Jumatatu, 25 Machi 2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tano


Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Tano
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Majaliwa ya Binadamu Yanaamuliwa na Mwelekeo Wake Kwa Mungu Sehemu ya Mwanzo ya Kumcha Mungu ni Kumtendea Kama Mungu Wale Watu Wasiotambuliwa na Mungu Maneno ya Maonyo

Mwenyezi Mungu anasema, "Mungu ni Mungu aliye hai, na kama vile tu watu wanavyotenda tofauti katika hali tofauti, ndivyo mwelekeo wa Mungu ulivyo katika utendakazi huu na unavyotofautiana kwa sababu Yeye si kikaragosi, wala Yeye si hewa tupu. Kupata kuujua mwelekeo wa Mungu ni jambo lenye thamani kwa wanadamu. Watu wanafaa kujifunza vipi, kwa kuujua mwelekeo wa Mungu, wanaweza kuijua tabia ya Mungu na kuuelewa moyo Wake kidogo kidogo. Unapouelewa moyo wa Mungu kidogo kidogo hutahisi kwamba kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ni jambo gumu la kutimiza. Kilicho zaidi ni kwamba, unapomwelewa Mungu, hakuna uwezekano wa wewe kufanya hitimisho kuhusu Yeye. Unapoacha kufanya hitimisho kuhusu Mungu, hakuna uwezekano wa wewe kumkosea Yeye, na bila kujua Mungu atakuongoza kuwa na maarifa Yake, na hivyo basi utamcha Mungu katika moyo wako. Utaacha kumfafanua Mungu kwa kutumia falsafa, zile barua, na nadharia ambazo umejifunza. Badala yake, kwa kutafuta nia za Mungu katika mambo yote na siku zote utaweza bila kufahamu kuwa mtu anayefuata moyo wa Mungu."

Kazi ya Mungu haionekani wala kugusika na wanadamu, lakini kulingana na Mungu, hatua za kila mmoja, pamoja na mwelekeo wake kwake Yeye—haya hayatambuliki tu na Mungu, lakini pia kuonekana vilevile. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anafaa kutambua na kuwa wazi kulihusu. Unaweza kuwa ukijiuliza siku zote: “Je, Mungu anajua kile ninachofanya hapa? Je, Mungu anajua kile ninachofikiria sasa hivi? Pengine Anajua, pengine Hajui.” Kama utakuwa na aina hii ya mtazamo, kufuata na kusadiki Mungu ilhali unatia shaka katika kazi Yake na uwepo Wake, basi hivi karibuni au baadaye siku itawadia ambapo utamghadhabisha, kwa sababu tayari unayumbayumba pembezoni pa jabali hatari. Nimewaona watu ambao wamesadiki katika Mungu kwa miaka mingi lakini bado hawajapata uhalisia wa ukweli, wala hawaelewi hata mapenzi ya Mungu. Kimo cha maisha yao hakipigi hatua yoyote, ukitii tu falsafa zile za kiwango cha chini zaidi. Hii ni kwa sababu watu hawa hawajawahi kuchukulia neno la Mungu kama maisha yao binafsi, na hawajawahi kukabiliana na kukubali uwepo Wake. Je, unafikiri kwamba Mungu huwaona watu kama hawa na kujawa na furaha? Je, wanamtuliza Yeye? Katika jinsi hiyo, ni mbinu ya imani ya watu katika Mungu ambayo inaamua majaliwa yao. Iwe ni swali la namna unavyotafuta Mungu au namna unavyomshughulikia Mungu, ni mwelekeo wako binafsi ambao ni jambo muhimu zaidi. Usikose kumjali Mungu ni kana kwamba Yeye ni hewa tupu nyuma ya kichwa chako. Siku zote fikiria kuhusu Mungu wa imani yako kama Mungu hai, Mungu halisi. Yeye hayupo kule juu kwenye mbingu ya tatu bila chochote cha kufanya. Badala yake, siku zote bila kusita Anaangalia kwenye mioyo ya kila mmoja, Akiangalia ni nini unachofanya, akichunguza kila neno dogo na kila tukio dogo, akiangalia mwenendo wako na mwelekeo wako kwa Mungu. Kama uko radhi kujitolea kwa Mungu au la, tabia yako yote na fikira zako na mawazo yako ya ndani zaidi ziko mbele ya Mungu, na yanaangaliwa na Yeye. Ni kulingana na tabia yako, kulingana na vitendo vyako, na kulingana na mwelekeo wako kwa Mungu, ambapo maoni Yake kwako, na mwenendo Wake kwako, vinaendelea vikibadilika. Ningependa kutoa ushauri fulani kwa wale ambao wangeweza kujiwekelea kwenye mikono ya Mungu kama mtoto mchanga, kana kwamba Yeye Anapaswa kukupenda sana, kana kwamba Asingewahi kukuacha, kana kwamba mwelekeo Wake kwako ni ule ule na usingeweza kubadilika: Acha kuota ndoto! Mungu ni mwenye haki katika kutendea kila mtu. Anakabiliana na kazi ya ushindi wa wanadamu na wokovu kwa bidii. Huo ndio usimamizi Wake. Anashughulikia kila mmoja kwa umakinifu, na wala si kama kiumbe cha kufugwa cha kucheza nacho. Upendo wa Mungu kwa binadamu si ule wa kudekeza au kupotosha; rehema na uvumilivu Wake kwa wanadamu si dokezi au ya kutotilia maanani. Kinyume cha mambo, upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kutunza, kusikitikia, na kuheshimu maisha; rehema na uvumilivu Wake vyote vinaonyesha matarajio Yake kwa binadamu; rehema na uvumilivu Wake ndivyo ambavyo binadamu anahitaji ili kuishi. Mungu yuko hai, na kwa hakika Mungu yupo; mwelekeo Wake kwa wanadamu unafuata kanuni, si yenye kutangazwa kama imani ya dini, na unaweza kubadilika. Mapenzi Yake kwa binadamu yanabadilika kwa utaratibu na kurekebishwa kwa muda, hali na mwelekeo wa kila mtu. Hivyo basi unafaa kuwa wazi kabisa katika hili na kuelewa kwamba kiini halisi cha Mungu hakibadiliki na tabia Yake itajitokeza katika nyakati tofauti na muktadha tofauti. Huenda usifikirie kwamba hili si suala muhimu, na wewe unatumia dhana zako za kibinafsi katika kufikiria namna ambavyo Mungu anafaa kufanya mambo. Lakini zipo nyakati ambapo kinyume kabisa cha mtazamo wako ni kweli, na kwa kutumia dhana zako za kibinafsi katika kujaribu na kumpima Mungu, tayari umemghadhabisha. Hii ni kwa sababu Mungu hafanyi kazi kama unavyofikiria wewe, Naye Mungu hatalishughulikia suala hili kama vile unavyosema Atalishughulikia. Na hivyo basi Nakukumbusha kuwa makini na mwenye hekima katika mtazamo wako katika kila kitu, na ujifunze namna ya kufuata kanuni ya kutembea kwenye njia ya Mungu katika mambo yote—kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima uimarishe uelewa dhabiti katika masuala ya mapenzi ya Mungu na mwelekeo wa Mungu; kutafuta watu walio na nuru kuuwasilisha kwako, na kutafuta kwa dhati. Usimwone Mungu wa imani yako kama kikaragosi—kuhukumu kiholela, kufikia hitimisho kiholela, kutomshughulikia Mungu kwa heshima Anayostahili. Katika mchakato wa wokovu wa Mungu Anapofafanua matokeo yako, bila kujali kama Yeye atakupa rehema, au uvumilivu, au hukumu na kuadibu, mwelekeo Wake kwako wewe unabadilika. Inategemea na mwelekeo wako kwa Mungu, na uelewa wako wa Mungu. Usiache dhana moja ya kupita ya maarifa au uelewa wako katika Mungu kumfafanua Yeye daima. Usisadiki katika Mungu aliyekufa; amini kwa yule aliye hai. Kumbuka hili! Ingawa Nimezungumzia ukweli fulani hapa, ukweli mliohitaji kusikia, kwa mujibu wa hali yenu ya sasa na kimo chenu cha sasa, Sitatoa mahitaji yoyote makubwa zaidi ili nisije nikaiondoa shauku yenu. Kufanya hivyo kutajaza mioyo yenu na huzuni na simanzi, na kuwafanya nyinyi kuhisi masikitiko mengi mno kwa Mungu. Badala yake Natumai kwamba mnaweza kutumia upendo wa Mungu katika mioyo yenu, na kutumia mwelekeo ambao ni wa heshima kwa Mungu wakati mnapotembea kwenye njia iliyo hapo mbele. Usimalizie suala la jinsi ya kushughulikia imani ya Mungu kwa kubahatisha. Lishughulikie kama mojawapo ya maswali makubwa zaidi yaliyopo. Liwekeni kwenye mioyo yenu, litieni kwenye matendo, unganeni nalo kupitia kwa maisha halisi—msikubaliane nalo kwa maneno pekee. Kwani hili ni suala la uzima na mauti, na ndilo ambalo litaamua hatima yako. Usilichukulie kama mzaha, kama mchezo wa mtoto! Baada ya kuwaambia maneno haya leo, Najiuliza mavuno ya uelewa yamekuwa nini katika akili zenu? Kunayo maswali yoyote ambayo ungependa kuuliza kuhusu kile Nilichokisema leo?"

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Tazama Video:Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni