Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tatu
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Namna Ambavyo Mungu Huanzisha Matokeo Ya Binadamu na Kiwango Ambacho Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu Swali la Kiutendaji Huleta Aina Zote za Aibu kwa Watu
Mwenyezi Mungu anasema, Kabla ya kuwa na mitazamo au hitimisho zako binafsi, unafaa kwanza kuelewa mwelekeo wa Mungu kwako, kile ambacho Mungu anafikiria, na kuamua kama kufikiria kwako ni sahihi au la. Mungu hajawahi kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya mtu, na Hajawahi kutumia kiwango cha mateso yaliyovumiliwa na mtu katika kuasisi matokeo yake. Basi Mungu hutumia kiwango gani katika kuasisi matokeo ya binadamu? Kutumia vipimo vya muda katika kuasisi matokeo ya binadamu—hii ndiyo inaingiliana zaidi na dhana za watu. Na pia kuna hao watu binafsi ambao mara nyingi mnawaona, wale ambao katika wakati fulani walijitolea kabisa, wakatumia muda mwingi kabisa, wakagharamika kabisa, wakateseka kabisa. Hawa ndio, kwa maoni yenu, wanaweza kuokolewa na Mungu. Kile tu ambacho watu hawa wanaonyesha, yote wanayoishi kwa kudhihirisha, ndiyo hasa dhana ya wanadamu kuhusu kiwango ambacho Mungu anaanzisha kuhusiana na matokeo ya binadamu. Bila kujali ni nini unachosadiki, Sitaorodhesha mifano hii mmoja baada ya mwingine. Nikiongea kwa ujumla, mradi tu si kiwango cha kufikiria binafsi kwa Mungu, basi kinakuja kutoka kwenye kufikiria kwa binadamu na ni dhana tu ya binadamu. Ni nini athari za kusisitiza bila mwelekeo dhana na kufikiria kwako binafsi? Bila shaka, athari inaweza kuwa tu Mungu akikusukuma mbali. Hii ni kwa sababu siku zote unaringa kuhusu sifa zako mbele ya Mungu, unashindana na Mungu, na kuleta mzozo dhidi ya Mungu, na hujaribu hata kufahamu kwa kweli kufikiria kwa Mungu, wala hujaribu kuzifahamu nia za Mungu na mwelekeo wa Mungu kwa binadamu. Kuendelea mbele hivi ni kujiheshimu kuliko yote na wala si kumheshimu Mungu. Unajisadiki; husadiki Mungu. Mungu hataki mtu wa aina hii, na Mungu hatamwokoa mtu wa aina hii. Kama huwezi kuachilia aina hii ya mtazamo, na kisha kuirekebisha mitazamo hii ya kale isiyokuwa sahihi; kama ungeweza kuendelea mbele kulingana na maagizo ya Mungu; anza kutenda njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa sasa na kusonga mbele; kuweza kuheshimu Mungu na kumwona kuwa mkubwa katika mambo yote; usitumie ndoto zako za kibinafsi, mitazamo au imani katika kujifafanua, kumfafanua Mungu. Na badala yake, unazitafuta nia za Mungu kwa hali zote, unatimiza utambuzi na uelewa wa mwelekeo wa Mungu kwa binadamu, na unatumia kiwango cha Mungu kutosheleza Mungu—kufanya hivi kungependeza! Huku kungemaanisha karibu unaanza katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni