Jumatatu, 27 Agosti 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | swahili worship songs | Njia Yote Pamoja na Wewe

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu,


  • Njia Yote Pamoja na Wewe
  • I
  • Nilikuwa kama mashua,
  • ikielea baharini.
  • Ulinichagua,
  • na mahali pazuri Uliniongoza.
  • Sasa katika familia Yako,
  • nikipewa joto na upendo Wako,
  • nina amani kabisa.
  • Unanibariki,
  • Unatoa maneno Yako ya hukumu.
  • Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako.
  • Kila mara nikiasi,
  • kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako.
  • Na bado Hunitendei kulingana na dhambi zangu
  • lakini Unafanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu.
  • Ninapokuwa mbali,
  • Unaniita nirudi kutoka hatarini.
  • Ninapoasi, Unauficha uso Wako,
  • giza likinifunika.
  • Ninaporudi Kwako,
  • Unaonyesha neema,
  • Unatabasamu ili kukumbatia.
  • Shetani anaponipiga,
  • Unatibu vidonda vyangu,
  • Unaupa joto moyo wangu.
  • Shetani anaponiumiza,
  • Uko nami kuanzia mwanzo hadi mwisho wa majaribu.
  • Alfajiri itafika karibuni,
  • na anga itang’aa samawati kama awali,
  • wakati Uko nami.
  • Alfajiri itafika karibuni,
  • anga itang’aa samawati kama awali,
  • wakati Uko nami.
  • II
  • Wewe ni uhai wangu,
  • Wewe ni Bwana wangu.
  • Mwenzi wa kila siku,
  • kivuli cha karibu kando yangu.
  • Ukinifunza jinsi ya kuwa binadamu
  • na kunipa ukweli na uhai.
  • Pamoja na Wewe maisha yangu
  • yanasonga mbele kwa utukufu.
  • Bila chaguo langu,
  • natii amri Yako.
  • Kuwa kiumbe wa kweli,
  • narudi upande Wako.
  • Kuishi katika uwepo Wako,
  • nazungumza na Wewe na kusikia sauti Yako.
  • Hutangoja tena katika umbali mpweke.
  • Pamoja na Wewe,
  • hakuna kuogopa dhoruba.
  • Usiku unaponifunika,
  • siko pekee yangu tena.
  • Pamoja na Wewe kando yangu,
  • hatari au matatizo, naweza kuvikabili.
  • Pamoja na Wewe,
  • safari hazitakuwa ngumu sana.
  • Njia zenye mabonde
  • zinapita katika matatizo,
  • zinafungua njia kwenda kwa chemichemi ya kupendeza.
  • Alfajiri itafika karibuni,
  • anga itang’aa samawati kama awali,
  • wakati Uko nami.
  • Pamoja na Wewe,
  • hakuna kuogopa dhoruba tena.
  • Usiku unaponifunika,
  • siko pekee yangu tena.
  • Pamoja na Wewe kando yangu,
  • hatari na matatizo, naweza kuvikumba.
  • Pamoja na Wewe,
  • safari haziwezi kuwa ngumu sana.
  • Njia zenye mabonde
  • zinapita katika matatizo,
  • zinafungua njia kwenda kwa chemichemi ya kupendeza.
  • Alfajiri itafika karibuni,
  • anga itang’aa samawati kama awali.
  • Niko pamoja na Wewe.
  •  
  • kutoka kwa Mfuate Mwanakondoo na Uimbe Nyimbo Mpya

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni