Jumapili, 3 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa Makanisa | Sura ya 104

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa Makanisa | Sura ya 104

Watu, matukio na vitu vyote nje Yangu vitakufa na kuwakatika hali ya kutokuwepo, ilhali watu, matukio na vitu vyote vilivyo ndani Yangu vitapata kila kitu kutoka Kwangu na kuingia katika utukufu pamoja na Mimi, kuingia katika Mlima Wangu Sayuni, makazi Yangu, na kuishi pamoja kwa amani nami milele. Niliumba vitu vyote mwanzoni na Nitamaliza kazi Yangu mwishowe, na pia Nitatawala milele kama Mfalme. Katikati, pia Ninaongoza na kuutawala ulimwengu mzima. Hakuna anayeweza kuondoa mamlaka Yangu, kwani Mimi ni Mungu mmoja Mwenyewe, na pia Nina uwezo wa kupitisha mamlaka Yangu kwawazaliwa Wangu wa Kwanza, ili wazaliwa Wangu wa kwanza waweze kutawala kandokando Yangu. Hili lipo milele na haliwezi kubadilishwa kamwe. Hii ni amri Yangu ya utawala. (Popote Ninapojadili amri Yangu ya utawala panarejelea kile kinachofanyika katika ufalme Wangu na kinakuwepo milele na hakiwezi kubadilishwa kamwe.) Lazima kila mtu aridhishwe moyoni na kwa neno, na lazima aone uwezo Wangu mkubwa ndani ya wale Ninaowapenda. Hakuna anayeweza kuliaibisha jina Langu—ni lazima nyote mtoke hapa! Si kwamba Sina huruma, ila kwamba wewe ni mdhalimu. Ukikosea kuadibu Kwangu basi Nitakushughulikia na kukufanya ufe milele na milele. (Bila shaka, haya yote yanawalenga watu walio nje ya wazaliwa Wangu wa kwanza.) Nyumba Yangu haitaki takataka kama hiyo, hivyo harakisha na uondoke hapa! Usichelewe hata kwa dakika moja au kwa sekunde moja! Lazima ufanye Ninachosema, au sivyo Nitakuangamiza kwa neno moja. Ni heri usisite bado, ni heri usidanganye bado. Wale wanaobuni upuuzi mbele Yangu, wale wanaodanganya mbele Yangu—ondokeni haraka! Muda Wangu ni mchache kwa mambo kama hayo. (Ikifika wakati wa kufanya huduma watafanya huduma, na ikifika wakati wa kuondoka wataondoka. Nafanya mambo kwa hekima, bila kupoteza dakika au sekunde, hazipotezwi hata kidogo. Yote ni ya haki na sahihi kabisa.) Lakini kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, Mimi ni mvumilivu bila kikomo nami Napenda hadi mwisho milele, Nikiwawezesha kufurahia baraka nyingi milele na maisha ya milele pamoja nami, na kwa sasa kutovumilia kipingamizi au hukumu tena. (Hii inahusu wakati mnaanza kufurahia baraka.) Hii ni baraka na ahadi isiyo na kikomo kwa wazaliwa Wangu wa kwanza Nilipoiumba dunia. Mnapaswa kuiona haki Yangu humo—Napenda wale ambao Nimewajaalia, Nawachukia wale ambao Nimewaacha na kuwaondoa, milele na milele.
Kama wazaliwa Wangu wa kwanza, nyote mnapaswa kushikilia wajibu wenu wenyewe na kusimama katika nafasi zenu, muwe malimbuko yaliyonyakuliwa mbele Yangu na kukubali uchunguzi Wangu binafsi, ili mweze kuishi kwa kudhihirisha taswira Yangu tukufu na mwanga wa utukufu Wangu uweze kung’aa kupitia nyuso zenu, ili matamshi Yangu yaweze kuenezwa kupitia vinywa vyenu, ili kwamba ufalme Wangu uweze kutawaliwa na ninyi, na ili kwamba watu Wangu waweze kutawaliwa na ninyi. Hapa Nataja “malimbuko” na pia neno kama “kunyakuliwa.” Malimbuko ni nini? Katika dhana za watu, wanafikiri ni kundi la kwanza la watu wanaonyakuliwa, au kwamba inarejelea washindi au watu ambao ni wazaliwa wa kwanza. Haya yote ni uwongo na ufahamu wa uwongo wa maneno Yangu. Malimbuko ni watu ambao wamepokea ufunuo kutoka Kwangu na kupata mamlaka kutoka Kwangu. Hii inayodaiwa kuwa “malimbuko” inahusu kumilikiwa na Mimi, kujaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. “Malimbuko” halimaanishi ya kwanza katika mfuatano. “Malimbuko” si jambo yakinifu machoni pa mwanadamu. Inayodaiwa kuwa “malimbuko” inahusu kitu kinachotoa harufu nzuri (hii ni maana ya ishara), yaani, wale wanaoweza kuishi kwa kunidhihirisha, kunidhihirisha, na kuishi nami milele. Ninapozungumza kuhusu “matunda” Ninarejelea wana na watu Wangu wote, ilhali malimbuko linarejelea wazaliwa wa kwanza ambao watatawala kama wafalme kandokando Yangu. Hivyo, “malimbuko” linapaswa kuelezwa kama kuwa na mamlaka. Hiyo ni maana ya kweli. “Kunyakuliwa” si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanavyofikiria. Hili ni kosa kubwa sana. Kunyakuliwa kunarejelea kujaaliwa Kwangu na kuchagua. Kunawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. Wale ambao wamepata hadhi ya wazaliwa wa kwanza, hadhi ya wana Wangu, au watu Wangu, wote ni watu ambao wamenyakuliwa. Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu.
Mtu anaelezaje “tarumbeta takatifu”? Ni nini ufahamu wenu wa hili? Mbona inasemwa kuwa takatifu na iliyopigwa tayari? Hili linapaswa kuelezwa kutoka kwa hatua za kazi Yangu na kueleweka kutoka kwa mbinu ya kazi Yangu. Wakati ambapo hukumu Yangu inatangazwa kwa umma ni wakati tabia Yangu inafichuliwa kwa mataifa na watu wote. Huo ndio wakati tarumbeta takatifu inapigwa. Yaani kwamba Nasema mara nyingi kwamba tabia Yangu ni takatifu na isiyokosewa, ambayo ndiyo maana “takatifu” inatumika kuelezea “tarumbeta.” Inaweza kuonekana kutoka kwa hili kwamba “tarumbeta” inarejelea tabia Yangu na inawakilisha kile Nilicho na Nilicho nacho. Inaweza pia kusemwa kwamba hukumu Yangu inaendelea kila siku, ghadhabu Yangu inatolewa kila siku, laana Yangu inafikia kila kitu kisicholingana na tabia Yangu kila siku. Basi inaweza kusemwa kwamba wakati hukumu Yangu huanza ni wakati tarumbeta takatifu inapigwa, na inapigwa kila siku, bila kukoma kwa muda au bila kukoma kwa dakika au sekunde. Kuanzia sasa na kuendelea, tarumbeta takatifu itatoa sauti kubwa zaidi na zaidi sawa na kushuka kwa taratibu kwa maafa makuu. Yaani, pamoja na ufunuo wa hukumu Yangu ya haki, tabia Yangu itakuwa wazi zaidi na zaidi, na kile Nilicho na Nilicho nacho kitaongezwa ndani ya wazaliwa Wangu wa kwanza zaidi na zaidi. Hii ni mbinu ya kazi Yangu ya baadaye; kwa upande mmoja kuruzuku na kuwaokoa wale Ninaowapenda, na kwa upande mwingine kutumia maneno Yangu kuwafichua wale wote Ninaowadharau. Kumbuka! Hii ni mbinu ya kazi Yangu, hatua za kazi Yangu, ambayo ni kweli kabisa. Hii imepangwa na Mimi tangu uumbaji na haiwezi kubadilishwa na yeyote.
Bado kuna sehemu nyingi za maneno Yangu ambazo ni ngumu kwa watu kuelewa, hivyo basi Nimeendeleza zaidi njia Yangu ya kusema na mbinu Zangu za kufichua siri. Kwa maneno mengine, njia Yangu ya kusema inabadilika na kuwa nzuri zaidi kila siku, kwa mtindo na mbinu tofauti kila siku. Hizi ndizo hatua za kazi Yangu na haziwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Watu wanaweza tu kusema na kutenda kulingana na kile Ninachosema.Huu ni ukweli kabisa. Nimefanya mipango ya kufaa kwa nafsi Yangu na mwili Wangu. Ndani ya kila hatua na kitendo cha ubinadamu Wangu kuna kipengele cha hekima ya uungu Wangu. (Kwa kuwa binadamu hawana hekima hata kidogo, kusema kwamba wazaliwa wa kwanza wana hekima Yangu kunarejelea wazaliwa wa kwanza kuwa na tabia Yangu takatifu ndani yao.) Wazaliwa wa kwanza wanapofanya mambo ya kipumbavu, ni kwa sababu bado mna dalili za ubinadamu ndani yenu. Hivyo basi ni lazima muondoe upumbavu wa ubinadamu na kufanya kile Ninachokipenda na kukataa kile Ninachokichukia. Yeyote anayetoka Kwangu lazima arudi ndani Yangu. Yeyote anayezaliwa kutoka Kwangu lazima arudi ndani ya utukufu Wangu. Wale Ninaowachukia lazima waachwe na kuondolewa mmoja mmoja kutoka Kwangu. Hizi ndizo hatua za kazi Yangu, usimamizi Wangu, na mpango wa miaka 6,000 Nilioutengeneza. Wale wote Ninaowaacha wanapaswa kunitii na kuniacha kwa utii. Wale wote Ninaowapenda, kwa sababu ya baraka Nilizowapa, wanapaswa kunisifu ili jina Langu liweze kuwa tukufu hata zaidi, na mwanga mtukufu uweze kuongezwa kwa uso Wangu mtukufu, ili kwamba waweze kujaa hekima Yangu katika utukufu Wangu, na kulitukuza jina Langu hata zaidi katika mwanga Wangu mtakatifu!
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili  
Masomo yanayohusiana: Maneno ya Roho Mtakatifu kwa Makanisa-Tamko la Mia Moja na Tatu   


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni