Alhamisi, 15 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utangulizi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Utangulizi

Mnamo Februari 11, mwaka wa 1991, Mungu alitoa tamko Lake la kwanza katika kanisa ambalo lilikuwa na athari isiyo ya kawaida kwa kila mmoja wa watu walioishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu wakati huo. Tamko hili lilitaja yafuatayo: “Makazi ya Mungu yameonekana” na “Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa.” Kwa maneno haya ya maana sana, watu hawa wote waliletwa katika ulimwengu mpya. Wale wote waliosoma tamko hili walihisi maelezo ya kazi mpya, kazi kuu ambayo Mungu alikuwa karibu kuanzisha. Lilikuwa ni tamko hili zuri, laini, na lenye habari nyingi katika maelezo machache lililoleta binadamu wote katika kazi mpya ya Mungu na katika enzi mpya, na ambalo liliweka msingi na kuanzisha kazi ya Mungu katika kupata mwili huku. Mtu anaweza kusema kwamba tamko ambalo Mungu alitoa wakati huu ni lile ambalo linaunganisha enzi; kwamba ni wakati wa kwanza tangu mwanzo wa Enzi ya Neema ambapo Mungu amezungumza wazi kwa jamii ya binadamu; zaidi, kwamba ni wakati wa kwanza Amezungumza baada ya kujificha kwa miaka elfu mbili; na, zaidi ya hayo, kwamba ni utangulizi, sehemu muhimu ya kuanzia, kwa kazi ambayo Mungu yuko karibu kufanya katika Enzi ya Ufalme.
Wakati wa kwanza Mungu alitoa tamko, Alifanya hivyo kwa jinsi ya sifa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu, kwa lugha ambayo wakati mmoja ilikuwa ya sanaa na ya ustaarabu na wazi na ya nyumbani, na vile vile ruzuku ya maisha ambayo ingeeleweka kwa urahisi na bila shida. Akiwa na hili, Alichukua kundi hili dogo la watu, waliojua tu jinsi ya kufurahia neema Yake wakingoja kurudi kwa Bwana Yesu kwa hamu, na kuwaleta kwa kimya katika hatua nyingine ya kazi katika mpango wa Mungu wa usimamizi. Katika hali hizi, binadamu hawakujua, sembuse kuthubutu kufikiri, ni aina gani ya kazi Mungu angefanya hatimaye, ama kilichokuwa njiani mbele. Baadaye, Mungu aliendelea kutoa matamko zaidi kuwaleta binadamu katika enzi mpya hatua kwa hatua. La kushangaza, kila tamko la Mungu ni tofauti katika maudhui na aidha hutumia aina tofauti za sifa na njia za maonyesho. Matamko haya, yaliyo sawa kwa sauti lakini ya namna mbalimbali katika maudhui, yamejazwa kila wakati na hisia za Mungu za utunzaji na kujali, na karibu kila moja lina ruzuku za maisha na maudhui tofauti na vile vile maneno ya kukumbusha, kushawishi, na kufariji kutoka kwa Mungu hadi kwa mwanadamu. Katika matamko haya, mafungu kama hili yanaonekana mara kwa mara: “Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote”; “Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu”; “Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake”; na mengineo. Ujumbe unapitishwa katika mafungu haya, ama mtu anaweza kusema kwamba mafungu haya yanapitisha ujumbe kwa jamii ya binadamu: Mungu tayari amekuja katika dunia ya binadamu, Mungu ataanzisha kazi kubwa hata zaidi, ufalme wa Mungu tayari umeshuka katika kundi fulani la watu, na Mungu tayari amepata utukufu na kushinda maadui Wake wengi. Kila tamko la Mungu linaushika moyo wa kila binadamu. Wanadamu wote wanamsubiri Mungu ayape sauti hata maneno mengi zaidi, kwa sababu kila wakati Mungu huzungumza, Anatikisa moyo wa binadamu hadi kwa kina chake, na zaidi Anaongoza na kuweka sawa kila mwendo na kila hisia ya mwanadamu, ili kwamba binadamu waanze kuyategemea na hata zaidi kuyaheshimu maneno ya Mungu…. Kwa njia hii, pasipo kujua, watu wengi sana walikuwa wameisahau Biblia kimsingi, na kuyasikiliza shingo upande mahubiri ya kale na maandishi ya watu wa kiroho, kwa sababu hawakuweza kupata katika maandishi ya zamani msingi wowote wa maneno haya ya Mungu, wala hawakuweza kugundua mahali popote makusudi ya Mungu katika kutoa matamko haya. Kwa sababu hiyo, ilimpasa kwa kiasi gani binadamu kukiri kwamba matamko haya ni sauti ya Mungu ambayo hayajaonwa wala kusikika tangu mwanzo wa wakati, kwamba yako mbali ya uwezo wa mtu yeyote anayemwamini Mungu, na kwamba yanapita matamko yote yaliyotolewa na mtu yeyote wa roho anayeishi katika enzi za zamani au na Mungu zamani. Wakihimizwa na kila moja ya matamko haya, binadamu waliingia bila kujua katika hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, kuingia katika maisha kwa safu ya mbele ya enzi mpya. Wakihimizwa na maneno ya Mungu, binadamu, wakiwa wamejawa na matarajio, walionja utamu wa kuongozwa binafsi na maneno ya Mungu. Naamini muda huu mfupi kuwa wakati ambapo kila binadamu ataangalia nyuma kwa kumbukumbu ya kuvumilia, wakati ambapo kwa kweli kile ambacho binadamu walifurahia wakati huu hakikuwa zaidi ya hali ya kuashiria wema wa kazi ya Roho Mtakatifu, au mtu anaweza kukiita ladha tamu ya kudanganya. Hii ni kwa sababu, kutoka hatua hii kuendelea, bado chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, bado katika hali ya kuashiria wema wa kazi mpya ya Roho Mtakatifu, binadamu waliongozwa katika awamu nyingine ya maneno ya Mungu pasipo kujua, ambayo ilikuwa hatua ya kwanza iliyohemshwa na tamko la Mungu katika Enzi ya Ufalme—jaribio la watendaji huduma.
Maneno yaliyotamkwa kabla ya jaribio la watendaji huduma yalikuwa hasa kwa jinsi ya maagizo, ushawishi, lawama, na kufundisha nidhamu, na katika sehemu nyingine yalitumia jinsi nzee ya utambulisho iliyotumiwa katika Enzi ya Neema—kutumia “Wanangu” kwa wale waliomfuata Mungu ili kufanya iwe rahisi kwa binadamu kumkaribia Mungu, au ili binadamu waweze kuchukulia uhusiano wao na Mungu kuwa wa karibu. Kwa njia hii, bila kujali hukumu ambayo Mungu alitoa kwa kujiona, majivuno na tabia nyingine potovu za binadamu, mwanadamu angeweza kushughulikia na kulikubali katika utambulisho wake wa “mwana,” bila kuwa na uhasama kwa matamko ya “Mungu Baba,” ambayo kwa kuongezea ahadi ambayo “Mungu Baba” alitoa kwa “wana” Wake haikuwa ya shaka kamwe. Katika kipindi hiki, binadamu wote walifurahia uwepo ulio huru kutokana na taabu kama wa mtoto mchanga, na hili lilitimiza makusudi ya Mungu, ambayo ni, walipoingia katika utu uzima, Angeanza kutekeleza hukumu kwao. Hili pia liliweka msingi wa kazi ya kuhukumu jamii ya binadamu ambayo Mungu anaanzisha rasmi katika Enzi ya Ufalme. Kwa sababu kazi ya Mungu katika kupata mwili huku hasa ni kuhukumu na kushinda jamii nzima ya binadamu, punde tu mwanadamu alipoweka miguu yake chini kwa uthabiti, Mungu aliingia katika mtindo wa kazi Yake mara moja—katika kazi ambamo kwayo Anamhukumu mwanadamu na kumwadibu. Kwa uwazi, matamko yote kabla ya jaribio la watendaji huduma yalitolewa kwa ajili ya kupitia mageuzi, lengo la kweli likiwa tofauti na lile lilioonekana kuwa. Nia ya hamu ya Mungu ilikuwa kwamba Aweze kuzindua rasmi kazi Yake katika Enzi ya Ufalme punde iwezekanavyo. Hakutaka kwa vyovyote vile kuendelea kumbembeleza binadamu mbele kwa kumpa maneno madogo madanganyifu; badala yake, Alikuwa na hamu kuona uso wa kweli wa kila mwanadamu kabla ya kiti Chake cha hukumu, na hata kwa hamu zaidi Alitaka kuona mtazamo wa kweli ambao binadamu wote wangekuwa nao kuelekea Kwake baada ya kupoteza neema Yake. Alitaka tu kuona matokeo, sio mchakato. Lakini wakati huo hakukuwa na mtu aliyeelewa nia ya Mungu yenye hamu, kwa sababu moyo wa binadamu ulishughulika tu na hatima yake na matarajio yake ya baadaye. Sio ajabu kwamba hukumu ya Mungu ilikuwa imeelekezwa, mara kwa mara, kwa jamii nzima ya binadamu. Ilikuwa tu wakati binadamu, chini ya mwongozo wa Mungu, walianza kuishi maisha ya kawaida ya binadamu ambapo mtazamo wa Mungu kwa binadamu ulibadilika.
Mwaka wa 1991 haukuwa wa kawaida: hebu tuuite mwaka huu “mwaka wa ustawi.” Mungu alianzisha kazi mpya ya Enzi ya Ufalme na kuelekeza matamko Yake kwa jamii yote ya binadamu. Wakati huo huo, binadamu walifurahia wema wa pekee na, hata zaidi, kupitia uchungu unaofuata hukumu ya Mungu ya pekee kwa mwanadamu. Jamii ya binadamu ilionja utamu usiojulikana mpaka sasa na kuhisi pia hukumu na hali ya kutupwa isiyojulikana mpaka sasa kana kwamba ilikuwa imempata Mungu na tena kana kwamba ilikuwa imempoteza Mungu. Kuteseka katika umiliki na kuteseka katika ufukara—hisia hizi zinajulikana tu na wale wanaozipitia wao wenyewe; ni kitu ambacho mwanadamu hana uwezo wala njia ya kueleza. Majeraha ya aina hii ni yale Mungu alimpa kila mtu kama aina ya uzoefu usioshikika na mali. Maudhui ya matamko yaliyotolewa na Mungu katika mwaka huu kweli yamo katika sehemu mbili kuu: Ya kwanza ni sehemu ambapo Mungu alishuka katika dunia ya wanadamu kuwaalika binadamu kuja mbele ya kiti Chake cha enzi kama wageni; ya pili, sehemu ambapo binadamu, baada ya kula na kunywa hadi kushiba, walitumiwa na Mungu kama watendaji huduma. Bila shaka ni dhahiri kwamba sehemu ya kwanza ni matakwa ya binadamu ya thamani nyingi na ari zaidi, hasa kwa kuwa wanadamu wamezoea tangu zamani kufanya kufurahia kila kitu cha Mungu kuwa lengo la imani yao Kwake. Hii ndiyo maana, punde Mungu alipoanza kuyapa matamko Yake sauti, binadamu wote walikuwa tayari kuingia katika ufalme na walisubiri hapo ili Mungu awape thawabu tofauti. Watu katika hali hizi hawakulipa gharama ya kufaa kabisa kwa kubadilisha tabia zao, kutafuta kumridhisha Mungu, kufikiria mapenzi ya Mungu na kadhalika. Kwa mtazamo wa haraka wa juu juu, wanadamu walionekana kushughulika huku na kule siku zote huku wakijitumia na kufanya kazi kwa ajili ya Mungu, wakati kwa kweli walikuwa wakifanya hesabu, katika mahala pa siri zaidi pa vina vya mioyo yao, hatua ifuatayo wanayopaswa kuchukua kupata baraka au kutawala kama wafalme. Mtu anaweza kusema kwamba, wakati moyo wa mwanadamu ulipokuwa ukimfurahia Mungu, ulikuwa ukifanya hila dhidi ya Mungu wakati huo huo. Wanadamu katika hali hii hukutana na chuki ya kina zaidi ya Mungu na karaha; tabia ya Mungu haivumilii binadamu yeyote kumdanganya au kumtumia. Lakini hekima ya Mungu haifikiki kwa mwanadamu yeyote. Ilikuwa katikati ya kuvumilia mateso haya yote ambapo Alisema sehemu ya kwanza ya matamko Yake. Kiasi cha mateso ambayo Mungu alivumilia, na ni kiasi gani cha kujali na fikira Alitumia wakati huu, hakuna mwanadamu anayeweza kuwaza. Lengo la sehemu ya kwanza ya haya matamko ni kufichua aina tofauti za ubaya ambazo mwanadamu huonyesha anapokabiliwa na cheo na faida, na kufichua ulafi na kustahili dharau kwa mwanadamu. Hata ingawa, katika kuzungumza, Mungu huyafuma maneno Yake kwa sauti ya kweli na ya moyo ya mama anayependa, ghadhabu katika kina zaidi ya moyo Wake huwaka kama jua la mchana ambalo Anaelekeza dhidi ya adui Zake. Mungu hataki katika hali yoyote kuzungumza kwa kundi la watu wasio na usawa wa kawaida wa jamii ya binadamu, na hivyo, wakati wowote Anapozungumza, Anazuia ghadhabu iliyo ndani ya moyo Wake ilhali wakati huo huo Akijizuia ili kuonyesha tamko Lake. Zaidi ya hayo Anazungumza kwa jamii ya binadamu isiyo na ubinadamu wa kawaida, isiyo na mantiki, potovu kabisa, na ulafi kugeuka kuwa asili ya pili, na isiyotii na inayomwasi Mungu hadi mwisho kabisa. Vina ambavyo jamii ya mwanadamu imeanguka vinaweza kufikiriwa kwa urahisi, na hata zaidi chuki na karaha ya Mungu kwa jamii ya mwanadamu inaweza kufikiriwa kwa urahisi, lakini jamii ya binadamu ina ugumu kufikiri kwamba maumivu waliyompa Mungu hayawezi kuelezwa na maneno. Lakini ilikuwa hasa katika usuli huu—ambapo hakuna mtu aliweza kugundua jinsi moyo wa Mungu unavyoteseka, na aidha hakuna mtu aliyegundua jinsi jamii ya binadamu isivyo ya akili na isiyorekebishika—kwamba kila mtu, bila aibu yoyote au haya hata kidogo, aliona kuwa jambo la kawaida kwamba alikuwa na haki kama wana wa Mungu kupokea thawabu zote ambazo Alikuwa amemtayarishia mwanadamu, hata kwa kiwango cha kugombana, kusiwe na mtu aliyetaka kubaki nyuma na wote wakiogopa sana kupoteza. Kufikia sasa unapaswa kujua ni nafasi ya aina gani ambayo watu wakati huo walimiliki machoni pa Mungu. Jamii ya wanadamu kama hii inawezaje kupata thawabu za Mungu? Lakini kile ambacho mwanadamu hupokea kutoka kwa Mungu ni hazina ya thamani sana nyakati zote, na kinyume chake kile ambacho Mungu hupokea kutoka kwa mwanadamu ni uchungu mkubwa kabisa. Tangu mwanzoni mwa uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, hiki ndicho mwanadamu amepokea daima kutoka kwa Mungu na kile ambacho amempa Mungu daima kama malipo.
Hata ingawa Mungu alijaa wasiwasi, Alipoona jamii hii ya binadamu, iliyo potovu kwa kina sana, Hakuwa na chaguo ila kuitupa ndani ya jahanamu ili iweze kusafishwa. Hii ni sehemu ya pili ya tamko la Mungu, ambapo Mungu aliwatumia binadamu kama watendaji huduma Wake. Katika sehemu hii, Mungu alitoka kuwa mpole hadi kuwa mkali, na kutoka machache hadi mengi, kuhusu mbinu na urefu, akitumia nafasi ya “nafsi ya Mungu” kama ubembe kufichua asili potovu ya mwanadamu ilhali wakati huo huo kuweka mbele vikundi tofauti vya[a] watendaji huduma, watu, na wana kwa watu kuchagua kutoka hapo. Bila shaka, kama vile Mungu alivyokuwa ametabiri, hakuna mtu aliyechagua kuwa mtendaji huduma kwa ajili ya Mungu, na badala yake wote walijitahidi kuwa nafsi ya Mungu. Hata ingawa, katika kipindi hiki, ukali ambao kwao Mungu alizungumza kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwahi kutarajia na sembuse kusikia, hata hivyo, kujali sana kuhusu hadhi, na juu ya hili, kushughulika kwa msisimko mkubwa na kupata baraka, hawakuwa na wakati wa kuunda fikira kuhusu sauti ya Mungu ya kuzungumza na njia Yake ya kuzungumza, badala yake wakinuia kutenda bila hadhari hadhi zao na kile kilichowangoja baadaye. Kwa njia hii, binadamu waliletwa, bila kujua, na tamko la Mungu ndani ya matata mengi Aliyokuwa amewawekea. Wakiwa wameshawishiwa, bila hiari, na mvuto wa siku za mbele na kudura yao, binadamu walijijua hawafai kuwa nafsi ya Mungu, na bado walikuwa wakisita kutenda kama watendaji huduma Wake. Wakiwa wamechanganyikiwa kati ya fikira hizi zinazopingana, bila kujijua walikubali hukumu ya pekee na kuadibu ambako Mungu alikuwa amewapa binadamu. Kwa kawaida, aina hii ya hukumu na usafishaji kilikuwa kitu ambacho binadamu hawakuwa tayari kukubali hata kidogo. Hata hivyo, Mungu tu ndiye aliye na hekima, na ni Yeye tu aliye na uwezo, kutoza unyenyekevu mpole kutoka kwa jamii hii potovu ya wanadamu, ili kwamba, watake au wasitake, wote walikubali mwishowe. Binadamu hawakuwa na mbadala kuchagua kutoka. Ni Mungu tu aliye na uamuzi wa mwisho, na ni Mungu tu anaweza kutumia mbinu kama hii kumpa mwanadamu ukweli na uhai na kumwonyesha mwelekeo. Mbinu hii ni kutoepukika kwa kazi ya Mungu kwa mwanadamu, na pia, bila shaka au ugomvi, ni haja ya lazima ya mwanadamu. Mungu hutumia mbinu kama hii kwa ajili ya kunena na kufanya kazi kupitisha ukweli huu kwa binadamu: Katika kumwokoa binadamu, Mungu hufanya hivyo kutokana na upendo na huruma Yake na kwa ajili ya usimamizi Wake; katika kupokea wokovu wa Mungu, jamii ya binadamu inafanya hivyo kwa sababu imeanguka hadi kwa hatua ambapo Mungu huzungumza Yeye binafsi tu. Mwanadamu anapopokea wokovu wa Mungu, hii ndiyo neema ya juu zaidi, na pia ni fadhila ya pekee, yaani, isingekuwa Mungu kulipa tamko Lake sauti Yeye binafsi, majaliwa ya jamii ya binadamu ingekuwa kutoweka. Wakati huo huo ambapo Anakirihi jamii ya binadamu, Mungu bado yuko tayari na mwenye radhi kulipa gharama yoyote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Wakati huo, mwanadamu huzungumza kwa kurudiarudia juu ya upendo wake kwa Mungu na jinsi anavyoweka yote wakfu kwa Mungu, anaasi dhidi ya Mungu na kupokonya kila aina ya neema kutoka kwa Mungu, na hata, wakati huo huo, akimwumiza Mungu na kuumiza moyo Wake kwa uchungu mbaya. Hivyo ndivyo ilivyo tofauti dhahiri kati ya asiye na ubinafsi na aliye na ubinafsi katika uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu!
Katika kufanya kazi na kuzungumza, Mungu halazimiki kufuata mbinu yoyote maalum, ila hufanya kufikia matokeo katika upande Wake. Kwa sababu hii, katika “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa,” Amehakikisha kutoonyesha utambulisho Wake kwa dhahiri, ila tu kufichua maneno machache kama “Kristo wa siku za mwisho,” “Mkuu wa ulimwengu,” na mengineyo. Hili haliathiri hata kidogo huduma ya Kristo au ufahamu wa binadamu wa Mungu, hasa kwa kuwa binadamu katika siku hizo za awali walikuwa wajinga kabisa kuhusu dhana ya “Kristo” na “kupata mwili,” kiasi kwamba Mungu alilazimika kujinyenyekeza Mwenyewe kuwa mtu na “kazi maalum” kuonyesha tamko Lake. Huu ni mfano wa nia ya juhudi ya Mungu, kwa sababu watu wakati huo wangeweza tu kukubali aina hii ya utambulisho. Bila kujali aina ya utambulisho ambao Mungu hutumia, matokeo ya kazi Yake hayaathiriwi, kwa sababu katika yote Anayofanya Mungu hunuia kumwezesha mwanadamu kubadilika, kumwezesha mwanadamu kupata wokovu wa Mungu. Bila kujali Anachokifanya, Mungu daima hufikiria mahitaji ya mwanadamu. Hii ndiyo nia ya Mungu kufanya kazi na kuzungumza. Hata ingawa Mungu yuko mwangalifu kikamilifu katika kufikiria vipengele vyote vya binadamu, na ni mwenye busara kikamilifu katika yote Anayofanya, Naweza kusema hili: Kama Mungu hangejishuhudia Yeye Mwenyewe, hakungekuwa na mmoja miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa ambaye anayeweza kumtambua Mungu Mwenyewe au kusimama kumshuhudia Mungu Mwenyewe. Kama Mungu angeendelea kutumia “mtu na kazi maalum” kama aina ya utambulisho katika kazi Yake, hakungekuwa na binadamu hata mmoja ambaye angemchukulia Mungu kama Mungu—huu ni huzuni wa binadamu. Yaani, miongoni mwa jamii ya binadamu walioumbwa hakuna mtu anayeweza kumjua Mungu, hakuna wa kumpenda Mungu, kumjali Mungu na kumkaribia Mungu. Imani ya mwanadamu ni kwa ajili ya kupata baraka pekee. Utambulisho wa Mungu kama mtu aliye na kazi maalum imetoa dokezo kwa kila binadamu: Binadamu anaona ikiwa rahisi kumchukulia Mungu kama mmoja miongoni mwa jamii ya wanadamu walioumbwa; uchungu na fedheha ya juu kabisa ambayo binadamu anamwumiza nayo Mungu ni hiyo hasa, Anapoonekana na kufanya kazi kwa wazi, Mungu bado anakataliwa na mwanadamu na hata kusahaulika na yeye. Mungu huvumilia fedheha ya juu zaidi ili kuiokoa jamii ya binadamu; katika kutoa kila kitu, lengo Lake ni kumwokoa binadamu, kupata utambuzi wa binadamu. Gharama ambayo Mungu amelipa kwa ajili ya haya yote ni kitu ambacho kila mtu aliye na dhamiri anapaswa kuweza kuthamini. Jamii ya binadamu imepata kuzungumza na kufanya kazi kwa Mungu, na kupata wokovu wa Mungu. Wakati uo huo, hakuna mtu ambaye amefikiria kuuliza hili: Na ni nini ambacho Mungu amepata kutoka kwa binadamu? Kutoka katika kila tamko la Mungu, binadamu wamepata ukweli, wamefanikiwa kubadilika, wamepata mwelekeo katika maisha; lakini kile ambacho Mungu amekipata si zaidi ya maneno Anayowia na minong’ono dhaifu za sifa. Hakika hii siyo fidia ambayo Mungu anadai kutoka kwa mwanadamu?
Ingawa matamko mengi ya Mungu sasa yameonyeshwa, watu wengi bado wamepumzika kidogo katika hatua inayowakilishwa na “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa” katika ufahamu na maarifa yao ya Mungu, ambapo kwayo hawajaendelea mbele—hii kweli ni mada chungu. Sehemu hii ya “maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa” ni ufunguo tu wa kufungua moyo wa binadamu; kupumzika kidogo hapa ni kutotimiza nia ya Mungu kabisa. Lengo la Mungu katika kuzungumza sehemu hii ya matamko Yake ni kumleta binadamu kutoka kwa Enzi ya Neema tu hadi katika Enzi ya Ufalme; Hataki hata kidogo binadamu wabaki wakisimama katika sehemu hii ya matamko Yake au hata kuchukua sehemu hii ya matamko Yake kama mwongozo, vinginevyo matamko ya baadaye ya Mungu hayatakuwa muhimu au ya maana. Iwapo kuna yeyote ambaye bado hawezi kuingia katika kile ambacho Mungu anadai kwamba mwanadamu apate katika sehemu hii ya matamko Yake, basi kuingia kwa mtu huyo kunabaki kusikojulikana. Sehemu hii ya matamko ya Mungu inajumuisha mahitaji ya msingi kabisa ambayo Mungu hutaka kutoka kwa mwanadamu katika Enzi ya Ufalme, na ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo binadamu ataingia katika njia sahihi. Iwapo wewe ni mtu asiyeelewa chochote, basi ni bora uanze kwa kusoma maneno katika sehemu hii!
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yameacha "vikundi tofauti vya."

 kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili


Kujua zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni