Ijumaa, 11 Oktoba 2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini”


Mwenyezi Mungu anasema, “Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni