Jumapili, 3 Februari 2019

"Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)" Sehemu ya Kwanza

"Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)" Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii: Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

Mwenyezi Mungu anasema, Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu. Lakini, hata hivyo, kwanza nitawaacha mchague kimoja kati ya vitu viwili ambavyo Nimezungumzia hivi punde. (Ninachagua kuhusu kumjua Mungu.) (Tunafikiri kwamba kufanyia ushirika maarifa ya Mungu ni bora pia.) Mnadhani mambo ambayo tumekuwa tukiyafanyia ushirika hivi karibuni kuhusu kumjua Mungu yanawezekana? Ni haki kusema kuwa ni nje ya uwezo wa watu wengi. Mwaweza kukosa kusadiki maneno haya. Kwa nini Ninasema hili? Kwa sababu mlipokuwa mkisikiliza Niliyokuwa nikisema awali, haijalishi Niliyasema vipi, au ni kwa maneno gani, moja kwa moja na kinadharia mlikuwa mnatambua Nilichokuwa nikisema, lakini tatizo lenu kubwa ni kwamba, hamkuelewa ni kwa nini Niliyasema mambo haya, ni kwa nini nilizizungumzia hizi mada. Hiki ndicho kiini cha hili suala. Na kwa hiyo, japo kusikia kwenu haya mambo kuliongeza na kuimarisha uelewa wenu kuhusu Mungu na matendo Yake, bado mnapata ugumu kumjua Mungu. Baada ya kusikia Nilichokisema, wengi wenu hawaelewi ni kwa nini Nilisema hili, na lina uhusiano gani na kumjua Mungu. Ugumu wenu wa kuelewa uhusiano wake na kumjua Mungu unahusu nini? Mmewahi kuliwazia hili? Huenda hamjawahi. Sababu ya kutoelewa mambo haya ni kwa sababu uzoefu wenu wa kimaisha ni wa juujuu sana. Ikiwa ufahamu na uzoefu wa watu kuhusu maneno ya Mungu utabaki kuwa wa juujuu, basi ufahamu wao mkubwa kuhusu Mungu utakuwa si yakini na kidhahania—utakuwa wa hali ya chini, wa kimafundisho, na wa kinadharia. Kinadharia, yanaonekana au kusikika kuwa na mantiki na razini, ila ufahamu kuhusu Mungu utokao vinywani mwa watu ni mtupu. Na mbona Ninasema kuwa ni mtupu? Kwa sababu, kwa hakika, moyoni mwako hauko wazi kama maneno kuhusu kumjua Mungu yatokayo kinywani mwako ni sawa au la, ikiwa ni sahihi au la. Hivyo basi, japo watu wengi wamesikia taarifa na mada nyingi kuhusu kumjua Mungu, ufahamu wao kuhusu Mungu haujatoka nje ya nadharia na mafundisho ya yasiyo yakini na dhahania. Kwa hiyo hili tatizo linaweza kusuluhishwa vipi? Je, mmewahi kuliwazia hilo? Ikiwa watu hawautafuti ukweli, wanaweza kuwa na uhalisi? Ikiwa watu hawautafuti ukweli, basi bila shaka hawana uhalisi, na hivyo, kwa hakika hawana ufahamu au uzoefu wa maneno ya Mungu. Je, yawezekana wasioyafahamu maneno ya Mungu wamfahamu Mungu? Hawawezi Kabisa. Haya mawili yameshikamana. Hivyo, watu wengi husema, “Kumjua Mungu kwawezaje kuwa kugumu hivi? Ninapozungumzia kujijua mimi mwenyewe, naweza kuzungumza kwa saa nyingi, ila inapofika kumjua Mungu nakoswa maneno. Hata ninapoweza kusema machache, ni kwa kushurutishwa, yanakosa uchangamfu—hata yanasikika ya kufedhehesha ninapojisikia nikiyasema.” Hiki ndicho chanzo. Ukihisi kwamba kumjua Mungu ni kugumu sana, kwamba kunakuchosha, kwamba huna la kuzungumzia—huna chochote cha kufanya ushirika na kuwapa wengine, na kujipa wewe mwenyewe—basi hili linathibitisha kwamba hujayapitia maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu ni nini? Je, maneno ya Mungu sio maonyesho ya kile Mungu anacho na alicho? Ikiwa hujapitia uzoefu wa maneno ya Mungu, unaweza kuwa na ufahamu wowote kuhusu anacho na alicho. Kwa hakika siyo. Vitu hivi vyote vimeshikamana. Ikiwa huna uzoefu wa maneno ya Mungu, basi huwezi kuelewa mapenzi ya Mungu, na hutajua tabia Yake ni nini, Anachokipenda, Anachokichukia, mahitaji Yake kwa mwanadamu ni yapi, mtazamo Wake kwa walio wazuri, na kwa wale walio waovu ni upi—kwa hakika haya yote yatakuwa tata na yenye mashaka kwako. Ikiwa mnamwamini Mungu katikati ya haya mashaka, wakati mnaposema kuwa nyinyi ni miongoni mwa wale wanaoutafuta ukweli na kumfuata Mungu, je, haya maneno yana uhalisi? Hayana! Hivyo, sasa, fanyeni uamuzi wenu: Mnachagua mada gani leo? (Tunachagua kuingia katika maisha.) Ni vipengele vipi vya mada ambavyo hamvifahamu kuhusu kuingia katika maisha? Je, mioyo yenu inawaambia kitu chochote? Bado hamjui, je mwajua? Je, dada na ndugu wengine wamechagua mada gani? (Tungependa kusikia kuhusu kumjua Mungu.) Wengi wenu mmechagua kumjua Mungu. Hivyo tuendelee kufanya ushirika kuhusu kumjua Mungu.
Nyinyi nyote mna shauku ya kuisikia mada tutakayoifanyia ushirika, sivyo? Mada tutakayowasiliana kwa karibu leo pia inahusiana na mada ya “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ambayo tumekuwa tukizungumzia hivi karibuni. Tumeongea mengi kuhusu jinsi “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote,” ambayo makusudi yake yalikuwa kutumia njia na mitazamo mbalimbali kuwaarifu watu jinsi Mungu anatawala juu ya vitu vyote, ni kwa njia gani Anavitawala vitu vyote, na ni kwa kanuni gani anavisimamia vitu vyote, ili kwamba viweze kuishi katika hii sayari Aliyoumba Mungu. Tulizungumza pia mengi kuhusu jinsi ambavyo Mungu anamkimu mwanadamu: ni kwa njia gani Mungu anamkimu mwanadamu, ni mazingira ya kuishi ya aina gani Mungu anampa mwanadamu, na ni kwa njia na nguvu gani Anampa mwanadamu mazingira thabiti ya kuishi. Japo Sikuzungumzia moja kwa moja uhusiano baina ya utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, uendeshaji Wake wa vitu vyote na usimamizi Wake, kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja Nilisema ni kwa nini Anaviendesha vitu vyote namna hii, na ni kwa nini Anamkimu na kumlisha mwanadamu namna hii—yote ambayo yanahusu usimamizi wa Mungu. Maudhui tuliyoyazungumzia yalikuwa mengi na mapana—kuanzia mazingira makubwa hadi vitu vidogo zaidi kama mahitaji na lishe ya msingi ya wanadamu; kuanzia jinsi Mungu anaviongoza vitu vyote na kuvifanya vitende kazi kwa utaratibu, hadi kwenye mazingira ya kuishi sahihi na ya kufaa Aliyoyaumba kwa ajili ya watu wa kila jamii, na kadhalika. Haya maudhui mapana yanahusu jinsi mwanadamu anaishi katika mwili. Hivi ni kusema, yote yanahusiana na vitu katika ulimwengu halisi vinavyoonekana kwa macho ya kawaida, na ambavyo mwanadamu anaweza kuvihisi, kwa mfano, milima, mito, bahari, tambarare… Hivi vyote ni vitu vinavyoweza kuonekana na kuguswa. Nizungumzapo kuhusu hewa na halijoto, mnaweza kutumia pumzi zenu kuhisi moja kwa moja uwepo wa hewa, na miili yenu kuhisi kama halijoto iko juu au chini. Miti, nyasi, na ndege na wanyama porini, vitu vinavyopaa angani, na kutembea ardhini, na wanyama wadogo mbalimbali watokezao kutoka matunduni, vyote vinaweza kuonekana kwa wanadamu kwa macho yao wenyewe na kusikika kwa masikio yao wenyewe. Japo mawanda ya vitu kama hivyo ni mapana, miongoni mwa vitu vyote vinawakilisha tu ulimwengu halisi. Vitu yakinifu ni vitu ambavyo watu wanaweza kuviona na kuvihisi, yaani, ukivigusa, utavihisi, na macho yako yakiviona, ubongo wako utakupatia umbo, picha. Ni vitu ambavyo ni halisi na kweli; kwako si dhahania, bali vina umbo; vinaweza kuwa mraba, au duara, au virefu au vifupi; na kila kimoja kinakupa taswira tofauti. Vitu hivi vyote vinawakilisha sehemu ile yakinifu ya vitu vyote. Na hivi, “vitu vyote” katika “utawala wa Mungu juu ya vitu vyote” vinajumuisha nini kwa Mungu? Havijumuishi tu vitu ambavyo watu wanaweza kuona na kugusa, bali, vilevile, visivyoonekana na visivyoshikika. Hii ni mojawapo ya maana za kweli za utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Hata kama vitu hivi havionekani na havishikiki kwa watu, kwa Mungu, alimradi vinaweza kuonekana kwa jicho Lake na vipo ndani ya ukuu Wake, kwa hakika vipo. Hata kama, kwa mwanadamu, ni dhahania na visivyofikirika—na hata kama, aidha, havionekani na havishikiki—kwa Mungu kwa kweli na kwa uhalisi vipo. Huo ndio ulimwengu mwingine wa vitu vyote ambavyo Mungu anatawala, na ni sehemu nyingine ya mawanda mengine ambayo Anatawala. Hii ndiyo mada ambayo tutaifanyia ushirika leo—jinsi Mungu anatawala na kuuongoza ulimwengu wa kiroho. Kwa kuwa mada hii inagusia jinsi Mungu anatawala na kusimamia vitu vyote, inahusiana na ulimwengu ulio nje ya ulimwengu yakinifu—ulimwengu wa kiroho—na kwa hivyo ni muhimu sana kwetu kuuelewa. Ni baada tu ya kushiriki na kuelewa maudhui haya ndipo watu wanaweza kuelewa kwa hakika maana ya kweli ya maneno “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.” Hii ndiyo maana tutazungumzia mada hii. Na shabaha ya mada hii ni kukamilisha dhamira ya “Mungu anavitawala vitu vyote, na Mungu anavisimamia vitu vyote.” Pengine, mtakapoisikia mada hii, inaweza kuonekana ni ya ajabu na isiyoaminika kwenu—lakini bila kujali mnavyohisi, kwa kuwa ulimwengu wa kiroho ni sehemu moja ya vitu vinavyotawaliwa na Mungu, ni sharti mjifunze kitu kuhusu mada hii. Baada ya kujifunza, mtakuwa na ufahamu wa kina, uelewa na maarifa kuhusu maneno “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.”

kutoka katika Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni