Jumanne, 19 Februari 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Nne

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika moyo wa Bwana Yesu, Alikuwa radhi kujitoa kwa ajili ya mwanadamu, kujitoa Mwenyewe. Alikuwa radhi pia kuchukua nafasi ya sadaka ya dhambi, kusulubishwa msalabani, na Alikuwa na hamu ya kukamilisha kazi hii. Alipoona hali za kusikitisha za maisha ya binadamu, Alitaka hata zaidi kukamilisha misheni Yake haraka iwezekanavyo, bila ya kuchelewa hata dakika au sekunde moja. Alipokuwa na hisia hii ya dharura, Alikuwa hafikirii namna ambavyo maumivu Yake binafsi yangekuwa wala hakufikiria kwa muda wowote zaidi kuhusu ni kiwango kipi cha udhalilishaji ambacho Angevumilia—Alishikilia azimio moja tu moyoni Mwake: Mradi tu Alijitoa Mwenyewe, mradi tu Angesulubishwa msalabani kama sadaka ya dhambi, mapenzi ya Mungu yangetendeka na Angeweza kuanza kazi mpya. Maisha ya wanadamu katika dhambi, hali yao ya kuwepo katika dhambi ingebadilika kabisa. Imani yake na kile Alichoamua kufanya vyote vilihusiana na kumwokoa binadamu, na Alikuwa na lengo moja tu: kufanya mapenzi ya Mungu ili Aweze kuanza kwa ufanisi hatua ambayo ingefuata katika kazi Yake. Haya ndiyo yaliyokuwa katika akili ya Bwana Yesu wakati huo.”

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Sikiliza zaidi: Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu I" Sehemu ya Tatu

Tufuate:Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni