Jumatatu, 12 Agosti 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mungu Huweka Mipaka kwa ajili ya Vitu Vyote ili Kuwalea Binadamu Wote

Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya hii. Ni mada gani? (Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Inaonekana yale mambo na mada niliyoyazungumzia yaliwachia kila mtu wazo dhahiri. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu. Matendo haya yanayofanywa na Mungu hayakomei tu kwenye maandalizi Yake ya mazingira kwa ajili ya watu kuendelea kuishi na riziki zao za kila siku–yana mawanda mapana zaidi kuliko hayo. Licha ya aina mbili hizi za kazi, pia Anaandaa mazingira mengi na hali kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni lazima kwa ajili ya maisha ya mwanadamu. Hii ni mada nyingine ambayo tutaijadili leo, Pia inahusiana na matendo ya Mungu; vinginevyo, kuizungumzia hapa isingekuwa na maana. Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu lakini wana maana ya moja kwa moja ya "Mungu," ya neno hilo, au ya vipengele vyote vya kile Mungu anacho na alicho, huo sio uelewa wa kweli. Sasa, njia kwa ajili ya maarifa ya Mungu ni ipi? Ni kumjua Yeye, kujua kila kipengele Chake kupitia matendo Yake. Kwa hiyo, kinachofuata tunapaswa kushiriki kuhusu matendo ya Mungu pale alipoumba vitu vyote."

Tazama Zaidi: Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (I)” Sehemu ya Tatu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni