Jumapili, 11 Novemba 2018

Matamshi ya Mungu | "Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu"

Matamshi ya Mungu | "Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu"
Mwenyezi Mungu anasema, "Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii kwa moyo wake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi inayofanywa na Mungu daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya vitendo kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni