Alhamisi, 22 Novemba 2018

nyimbo za kusifu na kuabudu | 76. Ni Mungu tu Ana Njia ya Uzima

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

nyimbo za kusifu na kuabudu | 76. Ni Mungu tu Ana Njia ya Uzima

I
Njia ya uzima si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuwa nacho;
si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kuipata kwa urahisi.
Kwani uzima unatoka tu kwa Mungu,
ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima,
ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima.
Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima,
na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele.
Tangu uumbaji wa dunia, Mungu amefanya kazi nyingi
ambazo zinahusisha umuhimu wa maisha, zinazoletea mwanadamu uzima;
Amelipa gharama kubwa ili mwanadamu apate uzima.
Kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele;
Yeye ndiye njia ambayo kwayo mwanadamu hupata ufufuo.
II
Mungu hajakosa kamwe kuwa katika moyo wa mwanadamu,
Kila wakati Anaishi kati ya mwanadamu.
Yeye ni nguvu inayoendesha kuishi kwao,
na msingi wa uwepo wao;
Yeye ni amana tajiri kwa mwanadamu kuishi kwa kumtegemea.
Anafanya mwanadamu kuzaliwa tena,
na kuwafanya waishi kwa nguvu katika majukumu yao tofauti.
ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima,
ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima.
Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima,
na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele.
Kwa sababu ya mamlaka Yake na nguvu Yake ya maisha isiokosa,
mwanadamu ameishi kizazi baada ya kizazi.
Mamlaka ya maisha ya Mungu yanamsaidia mwanadamu bila kukoma;
Mungu amelipa gharama ambayo hakuna mwanadamu wa kawaida amewahi kulipa.
III
Nguvu ya maisha ya Mungu inatawala juu ya mamlaka yote; na inazidi nguvu zote.
Maisha Yake ni ya milele, mamlaka Yake ni ya ajabu.
Hakuna kiumbe yeyote aliyeumbwa anayeweza kushinda nguvu ya maisha Yake,
ambayo ipo na inaangaza nuru inayong’aa
wakati wowote ama mahali, wakati wowote ama mahali.
ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima,
ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima.
Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima,
na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele.
Mbingu, dunia inaweza kubadilika sana, maisha ya Mungu hayabadiliki kamwe.
Vitu vyote vimeenda, lakini maisha ya Mungu bado ipo,
kwani Mungu ni chanzo na asili ya uwepo wa vitu vyote,
kwani Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele.
IV
Maisha ya Mungu yanatoka kwa Mungu, mbingu ipo kwa sababu ya Mungu,
na dunia ipo kwa sababu ya nguvu ya maisha ya Mungu.
Hakuna kitu kilicho na umuhimu kinachoweza kuvuka mipaka ya mamlaka ya Mungu,
na hakuna kitu kilicho na nguvu kinaweza kujiweka huru kutoka kwa mipaka ya mamlaka ya Mungu.
ni Mungu Mwenyewe pekee Aliye na kiini cha uzima,
ni Mungu pekee aliye na njia ya uzima.
Hivyo ni Mungu pekee ndiye chanzo cha uzima,
na kisima cha maji ya uzima kinachotiririka milele.
Katika njia hii, haijalishi wao ni nani,
wanadamu wote lazima watii, lazima watii utawala wa Mungu,
aishi chini ya amri Yake.
Hakuna anayeweza kuepuka, hakuna anayeweza kuepuka, kuepuka kutoka kwa udhibiti Wake.
kutoka kwa "Ni Kristo Wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Sikiliza nyimbo: Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni