Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III Mamlaka ya Mungu (II)” Sehemu ya Tano
1. Muumba Pekee Ndiye Anayeshikilia Nguvu za Maisha na Kifo juu ya Binadamu
Maudhui ya video hii:
Kifo: Awamu ya Sita
2. Yule Asiyejua Ukuu wa Muumba Atahangaika kwa Woga wa Kifo
3. Maisha ya Kuishi Ukitafuta Umaarufu na Utajiri Yatamwacha Mtu Akiwa na Hasara Akikabiliana na Kifo
Mwenyezi Mungu anasema, "Baadaya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kufifiliza na kuwa na wingu mbele yao, nayo ngozi laini, yenye unyumbufu inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa. Kusikia kwa mtu kunaanza kufifia, meno yake kulegea na kuanza kujiangukia, mwitikio wa mtu unaanza kuchelewachelewa, kutembea kunakuwa ni kwa kujikokota…. Wakati huu mtu ameaga kwaheri kabisa miaka yake ya nguvu ya ujana wake na kuingia katika maisha yake ya kwaheri: umri wa uzee. Kisha, mtu atakabiliana na kifo, awamu ya mwisho ya maisha ya binadamu."
Soma Zaidi: Neno la Mungu "Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni"
Yaliyopendekezwa: APP ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni