Punde tu Shetani anaposhindwa, hivyo ni kusema, punde tu mwanadamu anaposhindwa kabisa, mwanadamu ataelewa kwamba kazi yake yote ni kwa ajili ya wokovu, na kuwa mbinu ya wokovu huu ni kurejesha kutoka kwa mikono ya Shetani. Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika awamu tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Awamu hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, ambayo ni kusema, ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ambaye ameharibiwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati huo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani.
Hivyo, kama ilivyo kazi ya wokovu imegawanywa katika awamu tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika awamu tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu sio jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika awamu moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika awamu na vipindi, na vita vya kupigana na Shetani vinaambatana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. Pengine, katika mawazo ya mwanadamu, anaamini kuwa katika vita hivi Mungu atachukua silaha dhidi ya Shetani, katika njia sawa na vile ambavyo majeshi mawili yatapigana. Hili ni jambo ambalo akili ya mwanadamu ina uwezo wa kukisia, na lisilo dhahiri kupita kiasi na azimio lisiloweza kutendeka, na bado ndilo mwanadamu anaamini. Na kwa sababu Nasema hapa kuwa njia ya wokovu wa mwanadamu ni kupitia vita na Shetani, mwanadamu anawaza ya kwamba hivi ndivyo vita vinavyoendeshwa. Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, awamu tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika awamu tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizika kupitia kuzawadia mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu awe kamili. Kama jambo la kweli, vita na Shetani sio kuchukua silaha dhidi ya Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kuwa na ushahidi wa Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Awamu ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni awamu ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa utawala wa Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na awamu ya mwisho ya kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na mwanadamu kamwe hangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilika kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu wa usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha kazi yote ya Mungu ya usimamizi, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, ambayo ni kusema kuwa mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kuwa katika mateka ya Shetani. Shetani anashindwa kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye amechukuliwa mateka, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu ameachiliwa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, baada ya kuwa kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.
Mungu hana nia mbaya kwa viumbe na anataka tu kumshinda Shetani. Kazi yote yake—iwe ni kuadibu ama hukumu—inaelekezwa kwa Shetani; inafanyika kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na ina lengo moja: kufanya vita na Shetani mpaka mwisho kabisa! Na Mungu kamwe hatapumzika kabla ya kuwa mshindi dhidi ya Shetani! Atapumzika tu punde atakapomshinda Shetani. Kwa sababu kazi yote ambayo inafanywa na Mungu inaelekezwa kwa Shetani, na kwa sababu wale waliopotoshwa na Shetani wote wamo katika udhibiti wa utawala wa Shetani na wote wanamilikiwa na Shetani, bila kupambana dhidi ya Shetani na kumvunja, Shetani hangepumzika kushika watu hawa, na hawangeweza kupatwa. Kama hawangepatwa, ingethibitisha kwamba Shetani bado hakushindwa, na ya kwamba hakutiishwa. Na kwa hivyo, katika miaka 6,000 ya mpango wa usimamizi wa Mungu, kwenye wakati wa awamu ya kwanza Yeye alifanya kazi ya sheria, wakati wa awamu ya pili Yeye alifanya kazi ya Enzi ya Neema, yaani, kazi ya kusulubiwa, na wakati wa awamu ya tatu Yeye alifanya kazi ya kumshinda mwanadamu. Kazi hizi zote zilielekezwa katika kiwango ambacho Shetani alikuwa amempotosha mwanadamu, na yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na hakuna awamu moja ambayo si kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kiini cha miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi ni vita dhidi ya joka kubwa jekundu, na kazi ya kusimamia watu pia ni kazi ya kumshinda Shetani, na kazi ya kufanya vita na Shetani. Mungu amepigana vita kwa miaka 6,000, na hivyo kufanya kazi kwa miaka 6,000, ili hatimaye kuleta mwanadamu katika ulimwengu mpya. Wakati Shetani atashindwa, mwanadamu atakuwa amewekwa huru kabisa. Je, huu si mwelekeo wa kazi ya Mungu hivi leo? Huu kwa hakika ni mwelekeo wa kazi ya leo: ukombozi kamili na kuwekwa huru kwa mwanadamu, ili kwamba asiwe chini ya sheria yoyote, wala asiwekewe mipaka na vifungu au vikwazo vyovyote. Kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa kimo chenu na kwa mujibu wa mahitaji yenu, kwa maana kuwa nyinyi mnapewa mnachoweza kutimiza. Sio namna ya “kuendesha bata kwenye sangara,” ya kuwalazimisha kufanya mambo zaidi ya uwezo wenu; badala yake, kazi hii yote inafanywa kwa mujibu wa mahitaji yenu ya ukweli. Kila awamu ya kazi ni kwa mujibu wa mahitaji halisi na matakwa ya mwanadamu, na ni kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kwa kweli, hapo mwanzo hapakuwa na vikwazo kati ya Muumba na viumbe vyake. Zote zinasababishwa na Shetani. Mwanadamu ameanza kuwa asiyeweza kuona au kugusa chochote kwa sababu ya usumbufu wa Shetani na upotovu wake. Mwanadamu ndiye mwaathirika, yule ambaye amedanganywa. Punde tu Shetani anaposhindwa, viumbe watamtazama Muumba, na Muumba ataangalia viumbe na kuweza kuwaongoza binafsi. Haya ndiyo tu maisha ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo duniani. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kimsingi ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na punde tu Shetani anaposhindwa, mambo yote yatakuwa yametatuliwa. Leo, umeona kwamba ni jambo kuu kwa Mungu kuja miongoni mwa wanadamu. Yeye hajakuja kutumia kila siku kutafuta makosa kwenu, kusema hivi au vile, au kwa kifupi kuwawezesha kuona vile Yeye alivyo, na vile ambavyo Yeye huongea na kuishi. Mungu hajakuwa mwili tu ili kuwaruhusu mmtazamie Yeye, au kufungua macho yenu, ama kuwaruhusu kusikia maajabu aliyonena kuhusu na mihuri saba ambayo alifungua. Badala yake, amekuwa mwili ili amshinde Shetani. Yeye binafsi amekuja miongoni mwa watu kwa mwili ili amwokoe mwanadamu, kufanya vita na Shetani, na hii ni umuhimu wa Yeye kupata mwili. Kama haingekuwa ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, basi hangeweza kufanya kazi hii binafsi. Mungu amekuja duniani kufanya kazi yake miongoni mwa watu, kujifichua mwenyewe kwa mwanadamu na kumruhusu mwanadamu kumtazamia; je, hili ni jambo dogo? Ni kweli ni kuu! Si kama jinsi mwanadamu anafikiria kwamba Mungu amekuja ili mwanadamu aweze kumtazamia, ili mwanadamu aweze kuelewa kwamba Mungu ni wa ukweli na wala si yule asiye yakini ama tupu, na ya kuwa Mungu ni wa fahari lakini pia mnyenyekevu. Je, inawezekana kuwa rahisi hivyo? Ni hasa kwa sababu Shetani amepotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu ndiye Mungu anakusudia kuokoa, ya kuwa Mungu ni sharti achukue mwili ili afanye vita na Shetani na binafsi kumchunga mwanadamu. Hii pekee ndiyo yenye manufaa kwa kazi yake. Miili miwili hiyo iliyopatwa na Mungu imekuwepo ili imshinde Shetani, na imekuwepo ili imuokoe mwanadamu kwa ubora. Hayo ni kwa sababu mwili unaofanya vita na Shetani inaweza tu kuwa Mungu, iwe ni Roho wa Mungu au ni Mungu aliyepata mwili. Kwa kifupi, mwili unaofanya vita na Shetani hauwezi kuwa ni malaika, na wala kuwa mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Malaika hawana nguvu ya kuifanya, na mwanadamu ni dhaifu hata zaidi. Kwa hivyo, ikiwa Mungu anataka kufanya kazi katika maisha ya mwanadamu, kama Yeye anataka kuja binafsi duniani kumfinyanga mwanadamu, basi ni lazima Yeye binafsi awe mwili, hivyo ni kusema, lazima binafsi Apate mwili, na utambulisho wa asili na kazi ambayo ni lazima afanye, aje miongoni mwa wanadamu na kumwokoa mwanadamu binafsi. La sivyo, kama ingekuwa ni Roho wa Mungu au mwanadamu ndiye aliyefanya kazi hii, basi vita hivi daima vingeweza kushindwa kutimiza matokeo yake, na kamwe havingelikwisha. Wakati Mungu anakuwa mwili ili binafsi aende kwa vita dhidi ya Shetani miongoni mwa watu ndipo mwanadamu anapata nafasi ya wokovu. Aidha, ndipo tu Shetani anaaibishwa, na kuwachwa bila nafasi zozote za kutumia au mipango yoyote ya kutekeleza. Kazi inayofanywa na Mungu aliyepata mwili haiwezi kutimizwa na Roho wa Mungu, na hata zaidi haiwezi kufanywa na mtu yeyote mwenye mwili kwa niaba ya Mungu, kwa kuwa kazi ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, na ili kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Kama mwanadamu angeshiriki katika vita, yeye tu angelikimbia kwa huzuni ya kuvurugwa, na hangekuwa na uwezo wa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Angekuwa hana uwezo wa kumwokoa mwanadamu msalabani, ama wa kushinda uasi wote wa mwanadamu, lakini tu angeweza kufanya kazi kidogo ya zamani kwa mujibu wa kanuni, au pengine kazi ambayo haihusiani na kushindwa kwa Shetani. Kwa hivyo, mbona ujisumbue? Kuna umuhimu gani ya kazi ambayo haiwezi kumpata mwanadamu, ama hata kumshinda Shetani? Na kwa hivyo, vita dhidi ya Shetani vinaweza kufanywa na Mungu mwenyewe, na haviwezi kufanywa na mwanadamu. Jukumu la mwanadamu ni kutii na kufuata, kwa kuwa mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha kipindi kipya, wala, zaidi ya hayo, anaweza kutekeleza kazi ya kupambana na Shetani. Mwanadamu anaweza tu kumtosheleza Muumba chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, ambapo Shetani hushindiwa; hili ndilo jambo pekee ambalo mwanadamu anaweza kulitenda. Na kwa hivyo, kila wakati vita vipya vinapoanza, kila wakati kazi ya enzi mpya inapoanza, kazi hii inafanywa na Mungu binafsi, ambapo kupitia kazi hiyo Yeye huongoza enzi nzima, na kufungua njia mpya kwa ajili ya wanadamu wote. Pambazuko la kila enzi mpya ni mwanzo mpya katika vita na Shetani, ambapo kupitia hiyo mwanadamu anaingia akiwa mpya zaidi, ulimwengu wa kupendeza zaidi na enzi mpya ambayo inaongozwa na Mungu Mwenyewe. Mwanadamu ni bwana wa vitu vyote, lakini wote ambao wamepatwa watakuwa matunda ya vita dhidi ya Shetani. Shetani ndiye mpotoshaji wa vitu vyote, na ndiye mshindwa katika mwisho wa vita vyote, na pia ndiye atakayeadhibiwa kufuatia vita hivi. Miongoni mwa Mungu, mwanadamu na Shetani, ni Shetani pekee ndiye atachukiwa na kukataliwa. Wale waliopatwa na Shetani lakini hawarejeshwi na Mungu, wakati huo huo, watakuwa wale ambao watapokea adhabu kwa niaba ya Shetani. Kati ya hawa watatu, Mungu pekee ndiye anapaswa kuabudiwa na vitu vyote. Wale waliopotoshwa na Shetani lakini wanarejeshwa na Mungu na wale wanaofuata njia ya Mungu, wakati huo huo, wanakuwa wale ambao watapokea ahadi ya Mungu na kuhukumu wale waovu kwa niaba ya Mungu. Bila shaka Mungu atakuwa mshindi na Shetani bila shaka atashindwa, lakini miongoni mwa wanadamu kuna wale watakaoshinda na wale watakaoshindwa. Wale ambao watashinda ni wale wa Mshindi na wale ambao watashindwa ni wale wa mshindwa; huu ni uainishaji wa kila mmoja kufuatana na aina, na ni matokeo ya mwisho ya kazi yote ya Mungu, na pia ni lengo la kazi yote ya Mungu, na kamwe haitabadilika. Msingi wa kazi kuu wa mpango wa usimamizi wa Mungu unalenga wokovu wa mwanadamu, na Mungu anakuwa mwili kimsingi kwa ajili ya msingi huu, kwa ajili ya kazi hii, na ili kumshinda Shetani. Mara ya kwanza Mungu kuwa mwili ilikuwa ili kumshinda Shetani: Yeye binafsi akawa mwili, na akasulubiwa msalabani binafsi, ili kukamilisha kazi ya vita vya kwanza, ambayo ilikuwa kazi ya ukombozi wa mwanadamu. Aidha, awamu hii ya kazi ilifanywa na Mungu binafsi, ambaye amekuwa mwili ili kufanya kazi yake miongoni mwa wanadamu, ili kusema neno lake binafsi na kumwezesha mwanadamu kumwona. Bila shaka, ni hakika kwamba Yeye hufanya kazi nyingine njiani, lakini sababu kuu ya kufanya kazi yake binafsi ni ili kumshinda Shetani, kushinda wanadamu wote, na kuwapata hawa watu. Na kwa hivyo, kazi ya Mungu kuwa na mwili ni jambo kuu kweli. Kama kusudi lake lilikuwa tu kumwonyesha mwanadamu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na aliyefichika, na kuwa Mungu ni wa ukweli, kama ingelikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi hii, basi hakungekuwa na haja ya kuwa mwili. Hata kama Mungu hakuwa mwili, yeye angefichua unyenyekevu na usiri wake, ukuu wake na utakatifu, kwa mwanadamu moja kwa moja, lakini mambo kama hayo hayana uhusiano wowote na usimamizi wa mwanadamu. Mambo kama hayo hayana uwezo wa kumwokoa mwanadamu au kumfanya awe kamili, na hata hayawezi kumshinda Shetani. Kama kushindwa kwa Shetani kungehusisha Roho tu akipigana vita dhidi ya roho, basi kazi kama hii ingekuwa na thamani ndogo ya ukweli; haingeweza kumpata mwanadamu na ingeharibu hatima na matarajio ya mwanadamu. Kwa hivyo, kazi ya Mungu leo ni moja ambayo ina umuhimu kupindukia. Sio hivyo ili kwamba mwanadamu aweze kumwona, au ili macho ya mwanadamu yaweze kufunguliwa, au ili ampe msukumo kiasi na kutiwa moyo; kazi kama hii haina umuhimu. Kama unaweza tu kuongea kwa hekima ya sampuli hii, basi inathibitisha kuwa wewe haujui umuhimu wa ukweli wa Mungu kupata mwili.
Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza—uumbaji wa ulimwengu—ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, na kama haikuwa hivyo, basi hakuna yeyote ambaye angekuwa na uwezo wa kumuumba mwanadamu; awamu ya pili ilikuwa ukombozi wa wanadamu wote, na pia ilifanywa binafsi na Mungu Mwenyewe, awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii. Kama mwanadamu anaamini tu kuwa Mungu alikuja kuonekana naye na kumfurahisha, basi imani kama hizo hazina thamani, na hazina umuhimu. Maarifa ya mwanadamu ni ya kijuujuu mno! Ni kwa Mungu kutekeleza kazi Yeye mwenyewe ndivyo Mungu anaweza kufanya kazi yake vizuri na kikamilifu. Mwanadamu hana uwezo wa kuifanya kwa niaba ya Mungu. Kwa kuwa yeye hana utambulisho wa Mungu ama kiini Chake, hana uwezo wa kufanya kazi hii, na hata kama mwanadamu angekuwa na uwezo, haingekuwa na matokeo yoyote. Wakati wa kwanza Mungu kuwa mwili kwa ajili ya ukombozi, ilikuwa ni ili kuwakomboa wanadamu wote kutoka kwa dhambi, ili kufanya mwanadamu aweze kutakaswa na kusamehewa dhambi zake. Kazi ya ushindi pia inafanywa na Mungu binafsi miongoni mwa wanadamu. Kama, katika awamu hii, Mungu angekuwa wa kusema tu ya unabii, basi nabii au mtu ambaye ana kipawa angepatikana wa kuchukua nafasi Yake; kama unabii pekee ungesemwa, mwanadamu angechukua nafasi ya Mungu. Lakini ikiwa mwanadamu binafsi angefanya kazi ya Mungu Mwenyewe na angefanya kazi kwa maisha ya mwanadamu, haingewezekana kwake kufanya kazi hii. Ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi: Ni lazima Mungu binafsi awe mwili ili kufanya kazi hii. Katika Enzi ya Neno, kama unabii pekee ungesemwa, basi Isaya au nabii Eliya wangepatikana wakifanya kazi hii, na hakungekuwepo na haja ya Mungu Mwenyewe kuifanya kazi hii binafsi. Kwa sababu kazi ambayo inafanywa katika awamu hii si tu ya kuongea kuhusu unabii, na kwa sababu ni ya umuhimu mkubwa zaidi kuwa kazi ya maneno inatumiwa kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, kazi hii haiwezi fanywa na mwanadamu, na ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi. Katika Enzi ya Sheria Yehova alifanya sehemu ya kazi ya Mungu, ambapo baadaye alinena baadhi ya maneno na kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa manabii. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu angemwakilisha Yehova katika kazi yake, na waonaji wangeweza kutabiri mambo na kutafsiri baadhi ya ndoto kwa niaba Yake. Kazi iliyofanyika hapo mwanzo haikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu moja kwa moja, na ilikuwa bila uhusiano na dhambi ya mwanadamu, na mwanadamu alitakiwa tu atii sheria. Kwa hivyo, Yehova hakuwa wa kuwa na mwili na kujifichua Mwenyewe kwa mwanadamu; badala yake Yeye aliongea moja kwa moja na Musa na wengine, akawafanya wao kusema na kufanya kazi kwa niaba yake, na kusababisha wao wafanye kazi moja kwa moja miongoni mwa wanadamu. Awamu ya kwanza ya kazi ya Mungu ilikuwa uongozi wa mwanadamu. Ilikuwa ndio mwanzo wa vita dhidi ya Shetani, lakini vita hivi vilikuwa bado kuanza rasmi. Vita rasmi dhidi ya Shetani vilianza na kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya kwanza, na vimeendelea hadi leo. Tukio la kwanza la vita hivi ni wakati Mungu aliyepata mwili alisulubishwa msalabani. Kusulubiwa kwa Mungu aliyekuwa mwili kulimshinda Shetani, na ilikuwa mafanikio ya awamu ya kwanza katika vita. Wakati Mungu mwenye mwili huanza kufanya kazi kwa mwanadamu moja kwa moja, huu ni mwanzo rasmi wa kazi ya kumrejesha mwanadamu, na kwa sababu hii ni kazi ya kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ni kazi ya kufanya vita na Shetani. Awamu ya kazi iliyofanywa na Yehova hapo mwanzo ilikuwa tu ya uongozi wa maisha ya mwanadamu duniani. Ilikuwa ndio mwanzo wa kazi ya Mungu, na hata ingawa ilikuwa bado haijashirikisha vita vyovyote, au kazi kuu yeyote, ilikuwa imeweka msingi kwa ajili ya kazi ya vita vijavyo. Baadaye, awamu ya pili ya kazi wakati wa Enzi ya Neema ilihusisha kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ambayo ina maana kuwa Mungu Mwenyewe alitengeneza kwa ustadi kazi ya mwanadamu. Hii ilikuwa ni lazima ifanywe na Mungu: ilihitaji kuwa Mungu binafsi awe mwili, na kama hangekuwa mwili, hakuna mwingine angeweza kuchukua nafasi yake katika awamu hii ya kazi, kwa kuwa iliwakilisha kazi ya kupambana dhidi ya Shetani moja kwa moja. Kama mtu angekuwa amefanya kazi hii kwa niaba ya Mungu, wakati mwanadamu alisimama mbele ya Shetani, Shetani hangeweza kutii na haingewezekana kumshinda yeye. Ilibidi iwe Mungu aliyepata mwili aliyekuja kumshinda, kwa kuwa kiini cha Mungu mwenye mwili bado ni Mungu, Yeye bado ni maisha ya mwanadamu, na bado Yeye ni Muumba; chochote kitakachotokea, utambulisho Wake na kiini havitabadilika. Na kwa hivyo, Yeye alivaa mwili na alifanya kazi ili kusababisha kujisalimisha kwa Shetani. Katika awamu ya kazi ya siku za mwisho, kama mwanadamu angefanya kazi hii na angefanywa kusema maneno moja kwa moja, basi hangeweza kusema maneno hayo, na kama unabii ungesemwa, basi haungekuwa na uwezo wa kumshinda mwanadamu. Kwa kuchukua mwili, Mungu huja kumshinda Shetani na kusababisha kujisalimisha kwake kamili. Yeye humshinda Shetani kabisa, humshinda mwanadamu kikamilifu, na humpata mwanadamu kabisa, ambapo baadaye awamu hii ya kazi inakamilika, na mafanikio yanatimizwa. Katika usimamizi wa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa naibu wa Mungu na kuwa Mungu wakati hayupo. Hasa, kazi ya kuongoza enzi na kuzindua kazi mpya ina haja kubwa zaidi kufanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kumpa mwanadamu ufunuo na kwa kumpa yeye unabii kunaweza kufanywa na mwanadamu, lakini kama ni kazi ambayo ni lazima ifanywe na Mungu binafsi, kazi ya vita kati ya Mungu Mwenyewe na Shetani, basi kazi hii haiwezi kufanywa na mwanadamu. Katika awamu ya kwanza, wakati hakukuwepo na vita dhidi ya Shetani, Yehova binafsi aliongoza wana wa Israeli kutumia unabii uliosemwa na manabii. Baadaye, awamu ya pili ya kazi ilikuwa vita na Shetani, na Mungu Mwenyewe binafsi akawa mwili, kuja katika mwili, ili kufanya kazi hii. Chochote ambacho kinahusisha vita na Shetani pia kinahusisha kupata mwili kwa Mungu, ambayo ina maana kuwa vita hivi haviwezi kufanywa na mwanadamu. Kama mwanadamu angekuwa wa kufanya vita, hangeweza kumshinda Shetani. Jinsi gani yeye angekuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya Shetani wakati bado yumo chini ya utawala wake? Mwanadamu yumo katikati: Kama wewe utaegemea kuelekea kwa Shetani wewe ni wa Shetani, lakini wewe ukimridhisha Mungu wewe ni wa Mungu. Kama mwanadamu angeweza kuwa mbadala wake Mungu katika kazi ya vita hivi, je, yeye angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo? Kama angekuwa na uwezo, je, hangeangamia kitambo sana? Je, yeye si angekuwa ameingia katika ulimwengu wa jahanamu muda mrefu uliopita? Na hivyo, mwanadamu hana uwezo wa kuchukua nafasi ya Mungu katika kazi yake, ambayo ni kusema kwamba mwanadamu hana kiini cha Mungu, na kama ungepambana na Shetani hungeweza kumshinda Shetani. Mwanadamu anaweza tu kufanya baadhi ya kazi; anaweza kushinda baadhi ya watu, lakini hawezi kuwa mbadala wa Mungu katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Je, ni jinsi gani mwanadamu atafanya vita na Shetani? Shetani ataweza kukushika mateka kabla hata hujaanza. Ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye anaweza kufanya vita dhidi ya Shetani, na ni katika msingi huu mwanadamu anaweza kumfuata Mungu na kumtii. Ni kwa njia hii tu ndivyo mwanadamu anaweza kupatwa na Mungu na kutoroka kutokana na vifungo vya Shetani. Kile mwanadamu anaweza kufikia kwa hekima yake mwenyewe, mamlaka na uwezo wake ni kidogo sana; hana uwezo wa kufanya mwanadamu akamilike, kumwongoza mwanadamu, na, zaidi ya hayo, kumshinda Shetani. Akili na hekima ya mwanadamu haviwezi kuharibu miradi ya Shetani, hivyo je, ni jinsi gani mwanadamu awezavyo kufanya vita na Shetani?
Wale wote ambao wamo tayari kufanywa kamili wana nafasi ya kukamilishwa, kwa hivyo kila mtu ni sharti apumzike: katika siku zijazo ninyi wote mtaingia kwenye hatima. Lakini kama huko tayari kufanywa kamili, na huko tayari kuingia katika ufalme wa kustaajabisha, basi hilo ni tatizo lako mwenyewe. Wale wote ambao wako tayari kufanywa kamili na ni waaminifu kwa Mungu, wale wote ambao hutii, na wale wote ambao hufanya kazi yao kwa uaminifu watu wote kama hawa wanaweza kufanywa kamili. Leo, wale wote ambao hawatekelezi majukumu yao kwa uaminifu, wale wote ambao si waaminifu kwa Mungu, wale wote ambao hawajiwasilishi kwa Mungu, hasa wale ambao wamepokea kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu lakini hawaweki mafundisho hayo kwenye vitendo—watu wote kama hawa hawawezi kufanywa kamili. Wote wale ambao wako tayari kuwa waaminifu na kumtii Mungu wanaweza kufanywa kamili, hata kama ni wapumbavu kwa kiasi kidogo, wote hao ambao wako tayari kufuatilia wanaweza kufanywa kamili. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hili. Ili mradi umo tayari kufuata mwelekeo huu, unaweza kufanywa kamili. Mimi sina nia ya kuwacha au kuondoa chochote kati ya hizo miongoni mwenu, lakini ikiwa mwanadamu hajitahidi kufanya vyema, basi utakuwa unajiangamiza mwenyewe; siyo Mimi ndiye ninakuondoa, lakini ni wewe mwenyewe. Kama wewe mwenyewe hutajitahidi kufanya vyema—ikiwa wewe ni mvivu, au hutekelezi jukumu lako, au si mwaminifu, au hufuati ukweli, na daima unafanya unavyotaka, kutumia fedha na kuwa na ushirikiano wa ngono, basi unajilaani mwenyewe, na hustahili huruma ya yeyote. Lengo langu ni kwa ajili ya nyinyi nyote mfanywe kamilifu, na kuwa angalao muweze kushindwa, ili awamu hii ya kazi iweze kumalizika kwa mafanikio. Mapenzi ya Mungu ni kuwa kila mtu aweze kufanywa kamili, na kupatwa naye hatimaye, na kutakaswa naye kabisa, na kuwa mmoja anayependwa na Yeye. Haijalishi kama Ninasema nyinyi ni wa fikra za kurudi nyuma au wa kimo cha umaskini—hii yote ni ukweli. Huku kusema kwangu hakuthibitishi kuwa Mimi nina nia kukuacha wewe, kwamba Mimi Nimepoteza matumaini kwenu, au kwa kiasi kidogo kwamba sina nia ya kuwaokoa. Leo Nimekuja kufanya kazi ya ukombozi wenu, ambayo ni kusema kuwa kazi ambayo Mimi hufanya ni mwendelezo wa kazi ya ukombozi. Kila mtu ana nafasi ya kufanywa kamili: Ili mradi uko tayari, ili mradi ufuate, na mwishowe wewe utaweza kutimiza matokeo, na hakuna hata mmoja wenu ambaye ataachwa. Kama wewe ni mtu wa kimo cha umasikini, mahitaji Yangu kwenu yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha umaskini; kama wewe ni wa kimo cha juu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa kimo chako cha juu; kama wewe ni mjinga na hujui kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa ujinga wako; kama wewe unajua kusoma na kuandika, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa kiwango chako cha kujua kusoma na kuandika; kama wewe ni mkongwe, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa umri wako; kama wewe una uwezo wa kutoa ukarimu, mahitaji Yangu kwako yatakuwa kwa mujibu wa hilo; kama wewe unasema huwezi kutoa ukarimu, na unaweza tu kufanya kazi fulani, iwe ni kueneza injili, au kuchunga huduma ya kanisa, au kuhudhuria mambo mengine kwa ujumla, Ukamilifu Wangu kwako utakuwa kwa mujibu wa kazi ambayo wewe hufanya. Kuwa mwaminifu, kutii hadi mwisho kabisa, na kutafuta upendo mkuu wa Mungu—mambo haya ni lazima uyakamilishe, na hakuna vitendo vizuri zaidi kuliko mambo haya matatu. Hatimaye, mtu anatakiwa kuyafikia mambo haya matatu, na kama anaweza kuyafikia hayo atafanywa kamili. Lakini, zaidi ya yote, ni lazima ujitahidi na kuendelea kwa bidii, na usiwe wa kukaa tu kuelekea hapo. Nimesema kwamba kila mtu ana nafasi ya kufanywa mkamilifu, na ana uwezo wa kukamilishwa, na hii ina umuhimu, lakini iwapo hujaribu kuwa bora zaidi katika ufuatiliaji wako, kama huwezi kuvifikia vigezo hivyo vitatu, mwishowe lazima uondolewe. Nataka kila mtu afaulu kufikia wengine, nataka kila mtu awe na kazi na kupata nuru wa Roho Mtakatifu, na kuwa na uwezo wa kutii hadi mwisho kabisa, kwa sababu huu ni wajibu wa kila mmoja wenu ambao mnapaswa kufanya. Wakati nyinyi wote mmetimiza wajibu wenu, mtakuwa wote mmefanywa kamili, mtakuwa pia na ushuhuda wa kustaajabisha. Wale wote walio na ushuhuda ni wale ambao wamekuwa na ushindi juu ya Shetani na wanapewa ahadi ya Mungu, na wao ndio watakaobaki kuishi katika hatima ya ajabu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi: Maonyesho ya Mungu | "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni