Jumanne, 4 Desemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu"
Mwenyezi Mungu anasema, "Hata kama Mungu mwenye mwili hunena, kufanya kazi, au kutenda miujiza, Anafanya kazi kubwa katika usimamizi Wake, kazi ambayo haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kazi ya mwanadamu ni kufanya tu wajibu wake kama kiumbe katika hatua fulani ya usimamizi wa Mungu. Bila usimamizi kama huo, yaani, ikiwa huduma ya Mungu kuwa mwili itapotea, pia wajibu wa viumbe utapotea. Kazi ya Mungu kuendeleza huduma Yake ni kumsimamia mwanadamu, ilhali mwanadamu afanyapo wajibu wake ni kutimiza wajibu wake ili kuafikia masharti ya Muumba na haiwezi kwa vyovyote vile kuchukuliwa kwamba ameendeleza huduma ya mtu yeyote. Kwa nafsi asili ya Mungu, yaani, Roho, kazi ya Mungu ni usimamizi wake, bali kwa Mungu kuwa mwili akiwa na umbile la nje la kiumbe, kazi yake ni kuendeleza huduma Yake. Kazi yoyote Aifanyayo Mungu ni ya kuendeleza huduma Yake, na mwanadamu anaweza tu kufanya awezalo ndani ya upeo Wake wa usimamizi na chini ya uongozi Wake."
Tazama Video: Utongoaji wa Neno la Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni