juu yake au la, hataweza kufanya matendo mabaya. Watu wengine wasio na ubinadamu wanaweza tu kufanya matendo fulani mazuri chini ya sharti kuwa Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Bila ya Roho Mtakatifu kutenda juu yao, asili yao inafunuliwa. Nani anaweza kuwa na Roho Mtakatifu Akitenda juu yao kila wakati? Wengine kati ya wasioamini wana ubinadamu mzuri, pia hawana Roho Mtakatifu akitenda juu yao, ilhali hawashiriki katika matendo yoyote maovu. Kama unamwamini Mungu, unaweza vipi kushiriki katika matendo maovu? Hii inaonyesha tatizo la asili yako. Bila Roho Mtakatifu kutenda juu yao, asili ya watu inafunuliwa. Kukiwa na Roho Mtakatifu akifanya kazi kwao, Roho Mtakatifu atawasihi sana, Akiwapatia watu nuru na mwangaza, Akiwapa nguvu tele, kwa hivyo watu wanapofanya vitendo vizuri, sio swali la asili yao nzuri. Hivyo, watu wengi wanatenda matendo mabaya wakati wa utendaji wao, na kwa wakati kama huo, wanafichua asili yao.
2. Kuweka Kanuni Kadhaa za Kutatua Asili Yako
Unatatua asili yako vipi? Kwanza, lazima uijue asili yako na lazima pia uelewe neno na mapenzi ya Mungu. Utahakikisha vipi basi, kwa kiwango kikubwa zaidi, kuwa utaepuka kutenda matendo mabaya, ukifanya tu yale ambayo yanalingana na ukweli? Kama uko tayari kufanya badiliko, basi lazima utafakari hili kwa uanglifu. Kwa kauli ya asili yako yenye dosari, aina gani za ufisadi inayoihusisha na namna gani za matendo inaweza kutenda, mtazamo upi basi unaweza kuchukuliwa na ni jinsi gani inaweza kuwekwa katika matendo ili kuidhibiti—hili ndilo swali muhimu. Lazima uchunguze swali hili kwa makini, hata zaidi katika wakati wa giza (sio pamoja na baada tu ya kupokea ushirika kutoka juu, lakini ukiondoa hili, hivyo ni, baada ya zaidi ya siku kumi kupita), kuhusu jinsi unavyoweza kutatua suala hili, jinsi unavyoweza kutimiza wajibu wako vizuri, jinsi unavyoweza kuchukua njia sawa; lazima ujiwekee kanuni. Hili linategemea hiari ya mtu na iwapo anamtaka Mungu au la. Lin Zexu alikuwa mwepesi wa hasira. Kulingana na udhaifu wake mwenyewe aliandika chini wito ufuatao: “Idhibiti hasira yako.” Huu ni mtazamo wa mwanadamu, hata hivyo unafanya kazi kwa kweli. Kila mtu ana kanuni zake za kufuata, kwa hivyo lazima pia wewe uweke kanuni kulingana na asili yako mwenyewe. Kanuni hizi ni muhimu, kuwa bila kanuni hizi hakukubaliki. Huu pia unafaa kuwa wito wako wa kumwamini Mungu na mfumo wako wa matendo.
Kutatua asili ya mtu kunaanza na kuutelekeza mwili. Kuutelekeza mwili pia kunahitaji kanuni. Je, mtu anaweza kuutelekeza mwili kwa mtindo wa kipumbavu? Wakati utakapofika utakubali matakwa ya mwili. Ndugu wengine wanaweza kushikwa na bumbuazi wanapomwona mwanamke mrembo. Basi lazima ujiwekee wito mwenyewe. Unaweza kufanya nini mwanamke mrembo anapotokea? Unafaa kuondoka ama unafaa kufanya nini? Unafaa kufanya nini akiushika mkono wako? Kama huna kanuni, utajikwaa unapokumbana na hali ya aina hiyo. Kama unahisi mwenye tamaa unapoona pesa au mali, unaweza kushughulikia hili vipi? Lisome swali hili hasa, fanya mazoezi ya kulitatua kwa makini na polepole utaweza kuuacha mwili. Kuna kanuni ambayo ni muhimu sana, ambayo ni kufikiria mara mbili kabla ya kutenda; ichunguze mbele ya Mungu. Zaidi ya hayo, kila jioni lazima uzichunguze hali zako mwenyewe. Hii ni kanuni moja. Chunguza tabia yako mwenyewe: matendo gani yalifanywa kulingana na ukweli na matendo gani yalikiuka kanuni. Hoja hizi mbili ndizo za muhimu sana! Moja ni kujichunguza wakati wa tendo na nyingine ni kujichunguza baada ya tendo. Kanuni ya tatu ni: Kuwa wazi kabisa na nini maana ya kuuweka ukweli katika matendo na kinachomaanishwa na kusema kushughulikia mambo kwa namna ya kufuata kanuni. Unapokuwa wazi kabisa kuhusu hili, utashughulikia mambo kwa usahihi. Kwa kufuata kanuni hizi tatu, basi utaweza kujizuia. Asili yako ya kwanza haitaweza kujifichua, haitaweza kujitokeza. Hii pia ni kanuni ya msingi ya kushughulikia asili ya binadamu. Kwa kushikilia kanuni hizi imara, hata wakati Roho Mtakatifu hafanyi kazi juu yako, na baada ya wakati mrefu bila ushirika kutoka juu, kwa kugharimika juhudi inayotosha kufikia juu bado unaweza kujidumisha katika hali ya ukawaida, basi wewe ni mtu unayehifadhi ukweli kwa upendo mkubwa, mtu anayeutelekeza mwili. Wale ambao kila wakati wanategemea aliye juu kuwashughulikia ama kuwapogoa na kuwasiliana ukweli ni watumwa, hawawezi kamwe kuachiliwa ama kukua. Mtu anayefanya mambo bila kanuni, baada ya kipindi cha muda bila yeyote wa kumshughulikia ama kumpogoa, bila mtu wa kushiriki naye, atatenda kwa namna ya kutaka, kupoteza udhibiti wake mwenyewe na kuwa mwenye wazimu. Je, mtu kama huyu anaweza kumweka Mungu katika utulivu? Kwa hivyo, ili kutatua tatizo la asili ya mtu, mtu lazima azingatie kanuni hizi tatu. Kwa njia hii, utaweza kuchunga dhidi ya kufanya makosa makubwa.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni